KERO Responded NACTVET wana huduma mbovu katika kuwasiliana na wateja wao

KERO Responded NACTVET wana huduma mbovu katika kuwasiliana na wateja wao

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nina malalamiko yangu kwa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kuhusu huduma ya mawasiliano kwa wateja.

Kumekuwa na changamoto kubwa ya kutopokelewa simu tunapowasiliana na ofisi zao kwa ajili ya kupata msaada au ufafanuzi wa masuala mbalimbali. Mara nyingi unapiga simu kwa muda mrefu, wakati mwingine hata kwa zaidi ya saa moja, lakini hakuna anayepokea. Hali hii inasababisha usumbufu mkubwa kwa wanafunzi, wazazi na wadau wengine wanaohitaji huduma kutoka NACTVET.

Kwa kuwa wengi wetu tunatoka mikoani na tunategemea mawasiliano ya simu kabla ya kufanya safari za kwenda ofisini, kutopatikana kwa huduma hii kunatuongezea gharama na usumbufu usio wa lazima. Inasikitisha kuona namba za huduma kwa wateja zikiwekwa wazi ilhali hazijibuwi au hazitumiki ipasavyo.

Ushauri wangu ni kwamba NACTVET iboreshe huduma zake za mawasiliano kwa kuhakikisha simu za wateja zinapokelewa kwa wakati na majibu yanatolewa kwa ufanisi. Vinginevyo, ni bora kutoa taarifa rasmi kuhusu njia mbadala za mawasiliano ili wananchi wajue namna sahihi ya kupata huduma badala ya kupoteza muda mwingi kupiga simu zisizopokelewa.

Tunaiomba NACTVET kulifanyia kazi suala hili kwa haraka ili kuboresha huduma kwa wananchi na wadau wake.

Pia soma ~ NACTVET: Tumefanya maboresho ya mawasiliano kwa njia ya simu ili kuongeza ufanisi
 
Mkuu control namba hutumwa baada siku ngapi ili kulipia huduma ya application?
 
Kwanza mfumo wao mtandao uko slow sometimes haufanyi kazi kabisa.
Appmication za tarehe 7 wanatuma code leo tareh 10.
Control number za tareh 7 hazionekani mpaka leo.
Unaambiwa Click here, ukiclick unarudishwa kule kule hakuna kitu.
Mtandao mbovu huduna mbovu hawapikei simu, wakijitahidi sana utakuta wanatumika na mwisho watakukatia.

🧐💔
 
Kero yangu inaenda kwa Taasisi ya NACTVET na TCU kuwa simu zao za mawasiliano tunapokuwa tumepata shida hawapokei simu zetu hasa NACTEVT hii ni kero kwa watu tunaomba msaada wenu kutufikishia ujumbe huwezi kupiga simu kuanzia asubuhi mpaka jioni hampokei kama hawawezi kazi waachie Ofisi.
 
Kero yangu inahusu Taasisi ya NACTVET na TCU, kuwa simu zao za mawasiliano tunapokuwa tumepata shida hawapokei, hasa NACTEVT hii ni kero kwa watu tunaomba msaada wenu kutufikishia ujumbe huwezi kupiga simu kuanzia asubuhi mpaka jioni hampokei kama hawawezi kazi waachie Ofisi.
 
Back
Top Bottom