Nahitaji kujua kazi maalumu za askari wa kila cheo(JWTZ)

Nahitaji kujua kazi maalumu za askari wa kila cheo(JWTZ)

[emoji92]
Screenshot_20210110-213934.jpg
 
Ninahitaji kujua mambo kadhaa yanayohusiana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na askari wa vyeo tofauti tofauti vya kijeshi.Kuanzia cheo cha chini kabisa mpaka cha mwisho.Namaanisha majukumu ya kila siku.Mfano ukipita lugalo unaweza kuwakuta kuruta wanafyeka nyasi sijui kazi zao ndio za aina hiyo hizo kila siku?

Na katika medani za kivita ni askari wa vyeo gani huwa wanaingia kwenye uwanja wa vita kwa maana ya kushiriki vita na sio wale wapanga mikakati.Nimekuwa nikisikia askari wa kuanzia nyota moja wanakuwa wanaamrisha kikosi cha watu kadhaa.Askari wa nyota mbili nae ana watu kadhaa zaidi ya wa nyota moja.
kuruta ni askari alyoko mafunzoni(recrut) wale unawaona pale Lugalo wakiwa hawana cheo wanaitwa Private kule polisi wanaitwa constable kule Magereza wanaitwa Wader . Cheo cha kwanza baada ya mafunzo ya ukurufa kuisha kinaitwa private.Hawa ndiyo askari wapiganaji na watapangiwa kazi katika section kulingana na taaluma zao kijeshi. Nikisema section ni kikudi cha askari tisa anayeongoza anakuwa na v mbili anaitwa coploo na yule mwenye v moja anaitwa less coploo akakuwa mwisho kabisa mwa kikundi na anakuwa msaidizi wa coploo ukitaka kujua zaidi nenda depo au mgambo utajifunza.
 
Hapo ana uzoefu wa kufa mtu.. ukimpa kikosu uchwara anakitoa mavi
Hao jamaa utamu wao wapewe mission zinazofanana na za kigaidi gaidi , yaani wanakuwa kama wanaibukia ibukia

Kama adui wamejikusanya sehemu fulani hao jamaa wapelekwe wakiwa wamejichanganya na raia hiyo kazi baada ya hapo maadui wataelewa mbona
 
Sio kweli .
Kwani nchi zenye Vita wanajeshi wao HAWALINDI?.
amani ya nchi inaanza na wewe SIO JESHI
Hapa Baba umepuyanga kweli, Jamaa kamjibu vizuri tu, jukumu la msingi Kuilinda Mipaka ya Nchi huko kufye, ni usafi wa kawaida tu, akatolea mfano, kama yeye anavyofua box yake.

Unadhani jukumu la msingi la jeshi, haliwezi kufanana jukumu la jeshi lingine.

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
nakushauri nenda makao makuu ya jeshi utajibiwa maswali yako yote haya kwa ufasaha zaidi, humu hutapata majibu mazuri sana. ama nenda wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa.

ila watahitaji kujua hasa nia na mazumuni yako ni yapi ukiwajibu na wakalizika watakupa ushirikiano mzuri na vichura viwili vitatu ili ubaki na kumbukumbu nzuri kwa watakayokuelezea.
Hahaha
 
Ninahitaji kujua mambo kadhaa yanayohusiana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na askari wa vyeo tofauti tofauti vya kijeshi.Kuanzia cheo cha chini kabisa mpaka cha mwisho.Namaanisha majukumu ya kila siku.Mfano ukipita lugalo unaweza kuwakuta kuruta wanafyeka nyasi sijui kazi zao ndio za aina hiyo hizo kila siku?

Na katika medani za kivita ni askari wa vyeo gani huwa wanaingia kwenye uwanja wa vita kwa maana ya kushiriki vita na sio wale wapanga mikakati.Nimekuwa nikisikia askari wa kuanzia nyota moja wanakuwa wanaamrisha kikosi cha watu kadhaa.Askari wa nyota mbili nae ana watu kadhaa zaidi ya wa nyota moja.
Mleta maada ukitaka kujua kazi ya wajeda jarb kutembelea eneo lao, utaoneshwa vzr kazi zao.

Umenikumbusha siku moja tukiwa wadogo tulikuwa tunacheza maeneo fulani, tukanaibi kujimteremko kuelekea chini kumbe eneo lile ni jengo la jeshi

Tukacheza mchezo wa kuteleza baadae tukaona maenmbe eneo kama kita mbili tukaenda kuangua maembe.

Dak hazikuisha akaja mjeda akatuliza mna njaa sana ndo maana mnaangua maembe machanga tuliitikia ndio tuna njaa. Mjeda akatwambia tumfuate tulachukue biskut...mzee tukamfuata, kufika pale akasema biskut hakuna kuna wali tukamwambia huohuo.

