mkuu nina maswali mengi sana kutoka kwako, na ushauri pia
maswali:-
1. umesema ulianza kuwa atheist tangu ukiwa primary, unataka kuniambia ww huamini uwepo wa Mungu na bado uliweza kwenda kanisani kusali usiku kucha mpk magoti yakauma leo hii uje useme huamini uwepo wa Mungu, ulikua unamuomba Mungu yupi sasa?
2.nafahamu unasoma sana biblia, na unaifahamu dhambi ya kumkufuru roho mtakatifu haisamehewi..unafahamu kwamba unachokifanya hapo ni kutaka kuitenda iyo dhambi kwa maana mwisho wake unamkana Mungu na Yesu kristo unayemtaja kwene mahubiri yako kanisani?
3. kama umeamua kuwa atheist kwann usiache kuhubiri na bado unaendelea?
ushauri;-
Naamini ww ni mtu wa Mungu na anakutumia sana kuifanya kazi yake, hayo mawazo uliyonayo ni hila za shetani kukupoteza ktk mstari, nakushauri utubu hiyo dhambi na umrejee Muumba wako, watu wengi hapa wanakushauri ujinga tu kwamba endelea na maisha hayo na ufurahie, wote huo ni ubatili mtupu