Nahisi siku zangu za kuishi Dunia zinakaribia kuisha, sielewi!

Nahisi siku zangu za kuishi Dunia zinakaribia kuisha, sielewi!

Una depression!
That is part of life
Jiambie tu kuwa na hii itapita
Ukisikia mapito ya wengine utajiona una afadhali,
Mshukuru Mungu hata kwa afya ya hao watoto na mkeo na jiambie as long as bado wote mko hai kuna sehemu mtafika na mtasahau mapito yote!
Songa mbele maisha ndivyo yalivyo kuna wakati wa vita lakini na wakati wa amani upo!
 
Mkuu; wewe unapenda muziki? Yan unasikiliza muziki wa aina gani au kutumia vyombo vya muziki au kuimba ww mwenyewe? Naomba unijibu halafu nitaendelea baada ya jibu lako.
mimi mziki napenda ila kwaya... japo mimi ni muislam... kuna muda haswa kipindi hiki nyimbo nikisikiliza nahisi kama zinanipigia kelele...!

hivyo sio mpenzi san wa kelele...!
napenda kusikiliza motivation speaking haswa mahubiri... Mara kadhaa nilishawahi kufungulia radio zenye mahubiri hata ya mwamposa na mwakasege... nikisikilizaga mahubiri kidogo napata kaunafuu...!

japo kuna muda hata hayo mahubiri huwa siyaelewi...!​
 
nawaza kupauza... mkuu na Tangazo nilishaweka humu humu...kuna member wamenipigia baadhi wameenda kukiona walau naweza kupata ahueni kama wakifika bei... niende kijijini huko nikaanze maisha upya au nijenge nje ya mji huko...!

ila kwasasa hali yangu ni mbaya... kuna mambo siwezi kuyaandika jamii itanicheka😭😭😭​
Kwa nn kule Dubai usingeenda na wewe?

Pale ni kukomaa ukajenge, mana hata iweje mjini mjini tu. Wengi Wana nyumba mjini n wamerudi bush. Siku ukiuza mazao unakuja kuzuga hata wiki tatu town na familia yako! Kwako
 
Una depression!
That is part of life
Jiambie tu kuwa na hii itapita
Ukisikia mapito ya wengine utajiona una afadhali,
Mshukuru Mungu hata kwa afya ya hao watoto na mkeo na jiambie as long as bado wote mko hai kuna sehemu mtafika na mtasahau mapito yote!
Songa mbele maisha ndivyo yalivyo kuna wakati wa vita lakini na wakati wa amani upo!
nashukuru SANA 🙏 nitajitahidi
 
Kwa nn kule Dubai usingeenda na wewe?

Pale ni kukomaa ukajenge, mana hata iweje mjini mjini tu. Wengi Wana nyumba mjini n wamerudi bush. Siku ukiuza mazao unakuja kuzuga hata wiki tatu town na familia yako! Kwako
nafasi zilikuwa chache... harafu pia sikuwa nimejiandaa... ili hitajika fedha ya haraka haraka kama 700k kufanikisha huo mchakato...!

process ya kwenda nje inahitaji gharama hivi umekosa unatakiwa uwe hata na 1000k mkononi...!​
 
Wakuu huyu ni WA dozi tu haya ya mungu na upako yake kunisaidia dawa ifanye kazi vizuri. Psychiatrist yoyote ukimuambia kuwa uliwahi kufanya jaribio la kujiua ikashindikana uñaanza dawa hapo hapo mbele yake akuone
 
lakini kipindi hicho nilikuwa mdogo sana... miaka 9 mkuu
 
nafasi zilikuwa chache... harafu pia sikuwa nimejiandaa... ili hitajika fedha ya haraka haraka kama 700k kufanikisha huo mchakato...!

process ya kwenda nje inahitaji gharama hivi umekosa unatakiwa uwe hata na 1000k mkononi...!​
1 M. The bump ilikuaje kwani mbona ulionesha nia ya kumbeba jamaa?. Kaka Dan Zwangendaba sema neno hapa kijana Hana pa kushika huyu
 