Tulikuwa wanne nakumbuka alipakua wali ndoo nzima ya lita 20 ikakaribia kujaa akaweka na maharage tukaanza kula....tumekula kula kulaaaa weeee kitu haipungui, ye yupo anaingia ndani anatoka anatuuuliza vipi niwaongeze. Tumekula mzee matumbo ndiiiiiiiii...akasema kama mna kiu kuna maji hapa kwa ile shibe tukachukua maji kunywaaa...balaa zaidi tumbo limejaaa kinyama... akakomaa kuwa hakuna kuindoka hadi mmalize maana ninyi mnaangua embe changa kwa sbb ya njaa. Tukaendelea kula baada nakumbuka dogo mmoja tulikuwa tunamwita Makumbi akaanza kulia kuwa ameshiba sana hawez kuendelea kula...mj3da akachukua rula akaanza kumpiga vidoleili dogo ale akaendelea kula....sisi kuona vile tukakomaa kula lkn wapi. Hatukufanikiwa kumaliza baada ya hapo tulikula bakora za kutosha kwa nn tumesgundwa kumaliza chakula wakati tulikuwa na njaa iliyosabisha kuangua embe mbichi ... kuanzia hapo sijawahi kukanyaga tena eneo la jeshi...naheshimu sehemu hizo.
 
Amani inaletwa na kulindwa na wewe raia.
Kama wanajeshi nchi zote duniani Zina wanajeshi lakini haujiulizi kwanini nchi nyingine hazina amani na bado Zina WANAJESHI wa kuwalinda?
Hapa Baba umepuyanga kweli, Jamaa kamjibu vizuri tu, jukumu la msingi Kuilinda Mipaka ya Nchi huko kufye, ni usafi wa kawaida tu, akatolea mfano, kama yeye anavyofua box yake.

Unadhani jukumu la msingi la jeshi, haliwezi kufanana jukumu la jeshi lingine.

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Hao jamaa utamu wao wapewe mission zinazofanana na za kigaidi gaidi , yaani wanakuwa kama wanaibukia ibukia

Kama adui wamejikusanya sehemu fulani hao jamaa wapelekwe wakiwa wamejichanganya na raia hiyo kazi baada ya hapo maadui wataelewa mbona
Movie gani hii mkuu
 
Pole

Kazi zenye viapo mtu akikwambia majukumu yake ni sawa na kutoa siri.
Hivyo basi njia rais ni kwenda sehemu husika wanakupa majibu.
Jamii forum wameshinda kesi yao inayohusu uhuru wa kupeana habari ila tutambue hakuna uhuru usio na mipaka...hata nyumbani kwako kuna vinavyokaa sebuleni na vinavyo kaa chumbani...na mwilini mwako kuna nguo inayovaliwa nje na nyingine ndani...ukienda tofauti jamii itakuona tofauti na tunaishi km jamii na hili ni jukwaa la jamii
We subiri mtu humu aminywe Kende ndo akili itawakaa sawa
 
Majukumu ya kila siku hayapangwi kwa cheo chako yanapangwa kulingana na kitengo ulichopo
Mfano cpl ni MP, majukumu yake yatapangwa na mp kamanda na kuhusu mambo yao ya mp, yani mp's wote majukumu yao yatakuwa sawa kuanzia private na vyeo vyengine
Haiwezekani cpl wa lugalo na cpl airwing majukumu yao yawe sawa kisa wana cheo kimoja, bali majukumu yatakuwa tofauti kulingana na vitengo walivyopo
Mnaweza wote mkawa macpl ila mwengine yupo ofisi ya IO, UPM, MP, KARANI, HOSPITALI, UJENZI, DEREVA NK
 
Hahahaha una mda gani kwny chombo wewe???Nikukumbushe tuu kuna Ma IO wengine sio makamisheni Officers wapo ma IO ma Copro wapo mpaka ma sargent mzee japo tumezoea kuona Most of namba kumi ni Kamisheni Officers lkn pia sio kila IO yupo Chini ya CDF kuna ma IO wengine wopo kwa ajiri ya AMIRI JESHI MKUU na co CDF Japo CDF yy anajua wapo chini yake lkn kiuhalisia hawapo chini yake ni ma undercover wa AMIRI JESHI MKUU uwezi nielewa hapa na nitaishia hapa hapa....sasa CDF Ajaribu kuingiza mtu ambae hana sifa undercover IO ajue afu uone hatua za kinidhamu zinavyochukuliwa.....
Upo sahihi kabisa
 
Hata polisi majukumu yao yanapangwa kwa kitengo chako sio cheo chako mfano wote mnaweza macpl lkn mmoja akawa trafki, mwengine dereva mwengine ffu
Kwahiyo kamwe huwezi kujua majukumu ya kila cheo jeshini hata wanajeshi wenyewe hawajui
Cpl jkt itende mbeya hawezi kujua majukumu ya cpl comando ngerengere au majukumu ya cpl wa 603 airwing au majukumu ya cpl wa navy
Ukitaka kujua majukumu ya vitengo nenda vikosini kwao ukawaulize, ukitaka kujua majukumu ya kila siku ya commando nenda ngerengere watakwambia ukitaka kujua majukumu ya jeshi la anga nenda aiwing ukitaka kujua majukumu ya jeshi la wanamaji nenda navy ukitaka kujua majukumu ya jkt nenda kikosi cha jkt kilichopo karibu nawe wanakuelezea bila shida yoyote

Ahsante nadhani umeelewa [emoji1317][emoji1317]
 
Hukua na sababu hata moja ya kuandika hivi.
Sioni ulazima wake.
 
Back
Top Bottom