Nadharia ya Usalama wa Taifa (TISS) ibadilike kuanzia sasa, Taifa lipo hatarini

Status
Not open for further replies.

What kind of reforms would you like to see? Are the reforms you want viable to our socio-economic and cultural conditions?
 
TISS tatizo ni sheria dhaifu. Serikali inahakikisha kuwa sheria ziko dhaifu ili waweze kuwadhibiti watu wa TISS.

1. Kuna haja ya kuisuka tena upya taasisi hii HASA KWA KADA YA CHINI kwa kuwapatia mafunzo mazuri zaidi ya NIDHAMU. Wafanyakazi wengi wa TISS wana tatizo kubwa sana la nidhamu.

2. Majukumu yao yasizingatie nani anamjua nani. Professionalism ijengwe, itunzwe kwa maslahi ya Taifa na sio kwa maslahi ya watawala.

3. There is enormous amount of bullying/discrimination/ and other malpractices in this department that need to be sorted out.

4. Kwa sababu hakuna sheria zilizo wazi hasa kwa wafanyakazi wa kada ya chini TISS wenyewe, na hasa kwa sababu ya style yao ya slavery(creating dependency for your master to rule efficiently), hali iliyozaa kuwa wana TISS wengi kuishi kwa kutegemea rehema za maboss wao.

5.TISS ni jeshi. Lakini imekuwa ikitumiwa kama kitengo cha propaganda cha serikali.

Lakini wakati huo huo kukiwa na vuta nikuvute kati ya serikali na TISS kila mmoja akitaka kumweka mateka mwenzie! (TISS wakitaka pesa kwa kuzusha uongo/prpaganda wakati serikali inataka TISS kufanya kazi zake chafu - TISS wakiamini ni wajibu wao.
 

kutoa Attributes hakukupunguzii maarifa kijana wa Masters ya India, live like a truly Masters graduated buddy!
 
Wengi humu JF hatujui kitengo hiki kinavyofanyakazi zake...Napenda niwahakikishie kuwa TISS haifungwi haijafungwa na haifungamani na taasisi, jumuiya ama chama chochote cha siasa. Method operamond ya TISS inatanguliza maslahi ya Taifa mbele. Mkiona vya elea mjue kuna watu hawalali wanapigania nchi yao yenye neema nyingi na yenye kuvutia maadui wa kila aina...Wengi wetu humu tuko projected! tunaamini tunachokiona na nirahisi kudanganyika kwa kudhani kuwa ni halisi! Adui hana sura inayotambulika, wanaweza kupitia milango ya kutoa misaada, makanisani, misikitini, kwenye taasisi ya elimu nk nk...
Kazi za TISS ni nzito na hatusababishi makelele kwakuwa hawatangazi biashara, hivy hofu ya kusema kuna tatizo la uongozi ni -Ve, Technologia TISS iko juu sana, Kimuundo TISS iko sawa, Watu wenye ueledi uliotukuka wapo wengi... Nchi hii itaendelea kuwa salama chini ya TISS kwa miaka mingi ijayo....
 
Hakuna kitu hapo, wangekuwa wanafanya kazi mambo yangenyooka tanzania, tatizo wamekuwa wala rushwa mstari wa mbele,kila mtu anaangalia hela na sio kazi, ni kama ilivyo polisi. hata wakikamata deal leo litaishia kugawana... usalama ulikuwa zamani bwana....ndg yangu ukitaka kujua hilo nenda bandalini usalama wapo lakini hivyooo, nenda mipakani usalama wapo lakini wizi mtupu kaririila siku wanaharamu wanapita... nenda airport deal kama kawa na usalama wapo ndani, mnaowafagilia hamjui kiendeleacho, kilichobakia tanzania ni usalama wa viongozi tu na si usalama wa taifa... maana hapo bandarini kila siku deal feki, meno ya tembo na kadhalika vinapita...chezea bongo wewe
 
Nini kifanyike kuondoa hali hiyo unayodai ipo mkuu?
 
Hebu nikuulize swali Officer, kama sikosei Hans Kitine ndio alikuwa Boss wa TISS, lakini ni kitine huyo huyo aliyefoji invoince ya matibabu ya mke wake ili kuiba pesa za umma, sasa kama Boss ndio anakuwa namba moja kuhujumu maslahi ya umma hawa wengine hali ikoje?
 

Naomba ni kuhakikishie kuwa kila habari unayoipata si zote ni sahihi na zinaukweli...kama kuiba pesa za umma angeweza kujichotea kimya kimya mzee wa watu bila ya mtu yeyote kuhoji, hili la kufoji risiti ni muendelezo wa majitaka ambayo siku zote hutoa harufu mbaya ...
 
