Pre GE2025 Nabii Sanga: Mgawanyiko mkubwa utaikumba CCM mwaka 2024 na 2025, tuiombee

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Amesema Mungu amemwambia awaase raia kukiombea Chama Cha MAPINDUZI CCM Kwakuwa mtikisiko wa chama tawala utaathiri pia Nchi Kwa ujumla, na ujumbe wa kukiombea CCM ni Ishara kuwa Mungu BADO anapenda CCM iendelee kuongoza Nchi na amesema kuwa, adui amepanga kutumia mgawanyiko huo kuivuruga Amani ya nchi.
HAELEWEKI ANAUMA ANAPULIZA

Sent using Jamii Forums mobile app
Ujumbe Kwa watu wote lazima uwe namna hiyo.

Soma Aya ya mwisho, amerudia tena kati.😀😀
 
Kama ni hivyo basi sehemu kama Somalia atakuwa amekosea sana?
Rudi kwenye historia,

Mazoea ya kumwaga Damu, Damu ,Damu ilomwagika haiwezi kuruhusu kukoma Kwa matendo hayo.

Ndomana CCM wameitwa kutubu, sababu sauti ya Damu na walioonewa Huwa unadai kiisasi.
 
Salaam, Shalom.

Katika Unabii wa mwaka 2024, Nabii Sanga ametoa ujumbe Kwa Watanzania kuingia katika maombi kukiombea chama tawala CCM, amesema ameambiwa kuwa mwaka huu 2024 kutakuwa na mgawanyiko mkubwa utakaokikumba chama hiki.

Amesema pia kuwa, mgawanyiko na mtikisiko utakaokikumba chama Cha MAPINDUZI CCM, haitakuwa Siri, itakuwa ni mtikisiko wa wazi ambao hata raia wa kawaida watajua.

Amesema Mungu amemwambia awaase raia kukiombea Chama Cha MAPINDUZI CCM Kwakuwa mtikisiko wa chama tawala utaathiri pia Nchi Kwa ujumla, na ujumbe wa kukiombea CCM ni Ishara kuwa Mungu BADO anapenda CCM iendelee kuongoza Nchi na amesema kuwa, adui amepanga kutumia mgawanyiko huo kuivuruga Amani ya nchi.

Amesema pia, amepata ujumbe kuwapa Marais wote wa Africa kuwa Waaminifu Kwa Nchi zao na kuwatumikia wananchi Kwa HAKI, la sivyo, patakuwako maandamano katika Nchi nyingi Afrika ikiwa hawatakuwa Waaminifu.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni.🙏

Source: POG family Tv.
Sanga ni mmbea tu kama Prof. Janabi
 
Nabii wa mchongo

Sent using Jamii Forums mobile app
20231224_095052.jpg
 
Rudi kwenye historia,

Mazoea ya kumwaga Damu, Damu ,Damu ilomwagika haiwezi kuruhusu kukoma Kwa matendo hayo.

Ndomana CCM wameitwa kutubu, sababu sauti ya Damu na walioonewa Huwa unadai kiisasi.
Nimeuliza huyo ''mungu'' anayeongolewa kwenye hii thread huko Somalia vipi? Kwa wapalestina vipi? Kwa nini awape tu CCM chance ya kutubu?
 
Mpk sasa Kuna mtikisiko. Makonda hatakiwi na viongozi waandamizi wa ccm karibu wote . Sijui mama kamteua wa nn huyo muuaj!!!!?
 
Salaam, Shalom.

Katika Unabii wa mwaka 2024, Nabii Sanga ametoa ujumbe Kwa Watanzania kuingia katika maombi kukiombea chama tawala CCM, amesema ameambiwa kuwa mwaka huu 2024 kutakuwa na mgawanyiko mkubwa utakaokikumba chama hiki.

Amesema pia kuwa, mgawanyiko na mtikisiko utakaokikumba chama Cha MAPINDUZI CCM, haitakuwa Siri, itakuwa ni mtikisiko wa wazi ambao hata raia wa kawaida watajua.

Amesema Mungu amemwambia awaase raia kukiombea Chama Cha MAPINDUZI CCM Kwakuwa mtikisiko wa chama tawala utaathiri pia Nchi Kwa ujumla, na ujumbe wa kukiombea CCM ni Ishara kuwa Mungu BADO anapenda CCM iendelee kuongoza Nchi na amesema kuwa, adui amepanga kutumia mgawanyiko huo kuivuruga Amani ya nchi.

Amesema pia, amepata ujumbe kuwapa Marais wote wa Africa kuwa Waaminifu Kwa Nchi zao na kuwatumikia wananchi Kwa HAKI, la sivyo, patakuwako maandamano katika Nchi nyingi Afrika ikiwa hawatakuwa Waaminifu.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA [emoji1241]

Karibuni.[emoji120]

Source: POG family Tv.
Iko shida wenyewe kwa wenyewe waendelee tu sisi tunatizama
 
Wewe huoni haja ya CCM kutubu?

Au ukakasi umekuingia uliposikia CCM iombewe?
CCM itubu na kuombewa ili iweje? Wanaopaswa kuombewa ni chawa wote wanaokiwezesha na kushabikia kikundi cha mashetani, wala rushwa na mafisadi kubaki madarakani akiwemo huyo nabii wako anaefikiri bila CCM nchi haitakuwa na amani!!
 
Mungu ana ubia Gani na CCM mpaka akwambie uwaombee.

Ili iweje Sasa,wabaki madarakani au vipi?
Maana kama ni hivyo Mungu anaweza hiyo kesi kumaliza hata bilaa maombi yetu
 
Ikiwa huamini manabii,

Kwako wote ni WA mchongo.

Bt karama ya unabii Kwa waliookoka Kila Kanisa, lazima awepo mwenye karama ya unabii.
Rabbon nimeishi na asilimia 90 ya manabii wa ndani na nje ya nchi.. Cover unayoiona mbele ya madhabahu zao kwenye camera ni tofauti kabisa na kilichomo nyuma ya pazia zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom