Nafasi za Ajira za muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Nafasi za Ajira za muda za Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Kutokana na ufinyu wa vigezo vya hz kazi nilijua watu watakaoomba watafika milioni plus, Ila kwa muendelezo huu hata Laki 6 hawatofika.. na inaonesha robo ya waombaji watakuwa wametuma maombi kimakosa.. just imagine wengine hawana namba za NIDA, vyeti vya kuzaliwa.. But Kila la kheri Wasakatonge
Tatizo masharti mengi halafu magumu hizi ajira watu hawatatosha na wataishia kuchukuana wenyewe tu ndiyo maana hata wameongeza mda
 
kwa wale watu wanaopata changamoto ya kutuma maombi na kushindwa kupata form au kupata ujumbe wa aidha namba ya simu email nida au namba ya form four imetumika fuata taratibu hizi kupata form au password

1. jaribu kupiga simu wakipokea waambie changamoto unazozipata watakutatulia ila hapa ni kazi sana simu yako kukielewa.

2. kama una jamaa au ndugu yako yuko dodoma mtume aende NBS akakuchukulie password yako hii njia ni 100% leo mimi nimetuma mdogo wangu wakampa password na form tayari nime print.
 
Kwenye kuchagua mkoa napata machaguo vizuri ila kuanzia wilaya, halmashauri, jimbo, n.k machaguo hayaji na nikiandika kwa kawaida hayakai. Vipi shida ni nini hapo? Nifanyeje kuendelea??
Bonyeza halafu subiri kidogo yatajionyesha baada ya mda
 
WANAWEZAJE KUPROVE KAMA FINGERPRINT NI ZA WADHAMINI KWELI? kama maombi yenyewe ndio hayo zaidi ya laki
Huo muda wa kukagua madole gumba wanaupata wapi ratba yenyewe inawabana
 
Wewe Fanya unachoweza kufanya hayo mengine achana nayo,,mbona unaumiza kichwa mambo ambayo hufaidiki nayo!!!!
Sifaidiki nayo kivipi wakati mimi ndio ninaapply na hao wadhamini wanazingua kwenye fingerprint? ndio maana nataka nijue kama ni lazima sana
 
Watakaochaguliwa majina Yao yatatumwa kwa watendaji au kwenye email zetu? Naomba msaada wa majibu
Nilivyoambiwa na mtendaji (rfk angu)
Huko utumishi watachagua kulingana na vigezo,then watayatuma kwa maafisa utumishi wa mkoa,kila mkoa/wilaya!
Then wao nao watachagua kwahiyo ni yaleyale!.
Mi hata siombi!
Nimechoka
 
Iv Kama mwanzo haukuweka kiambatanisho kingine .. kweny ku update unaweza kukiattach?
 
kwa wale watu wanaopata changamoto ya kutuma maombi na kushindwa kupata form au kupata ujumbe wa aidha namba ya simu email nida au namba ya form four imetumika fuata taratibu hizi kupata form au password

1. jaribu kupiga simu wakipokea waambie changamoto unazozipata watakutatulia ila hapa ni kazi sana simu yako kukielewa.

2. kama una jamaa au ndugu yako yuko dodoma mtume aende NBS akakuchukulie password yako hii njia ni 100% leo mimi nimetuma mdogo wangu wakampa password na form tayari nime print.
Sorry mkuu.
Wamemuuuliza viambata vip ili na mmi nimtume ndughu yangu
 
Back
Top Bottom