Huko telegram nilipewa code ya wadau wa Free internet na Vpn Tz kuna nimekuta kuna members zaidi ya buku mianne Kazi kuombana free Vpn na kupeana michongo ya kuperuzi kea gharama nafuu , nikasikitika sana jinsi hali ilivyokuwa ngumu nchini na watu wanavyopambania kutafuta unafuu
Mimi nina Vpn mbili za kunisaidia gugo na wasap wakati wa emergency nikiwa nimepigika ila zipo slow kukonect kwa mbinde wakati fulani sio kama zile Sky Vpn na Ec Tunnel ambazo nilikuwa napeta nazo mpk Insta na YouTube bila kukwamakwama.