NAFUMUA MSHONO: Simu za iPhone ni mdebwedo, wanaozitumia ni watu wa kufuata mkumbo bila reasoning. Simu za Android ndio mpango mzima!

Vipi unazitumia? Narudia tena 0.0001% ndio wananunua simu ya thamani ya mls 3 kuweka emulator wacheze games otherwise consoles zipo kwa ajili hiyo

Downloads milioni 100.

Na most of time playstore wapenda emulators hawaitumii sababu inakuwa na version za zamani.

Hivyo mkuu milioni 100 atleast ni asilimia kadhaa ya watumiaji wa android.
 
Mkuu mimi kwakweli kupingana na wewe siwezi maana wewe ni kati ya malegendary wa jukwaa hili japo pia na wewe ni mnazi wa android, microsoft, nokia kama alivyo mkbh na Apple 😄😄
Sema you always make your points, na ninaheshimu sana hilo.
 
Nimetumia iPhone, nikateseka weeee na kauchumi kangu ka enzi za Magu, now nimerudi zangu android naona niko huru kabisaaa...

Anyway, kila mbuzi ale urefu wa kamba yake. Ukiweza iPhone, sawa ukienjoy android pia tu, tushauriane kwa upendo, ila tusipangiane maisha
 
Alafu cha ajabu ni kwamba huo Uhuru wa android ambao wengi wanauzungumzia ni wa mambo ya kitoto sanaa yaani... Mfano kudownload nyimbo, kubadili rangi ya screen nk🤣🤣🤣
 
Shida ipo kwenye Matumizi. Kaka wewe siyo mtu wa Costomization basi Iphone inakufaa lkn kama ni mtu wa customization nadhani android ni sahihi, ila hata hivyo wengi wananunua simu hawajui wafanyie nini na hizo simu zao, mwingine anaona ufahari tu kumiliki simu ya bei mbaya lkn hata kuscan document hawezi na hajui kama simu yake inaweza kufanya hivyo
 
Mkuu hiki unachokieleza hapa wengi hawakuelewi lkn ndio ukweli wenyewe. Mtu unaishi kwenye Rough Road unaemda kununua gari ya chini alafu unalalamika Gari uliyonunua haifai🤣🤣🤣
 
Maji
Maji ya Kilimanjaro mara nyingi utayakuta bungeni, mahotel makubwa na sehemu zingine za heshima. Maji ya uhai hata muuza ukwaju anayo anapotembeza ukwaju wake. Itoshe kusema Ni sawa uliyoyaongea na watu wanayafahamu ila ukiona kitu kinatumiwa na wachache jua Kuna Cha ziada. Huwezi kuwa Bora duniani Kama ujafanya kitu Cha ziada. Tununue tu simu zetu hizi hizi za Tecno.
 
Hichi ndicho nachozungumzia upo sahihi.
Mkuu hiki unachokieleza hapa wengi hawakuelewi lkn ndio ukweli wenyewe. Mtu unaishi kwenye Rough Road unaemda kununua gari ya chini alafu unalalamika Gari uliyonunua haifai🤣🤣🤣
 
Yes A15 bionic ni the most powerful prpcessor kwa simu as of now. Iko kwwnye iPhone na kama ulitumia iPhone 3gs, hebu jaribu sasa halafu urudi hapa useme kama iPhone sio pure multi tasking.

Hiyo A15 Bionic ya Apple kama haiwezi kuwasha mziki wa youtube wakati nasoma message za whatsapp then its worthless…
 
Hiyo A15 Bionic ya Apple kama haiwezi kuwasha mziki wa youtube wakati nasoma message za whatsapp then its worthless…
Hiyo ni feature tu ya app logic behind ni kwamba video unaitazama ukitoka kwenye app ya kutazama inajipause mpaka urudi.
 

Ukiwa na SD Card option huna ulazima wa kwenda Icloud kununua storage wala computer wala itunes wala app yeyote ile.

Kwa nini ulipie ku access data zako kwenye server Marekani wakati naweza kuwa na back up zangu hapa hapa Makete Stendi ???

Keep data local.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…