ILALA WAMEAMUA UGOMVI
Tulianza kama utani kukimbizana kutafuta fingerprint za wadhamini, tukasubiri Kwa muda mrefu hatimaye mkeka wa kwanza ulitoka Jina langu likawemo, kama mjumbe mmoja alivyosema kwenye Uzi wa Mamba Vs predators akasema eti kwakuwa mamba anataga basi hastahili kuingiankwenye Hilo kundi, Kuna mjumbe akasema usiombe ukutane na mamba wa mto Nile, Ndio kilichonipata Jina langu likakutwa na hao Mamba, linatafunwa huku mamba chozi Lina mtoka, kiufupi nimeliwa kichwa.
Nitumie fursa hii kumshukuru Mungu Maana maandiko yametuasa kumshukuru Kwa kila jambo, lakini pia niwashukuru wote ndani ya huu Uzi Kwa kutumia vifurushi au VPN mkaleta update ya kinachoendelea huko vyumbani. Ramli zote chonganishi zilipelekea watu wakataka kutoana ngeu.
Niwape pongezi wote ambao wamevuka Salama nawaasa Wakachape kazi, uvivu hautakiwi, na posho wazitumie vizuri hatutaki kusikia Tena ooh hatuna mitaji yakujiajiri, mitaji hiyooo msihonge kawekezeni. Wengine maisha lazima yaendelee wengi walikuwa wanazipigia hesabu hizo hela, usiihesabie Hela ambayo sio yako utaishia kukata tamaa.
Naomba kuaga rasmi kutoka kwenye huu Uzi.
TUJIANDAE KUHESABIWA