Salamu za Heri zinaendelea kumiminika. Hapa chini ni kutoka kwa nabii Mwingira:
View attachment 2058365
Salamu za kama hizi zinapoendelea kutufikia ni vyema kujitafakari. Ni wazi kuwa kama Taifa hatuko vizuri.
Walikuwapo kina Desmond Tutu, leo hatuko nao. Walifanya sehemu yao, wamekwenda. Angalia katika kuwaomboleza hakuna dongo hata moja.
"Tunayo ya kujifunza."
Kila mtu kwa nafasi yake anayo sehemu yake ya kufanya, atakayo kumbukwa nayo.
Ni wazi kuwa chuki tunazoziona kwetu ni matokeo ya kumea kwa mbegu zake tunazozipanda wenyewe.
Haki huinua taifa.
Barikiwa mtumishi wa bwana, nabii Mwingira.