mimimchaga
New Member
- Feb 24, 2025
- 2
- 33
Si tunatafuta mume na wewe unaacha mkeNina miaka 38...Niko single(nimeachana na mke wangu)....sivuti sigara na wala sinywi pombe...sijaajiliwa nimejiajili kwhy hela ya kula vizuri na matumizi madogo mdogo hainipigi chenga kwa kifupi sina njaa...uhakika wa mbunye upo yani simu moja tu naletewa mbunye mpka mlangoni kwa kifupi japo niko single ila uhakika wa mbunye si haba nnao mda wowote nikiwa na upwiru
Ila shida yangu kubwa pamoja na mahitaji yote ya muhimu ambao naweza kuyapata lakini najiona kabisa mda mwingi sina furaha.kama siku sina kazi ya kufanya basi nisipokaa kwenye tv au nisiposhika simu yangu hiyo siku itakua ya huzuni sana kwangu
Kwa siku naweza kutumia zaidi ya 10,000 peke yake kwa ajili ya bundle tu ili nijaribu kuitafuta furaha mtandaoni ila bundle likikata narudi kwenye huzuni...nimekua addicted na simu pamoja naTV yangu kwasababu ya kukosa furaha mpka nafikia hatua usiku nalala sa8 mapak sa10 na nnachokifanya cha maana sikioni...inafikia hatua asubuhi naweza kupanga nitatoka sa1 ila nikishika tu simu najikuta imefika sa4 bado sijatoka
Kuna mda niliamini labda furaha ya kweli pekee ipo ndani ya yesu kristu kwhy niliamua mda mwigi niutumie kumtafuta mungu kwhy nilifuta kila kitu kwny simu yangu kuanzia insta.x.tiktok na social media zote mpka jamiiiforums niliifuta lakini changamoto ikaja hata kusoma mistari miwili tu ya biblia kichwa kilikua hakitaki ni huzuni tu
Kwani watanzania wenzangu mnafanyaje kupata furaha kwenye haya maisha mbona mm mda wote nakua na huzuni au mm nina tatizo la afya ya akili au nimelogwa au mtu akiwa single kwa mda mrefu ndo anakua na hali hii ili kama ndo sababu niende kumpgia goti mke wangu arudi... naomba wataalumu wa afya ya akili mnisaidie ili niweze kuondokana na hii hali najiona naelekea kudata