Yan mkuu acha tu .. sisemi sana! Ila hali si shwari kila Kona ila muda wa kusononeka ndo haupatkan. Prince Mhando kaza makalio hayo .. vijana hatuna pa kushika! Bora wewe uchumi wako unalisha familia ya watu wanne Milo mitatu .. Kuna watu humu tuna hali mbaya.. ila tunaamin katika kila hatua tuliyopo na tunajifunza namna ya kusonga mbele na kuyabeba maumiv yake
Sijui kama anaelewa
 
kiuchumi siwezi kusema nina tatizo kihivyo kwani nina jishughulisha... japo sina kipato kikubwa cha kumsaidia mwingine ila nina uwezo wa kula milo mitatu...!

kwakweli sielewi kwanini nimewaza hivyo...!​

Ukiweza pata muda nenda Ocean Road hospital salimia wale wagonjwa.

Pia pita Muhimbili ona watu wanaopambania uhai, wanavyotamani wawe na afya Bora tu bila kujali wanamiliki kitu Gani.

Mawazo au Hali unayojiweka inamchangi Mkubwa sana kwenye matokeo ya kesho Yako, usikate tamaa kamwe.

Ukianza kuwazawaza kufa, ni kama una amrisha mwili wako na viungo vyote kuanza kuitikia hiyo sauti.
 
inabidi tutengeneze majukwaa ya vijana kushauriana ana kwa ana kwakweli hali mtaani ni mbaya mno.

watu jamii yangu wapo wengi na awana pa kusemea... wakuu ukiona mtu kajinyonga usimcheke😭😭😭

kuna mambo hayaelezeki​
Eeeh hapo kwenye jukwaa hapo,hayo ndio mambo ya kuongea sio kuongea mambo ya kufariki Ili iweje?Ngoja nikuchek PM tuanzishe jukwaa
 
Ukiweza pata muda nenda Ocean Road hospital salimia wale wagonjwa.

Pia pita Muhimbili ona watu wanaopambania uhai, wanavyotamani wawe na afya Bora tu bila kujali wanamiliki kitu Gani.

Mawazo au Hali unayojiweka inamchangi Mkubwa sana kwenye matokeo ya kesho Yako, usikate tamaa kamwe.

Ukianza kuwazawaza kufa, ni kama una amrisha mwili wako na viungo vyote kuanza kuitikia hiyo sauti.
nashukuru SANA 🙏... muda mwingine nawaza na sipati majibu ya ninacho waza...!

ila kupia andiko hili wachangiaji wengi wamenisaidia kwakweli nime pata unafuu kabisa... kuna mzigo ulikuwa una nielemea kidogo nimeutua...!​
 
Wakuu huyu ni WA dozi tu haya ya mungu na upako yake kunisaidia dawa ifanye kazi vizuri. Psychiatrist yoyote ukimuambia kuwa uliwahi kufanya jaribio la kujiua ikashindikana uñaanza dawa hapo hapo mbele yake akuone
na hizo dozi... si zinapatikana kwenye maduka yetu haya...? ya mtaani..? pharmacy
 
Prince Mhando una psychosis.. una mental I'll iliyokomaa hasa tabgu nikufaham.

Ugumu wa maisha utakupoteza kabisa. Kwa kazi zote ulizofanya hujapata ya kukomaa nayo na kumbkumb zangu zinanambia upo unalinda shamba kisarawe la The bump. Je tatizo nn hasa?

Kama uliwahi kufikiria kujiua maana yake unatembea na wazo Hilo.. unahitaji haloperidol amitriptyline na folic acid. Pia therapy mana kwa hali hiyo utaanza kupata maruwe ruwe yani kuongea peke yako tena hivyo na kuokota karatas.

Nina ndugu yangu ana experience kama yako, unahitaji therapy na matibabbya mda mrefu sana kurudi kuwa kawaida. Umeshaianza kupoteza memory na huwezi kuconceteate? Duh
Tujifunze kuongea Maneno Mazuri kwa Watu wenye matatizo kama haya hasa Depression iliyosababisha na stress au na mental Probl..

Kuna baadhi ya maneno tunaweza kuyasema yakachochea tatizo na likawa baya kuliko hata mwanzoni lilivyokuwa....

"KAULI INAO UWEZO WA KUUA au KUBORESHA"

Mimi sio msimuliaji mzuri ila nitajaribu kutoa kisa kimoja kilichowahi kunitokea kwa uzembe wa Daktari mwenye kauli mbovu..

