Nafasi za Ajira za muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Tu share uzoefu kwa ambao wameshafanyiwa usahili tafadhali

Naanza mimi😀story kidogo

Nilikuwa kwenye daladala nmechelewa sana eneo la usahili,sababu majina nliyaona saa 10 jioni halafu yanasema usahili ni kesho,mimi nlikuwa Morogoro - usahili unafanyika Tabora imagine,nkasema ok- ngoja nijaribu

Saa mbili usiku nkapata lori😀limetembea usiku mzima,dereva kulipokucha ikabidi nimueleze kinachoniwahisha- alikuwa humble sana,tulifika mahali akanisimamishia daladala ili niwahi( Hapo saa sita mchana,usahili naulizia huko nakoenda ushaanza)


humo kwenye kwenye daladala nkakuta watu wawili,mkaka na mdada- wametoka kwenye usahili,sura zao zikiwa hazina matumaini(nliwagundua baada ya story zao)

wanasema,hapa tulikuwa tunatoa ushahidi tu,maana maana walivyohojiwa kana kwamba kuna watu walikuwa prepared na hao walikuwa wanasema ni walimu.,walifanyiwa usahili na walimu wakuu- na walimu wa kawaida walikuwa wanapewa priorities "iweje mwalim mkuu awaache walimu wake anichukue mimi,sidhani" story zao

mimi humo kwenye daladala nikawa najiuliza,nimechoma nauli yangu kubwa kwa hili! anyway ngoja nifike.

Ile nashuka kwenye daladala saa nane mchana,nikauliza mtu kama wanaendelea au nisubiri kesho.. akasema wanaishia leo tu. Na wamebaki watu wawili😀😀ni mbali bado.,nikachukua boda elf8 kwenda site,nlikuta watu washaisha wanajiandaa kutoka. Nikawaambia mimi bado,ok wakaitikia karibu,

cha kwanza wananiuliza,wewe ni mwenyeji wa wapi? nikawajibu (sehem nliyoomba)

Pale kulikuwa na watu wa3-wakaniuliza unamjua nani kati ya hawa? kusema ukweli sikuwa namjua mtu sabab sijakaa muda eneo husika.(wakasema basi wewe ni mzaliwa lakini hukai huku- huyu mzee mmoja anaonekana mwalim mkuu+ mnoko.

wakaomba vyeti-nikawapa,vyeti vinaonesha nmesoma sehem nyingine lakini nikawaelewesha-hapo hapakuwa na shida - vyeti vilikuwa vizuri saana vyote o'level + A'level,birth certificate ilionesha nmezaliwa pale nlipoombea

Maswali mengine ni kama nmewahi kutumia smartphone,

Endapo iki stack ntafanyeje

Sensa ngapi zimefanyika,

Ikiwa nitachaguliwa kwenye mafunzo,na ikawa free nitafanya?

Napenda kufanyia sehem gani na kwanini

Ofcourse majibu yangu yaliwa encourage kidogo,wale wawili ispokuwa yule mzee(alikuwa haniangalii hata)😂😂.

Nlikuwa nmevaa tshirt +jeans(jeans ya kawaida kila mtu ana vaa)+ raba
Nywele zilikuwa zimevurugika kidogo-sikupata muda wa kujiandaa

Nguo nlizoziandaa kwa ajili ya interview sikupata mda wa kutupia😀

Anyway nlijibu vizuri,
 
ukipata usinisahau mwenzio hata kapepsi.
 
napapendaa sanaa tanga maana sijawahi fika ,nataka huko nije kula demu kimasihara maana huko nasikia mambo si mambo pisi kali za kutoshaaa na wajuzi wa mambo nikipata pesa nitakuja kujivinjari kidogo huko aisee nione dunia ya huko inakwendaje.
Hahahaha Kijana ukija utumie kinga au upime nao pia usijetongoza wake za watu ukajulikana
 
Daaa nimeipenda hiyo allocation
Sisi tulipigwa laki nne out of 1.2M ada na meals and accommodation imeisha hiyo tangu niende chuo hakuna nguo mpya ni maden tu
Tumaini langu ni sensa
 
Mna uhakika gan kama hao mlowatuma kusimamia usaili wametenda haki?
 
Hizo marks 50 wanazitoa vipi?ikiwa kuna wengine wameulizwa maswal mawil, wengine matatu tuu. Wengine manne?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…