Prince Mhando una psychosis..
una mental I'll iliyokomaa hasa tabgu nikufaham.
Ugumu wa maisha utakupoteza kabisa.
Kwa kazi zote ulizofanya hujapata ya kukomaa nayo na kumbkumb zangu zinanambia upo unalinda shamba kisarawe la The bump. Je tatizo nn hasa?
Kama uliwahi kufikiria kujiua maana yake unatembea na wazo Hilo.. unahitaji haloperidol amitriptyline na folic acid. Pia therapy mana kwa hali hiyo utaanza kupata maruwe ruwe yani kuongea peke yako tena hivyo na kuokota karatas.
Nina ndugu yangu ana experience kama yako, unahitaji therapy na matibabbya mda mrefu sana kurudi kuwa kawaida. Umeshaianza kupoteza memory na huwezi kuconceteate? Duh
Tujifunze kuongea Maneno Mazuri kwa Watu wenye matatizo kama haya hasa Depression iliyosababisha na stress au na mental Probl..
Kuna baadhi ya maneno tunaweza kuyasema yakachochea tatizo na likawa baya kuliko hata mwanzoni lilivyokuwa....
"KAULI INAO UWEZO WA KUUA au KUBORESHA"
Mimi sio msimuliaji mzuri ila nitajaribu kutoa kisa kimoja kilichowahi kunitokea kwa uzembe wa Daktari mwenye kauli mbovu..
"
Ntatoa kisa kimoja"
Miaka saba au nane nyuma Nikiwa Nyumbani alinipigia Simu Rafiki yangu mmoja mhandisi, Tumeshibana sana (
Marafiki Tangu tukiwa wadogo na tulibahatika pia kuwa marafiki wa Ukubwani na kukaa Mkoa na Wilaya moja)
akaniambia Baba yake yuko Nyumbani kazidiwa sana na hawezi hata Kuongea na ana siku ya Tatu hajala wala kunywa chochote na hali yake imezoroteka sana (Kwa kuwa Baba yake ni mtu ambaye nilikuwa nataniana naye sana na nilizoeana naye kwakuwa Kwanza alikuwa Yanga "Mimi ni Simba" pili alikuwa kabila Hasimu "Watani" na kabila langu)
Hiyo ilijenga Imani kwake hata kwa baadhi ya mambo ya ndani ya kimatibabu yeye kuniambia mimi na nilkuwa namshauri vizuri tu..
Sasa tuendelee
Sasa nikashtuka na kumlaumu sana Rafiki yangu inawezekanaje baba anaumwa na hawezi kula siku ya Tatu na hakuweza kuniambia?
Akanijibu yeye mwenyewe hakuwepo amerudi leo kutoka safari amekuta Mdogo wake akamwambia hivyo na kutwa alikuwa akitaja Mimi niende kumuona au Nimshauri kuhusu ugonjwa wake kabla hajafa..
Kupunguza Story isiwe ndefu sana
Ni kwamba Baba wa rafiki yangu aliugua Ghafla akalalamika tumbo na akaondoka nyumbani akiwa mzima tu ila alitaka kwenda kufanya check up ya Tumbo ili kujua Nini kinamsumbua mbona tumbo linamuuma halafu muda mwingine linaacha..
Kufika hospitali kafanya Vipimo vyote ikiwemo Ultrasound..
Kitu kilichokuwa sumu kwake ni ile kauli ya Daktari Kwenye Kumpa majibu ntanukuu alivyomwambia..
" Mzee vipimo vyako ni Vibaya sana, Ini lako Limeoza kabisa na hata tumboni sio kuzuri kabisa, Inaonekana Una cancer kabisa, Pole sana Mzee na hata ninashangaa umewezaje kufika hapa maana Huko tumboni hakufai kabisa mzee wangu, Nitakuandikia Dawa lakini kwa maradhi yako ni vigumu sana kupona"
haya maneno Bado huwa nayakumbuka Kwenye Kichwa Changu yule mzee ananiambia kwa akiyarudia rudia..
Kabla ya kujibu chochote nikaomba majibu vipimo ya yule mzee pamoja alivyoandikiwa halafu nikaomba na namba ya Yule daktari..
Majibu ni kwamba Mzee alikuwa na Hepatitis, Ilikuwa kwenye Very Early stages..Kulikuwa na Njia nyingi za kumwambia na Akaishi kwa muda mrefu huku akitumia ART
Kiukweli kazi aliyofanya Yule daktari kwa Dakika chache Ilituchukua Wiki nzima kuirekebisha huku Tukitoa ushauri mkubwa sana Japo mzee Alifafiki Baada ya wiki mbili..
Naamini kabisa Kama mzee angepewa maneno mazuri Yasiyo na unyama wa namna ile huenda angechukua Mwaka au hata miezi sita kufariki..
Mzee alikuwa akisema " Nakula nini sasa kama tumboni nimeshaoza" "mimi siponi ntakufa sasa kuna haja gani ya kula"...
Madaktari Na washauri Kauli zenu zinaweza kuua..
Tuzingatie tunapotoa HUDUMA ya USHAURI KWA serious Situation kama Hizi...