Nafikiri hivi ndivyo mambo yatakavyo kuwa kama ikitokea kwa asilimia kubwa ulimwengu ukawa chini ya influence ya Russia, China, Iran na marafiki zao

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
GEOGRAPHICALLY
North Korea atamvamia South Korea ili kutengeneza Korea ya Mamlaka yao

China itazichukua Taiwan na Hong Kong kwa asilimia 100.

Russia atamchukua Ukraine, Georgia na vinchi vidogo vidogo vya ulaya vile ambavyo vilikuwa chini ya USSR.

Iran atamtoa muisrael huku akitengeneza nchi ya uongo ya palestina angali yeye ndio atakuwa anapaongoza.

Iran atafadhiri vikundi vya militia katika nchi za Kiarabu zilizoachana na itikadi kali ( mfano UAE) ili vipambane kuondoa mamlaka za nchi hizo

Ongezeko kuu la wahamiaji kuingia europe kiholela ila kuinfluence na kuua ideology ya magharibi

POLITICALLY
Ongezeko la mapinduzi ya kijeshi katika nchi za kiafrika na kupatikana viongozi dikteta wataokuwa chini ya support ya China na Russia

NATO na G7 itakupungua nguvu huku nchi nyingine zikikimbia muungano huo kwa kuhofia kuwa attacked na Russia.

Nchi zilizokuwq vugu vugu katika mahusiano na itakadi zitahamia upande wa Urusi na China kwa maana chini ya Marekani walipata uhuru wa kuamua namna ya kua.

IDEOLOGICALLY
Nina uhakika asilimia 100 kutatokea holocaust nyingine kwa wayahudi.

Iran itapush nchi nyingi ziruhusu sharia laws

Russia na Iran itakikisha Itikadi na utamaduni wa west unafifia huku namna yao ya maisha ndio iwe promoted.

Wakristo watanyanyaswa sana katika nchi za Kiarabu ambazo zitakazo kuwa rafiki mkuu wa China na Iran.

ECONOMICALLY
Kwa maana soko litakuwa litakuwa chini ya influence ya China, itaifanya china kuimarika maradufu.

Russia atachukua nafasi ya USA kama muuza silaha mkuu maana nchi zilizofanya mapinduzi zitakuwa zina urafiki nae.

Ushikaji mkuu wa soko la mafuta utakuwa wa Iran.

Iran

Kwa maana miradi mingi itakuwa chini ya wachina, watu wengi watakuwa under paid and under appreciated

Sio vibaya ukaongozea nyama na wewe
 
Poleeee
 
Haya mbona hata wakati huu ambao China Russia na Iran hawapo huko juu ila ndio yanayo tokea duniani kote
 
umejitahidi kuchambua. ila Wanaoipinga Israeli hawawezi kufanikiwa. kamwe. MWANZO 12:1-3

JESUS is Lord
 
Kuna CHADEMA wengi sana wanamshangilia Putin!
 
Kabisa mkuu, dunia itakuwa sio mahali salama tena machafuko ya vita yataongezeka.
Ndio hata west hawako perfect

Ila angalau dunia iko stable kidogo chini yao

Ila hawa wakomonisti na itikadi ndio tutasoma namba
 
Yatatokea kwa ukubwa zaidi
Ukubwa ama udogo unaonaje au unaupimaje nilijua utasema kwamba wakati huu hakuna ama hayatakuepo kumbe hata wakati huu yapo basi kama ikitokea hao wakakaa juu acha nawao wafanye wanavyo penda
 
umejitahidi kuchambua. ila Wanaoipinga Israeli hawawezi kufanikiwa. kamwe. MWANZO 12:1-3

JESUS is Lord
Mwanzo 12 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;
² nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;
³ nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…