Tipstipstor
JF-Expert Member
- Nov 29, 2021
- 1,528
- 3,352
Mwanaume aliyekamilika hawezi kutoa siri ya aendako kabla hajafika...Believe me ,She will ruin all his plans.Ikishachukua maamuzi unatakiwa umshirikishe Mungu tu akuongoze huko uendako na YEYE ndie anaeijua nia na dhamira yako kuwa hujaitelekeza familia bali umeenda kutafuta maisha katika njia zake ili uje uitunze familia. Kumbuka mwanzo alishasema kuwa mwanamke hataki kumruhusu ahame sembuse amwambie anasepa kwenda kutafuta maisha?Pole mkuu...japo nauona utoto kwako...unajiita handsome..hata kama.
Ushauri wangu ni mdogo tu.
1. Lipa kodi ndipo uondoke, ukiwatoroka hutofanikiwa kamwe uendapo.
2. Usiondoke kwa kashfa na kejeli.
Mwite mkeo na mwanao na uwaambie;
-mke wangu ninakupenda sana sana japo
ninasikitika kuwa hali yangu ngumu imeondoa furaha yetu.
-kwa hali hii inanibidi nikajaribu maisha kwingine, naomba umlee mtoto kwa upendo wote, nikifanikiwa huko nitawakumbuka mke wangu.
Mkuu hata kama umekusudia kumwacha kwa siri lakini kwa maneno haya atakuwa anakutakia heri na ufanikiwe skijua ukifanikiwa amefanikiwa...usiondoke mke akilia hutofanikiwa uendako.
Usitumie maneno makali kwa mwanamke...bora unyamaze.
Hawa viumbe wakilia wananyonya baraka zetu