Nafikiria kumpiga chini huyu Mwanamke, hajui kuishi kwa bajeti

Kwa nini ununue kilo badala ya robo.
 
Nafikiri uenda ni mazoea tu alivyolelewa, nilikuwa na mahusiano na binti wa namna hiyo lakini baadae niligundua ametokea familia yenye uwezo sana nikakubaliana na hali, kuna watu wametokea familia za wali kidogo mboga saba sasa kama wewe umetokea familia ya mboga moja lazima mtakwazana tu.
 
Ndiyo nilikuwa hapo Kwa siku mbili kikazi,maswala ya chama Cha mapinduzi

Nililala Kuna lodge inaitwa Norries ndo nililala hapo,kwa sasa nipo safarini kwenda Bariadi napitia sehemu inaitwa Mwandoya
Ohoo kwetu hapo! Ila nna muda mrefu sijarudi huko. Safi sana
 
Kumbuka kuwa, kilo moja ya nyama mbichi ikipikwa inapunguwa robo kilo, ukitiwa na inayochapwa na mizani za wauza nyama, ukija kutowa na machalati, unabaki na nusu kilo tu ya nyama inayolika, tena hiyo sijahesabia mifupa.

Kula vizuri nyama kwa uchache ni robo kilo kwa mtu mzima mmoja kwa mlo mmoja.

Mkeo yupo vizuri hapo.
 
Kabla ya kuoa hakikisha unauwezo wakulisha watu wanne kwa kuanzia bila kulia lia, imagine mnapigizana kelele kisa kilo ya nyama.

Mwanamke kabla ya kuolewa hakikisha unaelewa dhana ya chakula mchanganyiko, sio lazima upike kilo nzima ya nyama, unaweza pika nusu, ukapika maharage robo, na mchicha wa buku, na ugali/wali/tambi. Watu wale wawe satisfied wanahisi wamekula vya maana kumbe πŸ€·πŸ»β€β™€οΈ

Mara moja moja ndio unawapikia kilo yote au kilo mbili kabisa wale hadi hamu ziishe.
 
Hiyo ni typical symptom ya broken heart,mtu keshavunjika moyo mara nyingi kiasi kwamba kuachana kwake ni jambo la kugusa tu. Mtu kama huyu ndio afunge "pingu za maisha" kweli?
Sio kweli…..
 
Kumbe ni demu nilijua ni mke
 
Mfundishe ili Apate kuelewa mara nyingi watu walikulia vijijini hawajui umuhimu wa badget katika Familia watu wawili Nyama kg 1 inabidi kutumiwa kwa siku mbili Ahsubui na jion so mfundishe mchele robo tatu unabidi kuuliwa Ahsubui na jion .

Usimfukuze mpe somo
 
Umenikumbusha miaka mingi Kijijini kwetu, kuna Mzee alikuwa siku ya Kupika Nyama anaenda mwenyewe jikoni kupika na kuhesabu Mafinyango.

Siku ya kupika Matembele anapika Mke wake πŸ™Œ

Ni vizuri kupanua wigo wa kutafuta pamoja na kuongeza Kipato
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…