Nahisi kama napoteza mahusiano na mzazi

Watu wamecoment upande mmoja wa lawama kwa kijana pekee, lakini wamesahau pia sisi wazazi tuna shida. Kuna mzazi amchukia mwanae mpaka dunia inashangaa...mwingine anaomba hela kila siku na mtoto asipompa ni maneno mazito yatamtoka mzazi mpaka mnajiuliza ni mzazi wake kweli?!

Kama ni shida basi ziangaliwe pande zote. Ila kwa maelezo yake between the lines huyu dogo ana mzazi toxic...(probably mama yake ni mchaga, sorry to say this)
 
kijana acha utukutu...

Kwa mzazi yakupasa kujinyenyekeza hata kama hakupendi au anakuona chizi maarifa.. peleka na vizawadi mpe komaaa hadi atafungua moyo.. peleka zawadi nzuri apendayi
 
Una tatizo linataka kufanana na mimi.

Nikiwa mbali tunakuwa na uhusiano mzuri na mama ila nikiwa home duu tunagombana sana bila sababu za msingi.Kwasasa nilishafanya maamuzi nitakaaa huku niliko ili tuendelee kuwa na uhusiano mzuri.
tafta suluhisho mzee, generally ni vibaya
 
Siku ukimpoteza huyo mzazi wako ndio utaijua thamani yake,but itakua too late,

Tatizo lako unataka kushindana na mzazi wako,

Kuzozana nae ina maana kila mmoja kati yenu anajiona yupo right ila wewe ndio ulitakiwa umsikilize mzazi wako,wala usijifanye mjuaji mbele yake,

Hata kama atakwambia "Tembo anaweza kuruka angani" wewe mkubalie tu kua yupo sahihi,hutogombana nae tena na huo ndio utakua mwisho.
 
Sema ukweli, wakubwa wakusaidie😂😂
 
Acha kujidanganya chaliangu jishushe tulizana ishi vizuri na mama, Kuna mda wamama hua wanazingua lkn kuna namna ya kistaarabu unaweza ukaepuka mzozano na yy!

Kwa saiv unaweza kua unamtunishia misuli lkn ipo siku utajuta utatamani hata usikie sauti yake bila kujali hyo sauti inasema nn! Epuka ligi na mzazi ishi vzr na mzazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…