Nafasi ya Kazi Morogoro Mjini Mshahara 180,000/= + Internet ya bure

Nafasi ya Kazi Morogoro Mjini Mshahara 180,000/= + Internet ya bure

Kwa kijana anayeishi karibu na ofisi hii itamfaa. Kuna watu wanaponda hiyo ajira wakati wao hawajawahi ajiri mtu kwa huo mshahara.

Sio kila ajira ni ya kukutajirisha, nyingine ni kama stepping stone. Kuna watu hata pesa ya vocha na kununua chupi hawana.
 
Wengi wataomba iyo kazi ila tegemea 70% ni tamaa,ugumu wa maisha na mwishowe lazima watakaobahatika au kubahatika atapiga tukio kama si kuondoka na mauzo basi atasepa na mtaji
1. Ukiona kazi inatangazwa (hizi za ofisi ndogo ndogo, binafsi) basi kuna uwezekano mkubwa imeshawashinda wengi. Mtego ulioko kwenye hili tangazo ni muda wa kazi. Hakutaja!
 
Malaya wanawaza beer Kwa tsambelakisi hawapajui.
 
Imagine kuna muda kwenye maisha yangu nikiwa na degree nilipoteana mpaka nikawa natamani kazi ya chini ya mshahara huu. Lakini sasa mshahara huu ninaupata kwa chini ya siku moja. (Si ajira ni biashara binafsi).

Kwa yeyote unayepambana usikate tamaa, muda (time) ni jawabu la mambo yote.
 
Anahitajika binti mwenye uwezo mkubwa wa kutumia simu na computer.

Ofisi yetu inafanya kazi 2 ambazo ni kutoa huduma ya internet Morogoro mjini na kukata tiketi za treni ya SGR.

Anahitajika mdada smart anayefahamu kutumia computer na simu vizuri, awe sharp na asiye na hasira za hapa na pale maana kuna wateja wanachosha.

MAJUKUMU
1. Kukata tiketi za SGR kwa wateja wanaofika ofisini na wanaopiga simu (utaelekezwa).
2. Kuwaunganisha wateja wanaohitaji huduma ya internet ili kupata huduma hiyo kwenye simu zao.
3. Kukusanya malipo kwa wateja wetu wanaolipa kila siku. Wewe unapita tu ofisini kwao, unachukua hela unaleta ofisini, wale wabishi unakuja kuwaripoti.

Mshahara ni 180,000/=
Ofisi kali sana, full AC na internet yenye kasi kama yote unatumia hadi unachoka.

Maombi yatumwe kupitia Whatsapp no
+255758616614

NB: Lazima ujue kiswahili fasaha na kiingereza, pia uwe smart kuanzia akilini hadi mwonekano.

Ofisi iko Morogoro mjini.
internet imekuwa ni sehemu ya mshahara.
 
Back
Top Bottom