"Ntatoa kisa kimoja"

Miaka saba au nane nyuma Nikiwa Nyumbani alinipigia Simu Rafiki yangu mmoja mhandisi, Tumeshibana sana (Marafiki Tangu tukiwa wadogo na tulibahatika pia kuwa marafiki wa Ukubwani na kukaa Mkoa na Wilaya moja)

akaniambia Baba yake yuko Nyumbani kazidiwa sana na hawezi hata Kuongea na ana siku ya Tatu hajala wala kunywa chochote na hali yake imezoroteka sana (Kwa kuwa Baba yake ni mtu ambaye nilikuwa nataniana naye sana na nilizoeana naye kwakuwa Kwanza alikuwa Yanga "Mimi ni Simba" pili alikuwa kabila Hasimu "Watani" na kabila langu)

Hiyo ilijenga Imani kwake hata kwa baadhi ya mambo ya ndani ya kimatibabu yeye kuniambia mimi na nilkuwa namshauri vizuri tu..

Sasa tuendelee
Sasa nikashtuka na kumlaumu sana Rafiki yangu inawezekanaje baba anaumwa na hawezi kula siku ya Tatu na hakuweza kuniambia?

Akanijibu yeye mwenyewe hakuwepo amerudi leo kutoka safari amekuta Mdogo wake akamwambia hivyo na kutwa alikuwa akitaja Mimi niende kumuona au Nimshauri kuhusu ugonjwa wake kabla hajafa..

Kupunguza Story isiwe ndefu sana

Ni kwamba Baba wa rafiki yangu aliugua Ghafla akalalamika tumbo na akaondoka nyumbani akiwa mzima tu ila alitaka kwenda kufanya check up ya Tumbo ili kujua Nini kinamsumbua mbona tumbo linamuuma halafu muda mwingine linaacha..

Kufika hospitali kafanya Vipimo vyote ikiwemo Ultrasound..

Kitu kilichokuwa sumu kwake ni ile kauli ya Daktari Kwenye Kumpa majibu ntanukuu alivyomwambia..

" Mzee vipimo vyako ni Vibaya sana, Ini lako Limeoza kabisa na hata tumboni sio kuzuri kabisa, Inaonekana Una cancer kabisa, Pole sana Mzee na hata ninashangaa umewezaje kufika hapa maana Huko tumboni hakufai kabisa mzee wangu, Nitakuandikia Dawa lakini kwa maradhi yako ni vigumu sana kupona"

haya maneno Bado huwa nayakumbuka Kwenye Kichwa Changu yule mzee ananiambia kwa akiyarudia rudia..

Kabla ya kujibu chochote nikaomba majibu vipimo ya yule mzee pamoja alivyoandikiwa halafu nikaomba na namba ya Yule daktari..

Majibu ni kwamba Mzee alikuwa na Hepatitis, Ilikuwa kwenye Very Early stages..Kulikuwa na Njia nyingi za kumwambia na Akaishi kwa muda mrefu huku akitumia ART

Kiukweli kazi aliyofanya Yule daktari kwa Dakika chache Ilituchukua Wiki nzima kuirekebisha huku Tukitoa ushauri mkubwa sana Japo mzee Alifafiki Baada ya wiki mbili..

Naamini kabisa Kama mzee angepewa maneno mazuri Yasiyo na unyama wa namna ile huenda angechukua Mwaka au hata miezi sita kufariki..

Mzee alikuwa akisema " Nakula nini sasa kama tumboni nimeshaoza" "mimi siponi ntakufa sasa kuna haja gani ya kula"...

Madaktari Na washauri Kauli zenu zinaweza kuua..

Tuzingatie tunapotoa HUDUMA ya USHAURI KWA serious Situation kama Hizi...
 
Mimi ni kijana ambae nina mshukuru sana Mungu tokea nimezaliwa hadi hapa nilipofikia, watu wamenisaidia na bado wana nisaidia.

Kuna Muda huwa nina kufuru au kukana kutkukubaliana na uwepo wa Mungu😭 hii ni kutokana na asilimia kubwa ya matarajio yangu tokea nikiwa mdogo hayakuwahi kutimia.