And your point is!!...
 
kutoa Attributes hakukupunguzii maarifa kijana wa Masters ya India, live like a truly Masters graduated buddy!

Mwenzio ametoa mchango wake wenye manufaa wewe unaleta vivu wa kike...kama huna la kuchangia chapa lapa! unataka masters ya SAUT ndo uje yeye ni msomi? shwain wewe...
 
Kitu ambacho mnapaswa kuelewa nikwamba usalama wataifa imekuwa ni kapu lawalio feli shule na maisha.

Mkubwa yeyote mwenye mtoto au ndugu aliye feli shule au maisha mtaani maisha yamemshinda anaunganishiwa usalama wataifa. Hii ni aibu kubwa sana kwa taasisi yenye majukumu nyeti kama hii. Imekosa kabisa mwelekeo na maana hasa kipindi hiki cha awamu ya jk.

Utakuta vijana mtaani wanalewa ovyo na kujigamba eti ni usama wataifa. Wengine tumesoma nao shule na wakafeli leo hii unawaona kwenye misafara ya viongozi wa nchi.

Chaajabu zaidi maadili yakazi hakuna utawakuta wana pepeta umbea na kuvujisha siri za ofisi! Sijui tutafika wapi kama kweli hali ndo hii.

Waneshindwa kabisa kusimamia sheria na taratibu zinazo waongoza na kuanza ushabiki wa siasa.

Utasikia mtu anajiita usalama wataifa anasema chadema hawaendi popote, hawana ujanja kwani kule tumejaza vijana wetu wa usalama wataifa! Unajiuliza kazi ya usalama wa taifa ni kuitumikia ccm au maslahi ya nchi?

Sasa usalama wataifa umegeuka kuwa chama cha siasa badala ya taasisi yauma? Nilazima hii taasisi iondoke chini ya mwenekiti wa ccm yaani ikulu na iwe huru kwa maslahi ya uma na sio ccm! Hii ni aibu sana kwa nchi.
 
Mwenzio ametoa mchango wake wenye manufaa wewe unaleta vivu wa kike...kama huna la kuchangia chapa lapa! unataka masters ya SAUT ndo uje yeye ni msomi? shwain wewe...
sio mchango wake bali ni kazi ya mtu aliyeigeuza yake tuliyokuwa tunaongelea humu ndani kuhusu Dr Shayo ndiyo yanafanywa na kijana wa masters toka india sasa!
 
Well, tunaweza kusema mengi sana ya kwamba usalama wa taifa wamepoteza dira ama la. La msingi ni kwamba sheria ya usalama wa taifa inawabana. Usalama wa taifa wanariport kwa president, na president ndio anatoa maelekezo kwa vyombo husika vya usalama kama jeshi la polisi, mahakama ama JWTZ. Kwa hiyo umahili wa president ndio unaamua kama usalama wa taifa uonekane uko makini ama la. Lakini pia wao ni washauri tu, kwa lugha nyingine ni watafuta taarifa na kuzitoa, basi. Kama kuna la kufanya mpaka waelekezwe kufanya hivyo.Hii ni sheria inayowabana, na inawafanya waonekane mambulula pindi tuwapo na president mbulula. Naamini jamaa wanakusanya taarifa na kuzifikisha mahali husika, utekelezaji wa taarifa hizo ndio tatizo. Hiyo pekee inatosha kuwakatisha tamaa hivyo kuwapelekea kufanya kazi kivivu.Turekebishe sheria, usalama watafanya kazi yao, wako poa
 
Mkuu Yericko umeongea sana. What do u think would be wayfoward mzee??

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Inashangaza yani Usalama wa Taifa hawana mamlaka ya kuarest? basi TRA ni zaidi ya Usalama wa Taifa maana kuna maofisa wao wa juu wana mamlaka ya kuarest in the manner of TAXES issue.
 



Mkuu ueledi wa TISS ulionekana pale;

(1) Tulipouziwa radar kwa bei ya kuruka.
(2) Wezi wa EPA kushindwa kukamatwa
(3) Twiga kubebwa wazima wazima pale KIA
(4) Shimbo kujichotea yale matrilion atakavyo
(5) Wauzaji wa madawa ya kulevya kuendelea kutembea vifua mbele hapa mjini etc....

Ila kazi ya kuwatoa wananchi meno, kucha na sasa macho inaonekana. Nawapongeza sana TISS, najua majukumu yenu...
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…