Nafasi za kazi Jeshi la Polisi Tanzania

Nafasi za kazi Jeshi la Polisi Tanzania

Ndio oljoro kozi imepoa ,, hivyo wakishua wengi wanapagombania.
Uzuri mboga saba na watoto midebwedo au watoto wa vigogo ni wachache jeshini, wazalendo halisi wapo vizuri , kwa hiyo haina shida.

Ila kuleta ubishoo jeshini hususa ni kwenye kozi za kuandaa askari na kupangia hawa kambi ile na wale kambi flani kwa sababu za hadhi ya wazazi wa watoto ni mapuuza sana na ni vizuri waache.

Maana vita ikitokea haijui cha midebwedo, watoto mboga saba au wana walio vizuri kijeshi, ni kazi kazi dadekkkk
 
Kama nawaona vile walishapiga zao six weeks za mkesha saa hizi wako pori

Hilo jina lisikutishe mkuu Kihangaiko ni jina la kijiji tu huko Bagamoyo hiyo kambi imechukua jina la hicho kijiji

Kuna sehemu pia inaitwa Kiharaka huko Bagamoyo so ni majina tu
Pori si mwishoni mwa kozi au?
 
Nasikia kihangaiko(msata) ni pagumu hamna mfano.

Oljoro watoto wa maofisa wengi hupelekwa kule kwahiyo scale kuna muda huwa inasinyaa baada ya kukakamaa sana.
Sema lile baridi la Arusha sio poa ukiwa six week mkesha utapigika sana.

Kwa upande wangu me bhana maeneo ya baridi alafu upige kozi naona kuvunjika njenje maana sometimes viungo vinakaza,Nakumbuka nilivyokuwa jkt Makuyuni maafande walitushauri tule sana karanga mbichi kulainisha joints
 
Shukrani mkuu hili jibu limenyooka

Haya mambo yanachanganya sana maana kuna wengine wanasema Msata parahisi kwa wenye connection mara wengine wanasema Oljoro ndio parahisi ndio maana nikaona nije kuuliza humu

Hapo kwa scale umemaanisha kwamba course ya Oljoro huwa imepoa kidogo kuliko ya Msata au
oljora inaweza kuwa rahis kwenda ila ngumu kutoboa usaili,
 
oljoro inakuwa na watu wengi sana na usahili unakua mgumu ila msata usahili unakuaga kawaida tuu
 
Sema lile baridi la Arusha sio poa ukiwa six week mkesha utapigika sana.

Kwa upande wangu me bhana maeneo ya baridi alafu upige kozi naona kuvunjika njenje maana sometimes viungo vinakaza,Nakumbuka nilivyokuwa jkt Makuyuni maafande walitushauri tule sana karanga mbichi kulainisha joints
Mkuu mbona hata Msata kuna baridi hasa usiku waulize waliopita wakuambie, navyofahamu hakuna kambi ya Jeshi ya mafunzo ambayo iko kwenye eneo lenye joto labda kambi za malezi au hizi zilizopo Dar, ni kwamba tu baridi linazidiana ila Msata nako kuna baridi kule
 
Yeah kote lipo baridi ila Oljoro linazidi kama ulivyosema
 
Kila mtu anatamani ajue watu wanaoitwa lini nahawajajua, ilakwenye upande wavitu gani vinatakiwa wanajua duh!
 
Back
Top Bottom