Nahisi kama napoteza mahusiano na mzazi

1. me
2. 19
3. mmoja
4. kifo
7. hapana
8. hapana
9. hapana,
 
Kwa mtu anaeishi kwao mara nyingi shida inakuaga ni mtoto.

Ile kujiona kakua, au kuona mzazi hafanyi fair.
 
1. Mheshimu mzazi lakini kamwe usiwe mtumwa wake. Mheshimu Kwa mazuri na Mema lakini Kwa mabaya mwambie yeye kuwa mzazi haimpi uhalali wa kukupandia juu Kwa vitu visivyoeleweka.

2. Endelea kutekeleza wajibu wako kama Mtoto. Msalimie lakini Isiwe kila Siku kama anakauli za kukera. Salimia wiki Kwa wiki. Kama hamna bond.

3. Mwambie yeye ndio anakujua vizuri. Aliposema yeye ni mama yako ulimsikiliza na kumheshimu. Halikadhalika akisema yeye sio Mama yako pia utamsikiliza na kumheshimu. Mwambie hujawahi kulazimisha kuwa yeye ni mzazi wako. Ila unasikia na kuambiwa.

4. Ukiongea naye akujue wewe ni MTU wa Haki. Utamjibu na kumtendea Kwa haki. Na sio upendeleo.
 
Mzazi ukiwa mpole na mtu wa kujishusha mnapatana sana sana.

Inaumiza sana kujibishana na mzazi, mdogo wako tu akikujibu fyatu unamlapua. Sasa mama kukupiga hawezi ushakua kijeba anaishia kuishi kwa makasiriko tu.

Ujana wa kutorudi home tushaupitia ila waambie ukweli ni kipi kinakuweka huko.
 
Huu ushauri wako unampotosha bwana mdogo.
Kwanza kabla ya hayo yote inabidi amjue mzazi wake ni mtu wa namna gani, ana elimu gani ukimwambia hayo mambo ya haki na upendeleo atakuelewa??

Wazazi wetu wengi hawakwenda shule, wanaishi kimila zaidi eti usimsalimie aloo unajitaftia majanga tu na kuongeza makwazo.

Kijana kama ni msomi atumie emotional intelligence kumaliza tatizo. Haihitaji mambo ya haki na upendeleo. Kinachofanya tatizo liwe kubwa ni hisia.

Mama anahisi hivi, mtoto anahisi vile. Sasa mtoto ajue hisia za mama yake na acheze nazo, simple kabisa.
 
hata mimi nimeona hii ndo nzuri mkuu
Kama huwa humpigii sim basi jaribu kua unampigia hata mara 3 kwa wiki.

Mpigie jumapili mwambie umeenda kanisani kama ndo kitu hupenda kusikia. Kama anahisi unakula bata mueleze magumu unayopitia huko. Mwambie umemmisi muahidi siku utakayoenda nk.

Kama mnakwazana mara kwa mara nenda ukae siku 2 au 3 za furaha then geuka zako chuo.

Ni mama yako na ni mwanamke pia, wanatumia sana hisia kwenye maamuzi yao, inabidi ufanye akuamini wewe zaidi ya mtu mwingine anaetoa taarifa kuhusu wewe. Yeye huko anaskia wanachuo mnaolewa na mishangazi, anaskia mnakula bata, anaskia muda mwingi hamuendi chuo, mnapewa hela nyingi na serikali nk ila wewe humwambii kitu so anapigia mstari anayoambiwa na hivyo hizo tabia zako ndo kabisaaa anasema huyu kapata pesa kawa jeuri kumbe sivyo, hisia tu.
 

Haki ya mzazi aliyesoma na asiyesoma hazifanani.
Atende Haki.
 
Huyu mwamba amebonga ukweli mtupu
 
Mtoa mada kina mengi umetuficha Kati yako na mzazi wako,sidhani Kama mzazi anaweza kumchukia mwanaye bila sababu ya kueleweka.

Kama kweli ulimkosea mzazi wako nakuomba uurudishe moyo wako nyuma,jishushe Kisha nenda umuombe msamaha kea upole Sana.Ukishafanya hivyo bila Shaka mzazi wako atarudisha imani Yake kwako.

Mzazi Ni Mungu wako wa pili baada ya Mungu mwenyezi.
 
Kama ni wakiume Acha kiburi alafu angalia na marafiki wa kike ulionao kama unagombana na bi mkubwa,..

Kama ni wakike hiyo ni kawaida ila ukimaliza jitahidi uolewe na mwanaume anaye eleweka hapo mama anapoa..



Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Tunagombana sana[emoji848] aisee hii hajakaa sawa hata kidogo.

Acha kabisa tabia ya kugombana na mama wewe ni mtoto hata kama unaona kuna sababu ya kukukera.
Moyo wa mzazi unaumia na kusononeka ndani kwa ndani unapokosa kumheshimu.
Kuna maneno ya uchungu ambayo mzazi huyatamka wazi wazi au kwa siri ambayo matokeo yake utayaone baada ya kuchelewa

Zuia kinywa chako.

MTOTO KWA MAMA HAKUI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…