Nafikiria kumpiga chini huyu Mwanamke, hajui kuishi kwa bajeti

Nafikiria kumpiga chini huyu Mwanamke, hajui kuishi kwa bajeti

Tupo town hapa lakini cha ajabu anaishi kama tupo Itilima, hajui kabisa kuishi kwa bajeti na wala haelekezeki.

Tupo wawili tu mimi na yeye lakini cha ajabu ile kilo ya nyama ya ng'ombe inaisha kwa kutwa moja!

Wakuu hii ni kawaida kweli? Tayari nimefikiria kuchukua maamuzi magumu

Ushauri wenu tafadhali.
Kwa nini ununue kilo badala ya robo.
 
Nafikiri uenda ni mazoea tu alivyolelewa, nilikuwa na mahusiano na binti wa namna hiyo lakini baadae niligundua ametokea familia yenye uwezo sana nikakubaliana na hali, kuna watu wametokea familia za wali kidogo mboga saba sasa kama wewe umetokea familia ya mboga moja lazima mtakwazana tu.
 
Ndiyo nilikuwa hapo Kwa siku mbili kikazi,maswala ya chama Cha mapinduzi

Nililala Kuna lodge inaitwa Norries ndo nililala hapo,kwa sasa nipo safarini kwenda Bariadi napitia sehemu inaitwa Mwandoya
Ohoo kwetu hapo! Ila nna muda mrefu sijarudi huko. Safi sana
 
Tupo town hapa lakini cha ajabu anaishi kama tupo Itilima, hajui kabisa kuishi kwa bajeti na wala haelekezeki.

Tupo wawili tu mimi na yeye lakini cha ajabu ile kilo ya nyama ya ng'ombe inaisha kwa kutwa moja!

Wakuu hii ni kawaida kweli? Tayari nimefikiria kuchukua maamuzi magumu

Ushauri wenu tafadhali.
Kumbuka kuwa, kilo moja ya nyama mbichi ikipikwa inapunguwa robo kilo, ukitiwa na inayochapwa na mizani za wauza nyama, ukija kutowa na machalati, unabaki na nusu kilo tu ya nyama inayolika, tena hiyo sijahesabia mifupa.

Kula vizuri nyama kwa uchache ni robo kilo kwa mtu mzima mmoja kwa mlo mmoja.

Mkeo yupo vizuri hapo.
 
Kabla ya kuoa hakikisha unauwezo wakulisha watu wanne kwa kuanzia bila kulia lia, imagine mnapigizana kelele kisa kilo ya nyama.

Mwanamke kabla ya kuolewa hakikisha unaelewa dhana ya chakula mchanganyiko, sio lazima upike kilo nzima ya nyama, unaweza pika nusu, ukapika maharage robo, na mchicha wa buku, na ugali/wali/tambi. Watu wale wawe satisfied wanahisi wamekula vya maana kumbe 🤷🏻‍♀️

Mara moja moja ndio unawapikia kilo yote au kilo mbili kabisa wale hadi hamu ziishe.
 
Tupo town hapa lakini cha ajabu anaishi kama tupo Itilima, hajui kabisa kuishi kwa bajeti na wala haelekezeki.

Tupo wawili tu mimi na yeye lakini cha ajabu ile kilo ya nyama ya ng'ombe inaisha kwa kutwa moja!

Wakuu hii ni kawaida kweli? Tayari nimefikiria kuchukua maamuzi magumu

Ushauri wenu tafadhali.
Kumbe ni demu nilijua ni mke
 
Mfundishe ili Apate kuelewa mara nyingi watu walikulia vijijini hawajui umuhimu wa badget katika Familia watu wawili Nyama kg 1 inabidi kutumiwa kwa siku mbili Ahsubui na jion so mfundishe mchele robo tatu unabidi kuuliwa Ahsubui na jion .

Usimfukuze mpe somo
 
Umenikumbusha miaka mingi Kijijini kwetu, kuna Mzee alikuwa siku ya Kupika Nyama anaenda mwenyewe jikoni kupika na kuhesabu Mafinyango.

Siku ya kupika Matembele anapika Mke wake 🙌

Ni vizuri kupanua wigo wa kutafuta pamoja na kuongeza Kipato
 
Back
Top Bottom