Nadhani mimi ndie mwanamke mwenye sifa mbaya kuliko wote JF

Kwa vile umeshapoteza imani nae hata nikikuelezea huwezi niamini,mbaya zaidi we mwenyewe unauwezo wa kuchagua jema na baya,...We simama upande unaoupenda ninachoona unapata tabu ni hapo kujifanya unampenda na kumuamini kumbe hauko hivyo,hayo ni mates unapitia,simamimia unachoamini hayupo hayupo haina haja ya ku praise nothing,be real....
 
Angalau nimefarijika kusikia bado una ubinadamu ndani yako

kama hautaweza kuhubiri ukweli juu ya uwepo batili wa Mungu, mbingu, shetani na uchawi basi ni bora uachane kabisa na maswala ya dini na mahubiri

Tafuta chanzo kingine cha pesa ambacho kitakidhi mahitaji yako na ada ya kijana wetu he deserves better, na natumaini unamsomesha international school kutokana na tuition fee uliyoweka hapa

Hata mimi ni atheist, nilisoma seminary kabisa nimekaa sana na mapadre kanisani lakini baada ya kukua na kufikiri logically nikajikuta siamini tena kwenye maswala ya imani ni uongo na utapeli uliotukuka, sio mama wala rafiki zangu walinichukia kwa kubadilika na kupinga mawazo yao.

be real, be the change.
 
Am very straight.
I do men.
Napenda harufu ya mwanaume,
Wana jasho lao fulani hivi.😁

Swali lako la mwisho tuli delete my naona hatupaswi kuulizana hayo🙏
Nimekuuliza hivyo maana umeandika kana kamwa you are more than alone
 
Mtumishi,ila sisi unavyotuambiaga tutaenda motoni tuache kunywa ka wine nyieeeee
Watu wanaambiwa shika neno usofate matendo yangu ila hawajiongozi😁

Tena mwanzoni kabla sijazoea macho ya watu nilikua nabeba wine yangu kwenye chupa ya eneji then napiga pafu zangu kadhaa ndo napanda madhabahuni🙏🙏
 
Ndo naanza hivyo taratibu
Nikikutana na kina Kiranga
mara 3 tu nitakua level zingine
Its a process nitafika tu huko.
Asilimia 94 ya kipato changu hakihusiani na kanisa.
 
Watu wanaambiwa shika neno usofate matendo yangu ila hawajiongozi😁

Tena mwanzoni kabla sijazoea macho ya watu nilikua nabeba wine yangu kwenye chupa ya eneji then napiga pafu zangu kadhaa ndo napanda madhabahuni🙏🙏
Ha haaaa aloooooh!ina maana mnavyoimbaga vile worship kumbe mmekuwa mmeonja kitu kali?
 
Asante kwa maoni mkuu ila nikiwaza kwa mapana kama ulivyonishauri ndio naona kabisa kuwa hakuna Mungu
 
Maisha magumu hutupatia empathy ambayo tunaokutana nao baadae huona ni symbol ya weakness na ku take advantage.

Very touching story.
 
Za uzima mkuu.
Niliahidi nitakujibu maswali yako yote.
1)Wakati huo nilikua bado naamini tena kwa imani kubwa sana kuwa kuna Mungu ajibuye maombi.

2)Ni kweli nasoma sana biblia na ni kweli nafahamu kuhusu hiyo "dhambi" ila hiyo hainitishi sbb siku nikifa ndio habari yangu imeishia hapo.Paradiso na moto wa jehanamu ni hadithi zinazonichefua sana.Watu wanaacha kutumia miaka michache ya kufurahia maisha hapa duniani kisa wametishwa kuna moto.Watu wanakufa kwa kudanganywa kuna Mungu anayeponya na kupuuzia tiba halisi.Paradiso na kuzimu viko hapa duniani.Tukifa wote tunalala mpaka pale science itakapoamua iwe tofauti.

3)Hilo nishaelezea kwenye uzi na kwenye reply nilompa ferucho lamborgini

Asante kwa ushsuri ila kwa vile unaamini Mungu yupo naomba umshauri Mungu kuwa amuondoe shetani duniani mana sioni ni kwanini anataka tujaribiwe?Au hawezi kumtoa?,Kama kamshindwa sisi ndio tutamuweza?

Basi kama kamshindwa shetani mshauri kuanzia sasa aumbe version ya wanadamu ambao haiwezi kujaribiwa wala kuanguka dhambini.

Pia mshauri atimize ahadi zake na awe sawa kwa wote.Sielewi kwanini kuna wanaoteseka na upofu na wengine wazima.Sielewi kwanini wengine wanalelewa na kukua wakipata malezi na upendo ya baba na mama na wengine anaua baba na mama zao.
Kwanini kuna baba "anabarikiwa" uwezo wa kuwapa watoto wake kila kitu na wengine wanazika watoto wao kwa kukosa elfu tano ya dawa?

HAKUNA MUNGU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…