Maisha yangu yamekuwa ya mitihani sana, kila nilichojaribu kuanzisha hakikuwahi kufika mwisho 😭😭😭 kwakweli nimeishi nikiwa na huzuni na furaha chache, mpaka hapa nilipofikia nina watoto wa 3 ambao ninawapenda mno.

Vipo vitu vichache ambavyo vinanitokea hivi sasa vinapelekea mimi kuhisi pengine siku zangu hapa Duniani zina karibia kuisha.

Hivi karibuni kichwa changu kimekuwa kizito mno kutoa maamuzi na ni kama kichwa kinanielemea, kimekuwa na maumivu fulani mithili ya kichwa kilicho toka kuuma!

Kwa taaluma mimi ni Mwandishi wa Habari ambaye napenda sana kusoma vitabu na asilimia kubwa ya vitu vingi nimejifunza kutokana na kusoma vitabu, lakini hivi karibuni nimepatwa na hali ya kutokuelewa kila ninacho kisoma.

Vitabu vyote ambavyo nilikuwa navipenda nikivisoma nahisi vinanichanganya, hata baadhi ya mada nilizokuwa nazipenda hapa JAMIIFORUMS nazo pia nimekuwa sizielewi.🥲

Nimepatwa na hofu hata nikikaa karibu na watu ninaowapenda sifurahii uwepo wao, nahisi kujitenga tu nikae peke yangu tu muda wote.

miaka ya nyuma nilikuwa na ndoto pengine za kuwa fulani nikawa naziishi ndoto hizo kwa kuzipambania kwa vitendo lakini siku bahatika kuishi maisha ya ndoto zangu.

siku hizi ni kama siioni future yangu kabisa... muda mwingine mpaka najiona kabisa kama napoteza tuu muda 😭😭😭😭

kama ninge kuwa simu hope ingekuwa kwenye flight mode ✈️🤣🤣🤣

Ikitokea hamjaniona hewani mwezi mzima mfululizo mjue siku zangu niliziona kabisa zinahesabika hivyo malaika mtoa roho atakuwa amesha fanya yake.

Sifikirii kabisa kujiua kwa aina yoyote ile japo kwenye maisha yangu udogoni mwanangu nilishawahi mara 2 kujaribu kujiua. 😭

Mara ya kwanza nilijaribu kunywa sumu haikuniua, hapo nilikuwa na miaka 9 au 10, mwaka mmoja baadae nilijaribu kujinyonga bahati mbaya kile kitanzi pia hakikuondoka na maisha yangu.

Hivyo nichukue fursa hii kuwaaga ndugu zangu wana JAMIIFORUMS ambao tumeishi wote humu ndani kama familia. Kuna member humu nimesaidiana nao bila hata kufahamiana nao big up sana.

Kuna wengine tumekuwa ndugu na hata nje ya JAMIIFORUMS tumekuwa tukionana kwakweli sina cha kuwalipa.​
Nitajie mtu mmoja unayemfahamu siku zake za kuishi duniani hazikaribi kuisha. Nitajie mmoja tu.
 
Mkuu kumbuka mama yako anakutegemea hata kama unafanya kazi ya bolt
 
NJOO TUKUVUTISHE BANGI NA POMBE KALI ILI UWE NA ROHO MBAYA YA KUJUA WEWE DUNIANI UTAKIWI KUWA MZEMBE .PAMBANA HAKUNA KUCHOKA.
UKIANZA KUJIKATIA TAMAA NA MWENYE CHAMA CHA CHAUMA ASEMEJE
 
Yan mkuu acha tu .. sisemi sana! Ila hali si shwari kila Kona ila muda wa kusononeka ndo haupatkan. Prince Mhando kaza makalio hayo .. vijana hatuna pa kushika! Bora wewe uchumi wako unalisha familia ya watu wanne Milo mitatu .. Kuna watu humu tuna hali mbaya.. ila tunaamin katika kila hatua tuliyopo na tunajifunza namna ya kusonga mbele na kuyabeba maumiv yake
Na Dunia ya Sasa inataka watu wa namna hii,yaani ni ubishi na kukaza mpaka kieleweke, yaani ni ubishi kama Muha,plan A ikifeli unahami plan B
 
Back
Top Bottom