Nabii GeoDavie: Biblia sio neno la Mungu bali ni maneno ya wanadamu

Hao mitume na manabii wanajijua wanayofanya ndio maana wanaropoka lengo Lao zaidi ni mshiko na jamaa mtaji kashaupata anatafuta maisha mengine kiaina nje ya udanganyifu wake.
 
Anaamua kuipotosha BIBLIA baada ya uongo wake kufunuliwa. Kaona mbele atakimbiwa na waumini anaamua kwa makusudi kuwaua kiimani wafe kiroho. Hii ndiyo athari ya kukimbilia kwa mitume na manabii feki. Hao nyumbu wana bahati sana kusalimika hapo vinginevyo wakitiwa moto na kufukiwa kama kwa kibwetere na mackenzie. Hawa manabii feki ukiwashitukia janjajanja yao wakiona dili zao zinaenda kufeli huamua kuwakosesha washirika wao wafe kiroho
 
Adheists na kobazi hapa wanafurahia na kushabikia kama fisi aliyepata mzoga mkubwa ale mpaka ashibe. Hii ngoma inajibiwa freshi tu, hakuna hoja hapa nabii anapotosha ukweli. Huu uzi usifutwe ili huyo wakala wa shetani ajibiwe kikamilifu
 
Atheist wamepata hoja toka kwa nabii mkuu. Yule ni mpuuzi fulani anayejua kucheza na akili za nyumbu. Sasa akisema biblia ni maneno ya watu atuambie maneno ya Mungu ni yapi?
Ukisona kwa utulivu falsafa za wagiriki... Socrates, Plato, Aristotle, n.k.... na ukiambiwa kwamba biblia ya kale ilikuwa katika maandishi ya kigiriki.... Huoni taabu kupinga kwamba Biblia ni neno la Mungu, ISIPOKUWA ni hekima ya binadamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…