Nafasi za kazi Jeshi la Polisi Tanzania

Nafasi za kazi Jeshi la Polisi Tanzania

Kule unaishi kama mzuka mda wote mimi kuruta " mimi kuruta"

Mda wowote unaogopa kujichanganya ukaaga mashindano na asikwambie mtu hivi unajua maisha ya uoga ya kuwindana kama digidigi yalivyo ? [emoji3]


Ukiumwa kidogo malaria we tayari unfit , buti hujapiga kiwi we tayari ushaharibu [emoji3]


Ndio maana wakimaliza wakichomoka ccp wanakuwa wamevurugwa morali kama zote usiombe ukutane na kisanga cha askari mpya huo utukutu wako utaisha
Jamaa kila siku jtatu hadi ijumaa ni master parade,wanakaguliwa usafi,uwe umenyosha na kung'arisha kiatu vizuri.
 
Mimi nawaambia ndugu zangu Mungu kafanya miujiza yake majina yametoka upo kote kote polisi na uhamiaji au fire na polisi [emoji3]. Halafu unasema unaenda ccp

Labda kwa mapenzi yako binafsi na mahaba yaliyo juu unapenda uende uko


Ila tukiongea ukweli nyie wenyewe mnajua nasema hivi humu ndani ikitokea imewakuta hivyo mmepata kote kote hakuna atakaye enda huko labda MrBanks [emoji3] kidogo inaonekana anakupenda

Ila xmonster anayependa mshahara wa haraka haraka utamkuta tayari kasharipoti boma
PT,UT,ZT ukipata kote nakushauri nenda PT.
 
Daah Mimi nakuogopa Sana kule

Ila mimi najiuliza mpka leo sipata jibu ina maana polisi miezi 9 hawa wengine 6

Kwa nini inakuwa hivyo

Na kwenye maslahi wakoje?

Maana wanasema wizara ya ndani mishahara inalingana
Polisi mafunzo unapewa ujuzi kabisa,wako na mambo mengi sana,kwata,darasani,silaha nk.
 
Kinachofanya polisi ichukue muda mrefu ni darasani sana. Masomo mengi afu porini pia wanakaa muda mrefu kuliko hata JW. Inshort dogo ananiambia porini polisi wako vizur sana na mifumo ya kimapigano. Kule ndio kazi ipo sana.
Polisi wana mapuuza tu ila mafunzo yao ni magumu sana na wako vizuri sana uwanja wa medani.
 
Mkiamka hiyo saa 6 mpaka mnarudi mabio saa 11 hiyo tayar na saa 12 unatakiwa uingie parade so kulala inakuw issue. Ahueni kidogo ilikuja baada ya kutoka poring alafu na course ya pccb ilikuw inaendeshwa hapo so mabio tulikuwa tunaanz sisi halafu tukishamaliza pccb ndio wanaenda.
Nawasikia kipindi cha kozi wakipita mitaa ya Moshi mjini usiku mnene wakiimba chenja dah utawaonea huruma,sijui kama wanalala kweli karibu mwaka mzima wa kozi yao.
 
Ndio maana nawaambia watakaoenda huko watabadili kabisa mentality waliyonayo kuhusu polisi...tena wakienda porini ndio kabisa mtaelewa kazi. Polisi sio lelemama kama mnavyoaminishwa huko kwingine.
Noted: polisi siyo lele mama nawakubali Sana Polisi
 
Back
Top Bottom