Nahitaji kumpima DNA za Mtoto, Naomba kufahamu taratibu za upimaji

Nahitaji kumpima DNA za Mtoto, Naomba kufahamu taratibu za upimaji

Hakuna changamoto yoyote.
Mwanzo nilimkubali na kumuhudumia kama wangu.
Na hata mwezi wa 12 (wakati wa likizo) alikuwa kwangu.

Changamoto ni mdomo wa mama ake.
Kuna mambo huwa anaongea akiwa na jazba YANANIPA MASHAKA SANAA..!! na kunirudisha mwanzo kabisaa nilipokataa Momba.

#YNWA
Sawa mkuu, changamoto ni zile zile Kumbe. Fanya DNA
 
Ningekushauri uanze kupima hata vipimo vya awali,ambavyo ni Blood Group ya mtoto.. Mtoto hurithi group la damu kutoka kwa baba na mama.

Mfano,kama Mama ni group O na Baba ni group B, mtoto anaye zaliwa hawezi kuwa na group nje ya O ama B.

Mama kama ana Group O na Baba ni group O,then mtoto anaye zaliwa hawezi kuwa na group tofaut na O.

Nakushauri uanzie hapo kwanza,ingawa siyo accurate sana kwa sababu group lako linaweza kumatch pia na huyo aliye zaa naye ila inakupa uelekeo fulani.
hii si kweli hata kdg
tumeona mtu anaumwa si baba wala mama wanashindwa mtolea damu kwa sababu hawana group 1 la damu
 
Huduma za uchunguzi wa vinasaba hutolewa kwa mujibu wa Sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009.Taratibu zifuatazo hufuatwa ili kuweza kupata huduma za uchunguzi;-

1. Mteja anayehitaji kupatiwa huduma za uchunguzi wa Vinasaba anawakilishwa na taasisi zilizotajwa kwenye sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya Mwaka 2009 ili kumuombea mteja husika huduma za uchunguzi

2. Kwa mujibu wa kifungu cha 25(2) cha Sheria ya vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009, taasisi zinazoruhusiwa kumuombea mteja kupatiwa huduma za uchunguzi wa vinasabani pamoja na
  • Maafisa ustawi wa jamii
  • Mawakili
  • Mahakama katika uchunguzi unaolenga kutataua migogoro
  • Jeshi la polisi kwa masuala yanayohusu jinai
  • Madakatari kwa uchunguzi unaihusiana na tiba
  • Wakuu wa Wilaya
  • Taasisi za Tafiti zinazotambuliwa Kisheria
3. Taasisi hizo zitaandika barua za maombi ya kupatiwa huduma za uchunguzi kwa niaba ya mteja husika. Barua zote zitaandika kwenda kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali.

4. Malipo ya uchunguzi ni Tsh100, 000/=kwa sampuli ya mtu mmoja, hivyo kwa uchunguzi wa Baba, Mama na Mtoto jumla niTsh.300,000/=. Malipo yote hufanyika Benki.

5. Baada ya kukamilisha taratibu za malipo, sampuli za mpanguso wa kinywa(Buccal swab ) zitachukuliwa na watalaam katika maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi kulingana na Maombi ya Mteja.

6. Uchunguzi utafanyika na utakapokamilika majibu ya uchunguzi yatatolewa kwa taasisi iliyoandika barua ya maombi ya kufanyiwa uchunguzi na mteja husika atapata majibu yake kupitia taasisi hizo zilizoruhusiwa kisheria.

7. Majibu ya uchunguzi hutolewa kuanzia siku ya kumi na nne za kazi baada ya kuchukuliwa kwa sampuli.
 
Hakuna la maana kwa hayo mambo kwanza ukizingatia si mke wako,
Mlee mtoto kama wa ndugu yako tu achana na hayo mawazo ya kishetani!
Yaani kuwa na uhakika na jambo ndiyo siku hizi mnaita mawazo ya Kishetani? Kweli jamii ya sasa ipo spidi na ni ya kinyonge sana. Mara mia ukachukue watoto mtaani ulee kuliko wa kubambikiwa.
 
Mtafute afisa ustawi wa jamii maeneo ulipo, Ongea naye akuandalie barua (Japo huwa wagumu sana kukubali) Nenda mahakamani fungua shauri la kupima DNA nenda kwa mkemia mkuu na nyaraka na vielelezo fanya malipo (laki moja kwa test 1 kwa hiyo kwa test yako na mtoto ni laki 2) mtachukuliwa samples, utasubiri majibu.
Asante.
Hii ndio poa maana naifanya kimafia na kimyaaa sanaaaa.

#YNWA
 
INTRODUCTION
Mimi ni mwanaume
Nina miaka 33
Ni mtumishi wa Halmashauri moja wapo nchini
Nina mabinti wawili wa kwanza miaka 8 na wapili miaka mi3.

SCENARIO
Binti wa kwanza. Huyu ni mtoto wangu pure, yaani kila kitu ni Mimi. Ni copy ya sura na vitu vingi sanaa.

Binti wa pili.
Huyu ndio nahisi kuna TATIZO. Kifupi Kuna mambo mengi sanaa yametokea ambayo yanatia mashaka.

Watoto wangu kila mmoja na mama yake. Mwanamke wa mtoto wa pili ni mwanamke mwenye mdomo sanaaa. Na ukitaka siku yako iharibike "Hebu uongelee baba wa huyu mtoto ni nani?"

Hapo mwanzo alipozaliwa nilikataa mimba.
Ila baada ya wazazi nao kuingilia kati ilibidi nimkubali mtoto. Ila sasa Kuna mambo yanaendelea NDIO yananipa utata. Nahitaji kujua ukweli mapema.

Nimeandaa laki 6 kwa zoezi la upimaji DNA
1. Je inatosha?
2. Na procedure ni zipi?

THE PROBLEM.
Moyo wangu umegoma kabisaa kuwa na amani na huyu mtoto wa pili. Before it's to let nahitaji kupata ukweli.

#YNWA
hapo halmashauri unapofanya kazi hakuna afisa wa ustawi wa jamii? huyo ndiye atakushauri zaidi kuhusu taratibu.
 
Ningekushauri uanze kupima hata vipimo vya awali,ambavyo ni Blood Group ya mtoto.. Mtoto hurithi group la damu kutoka kwa baba na mama.

Mfano,kama Mama ni group O na Baba ni group B, mtoto anaye zaliwa hawezi kuwa na group nje ya O ama B.

Mama kama ana Group O na Baba ni group O,then mtoto anaye zaliwa hawezi kuwa na group tofaut na O.

Nakushauri uanzie hapo kwanza,ingawa siyo accurate sana kwa sababu group lako linaweza kumatch pia na huyo aliye zaa naye ila inakupa uelekeo fulani.
Biology ilikupita kushoto
 
Mtafute afisa ustawi wa jamii maeneo ulipo, Ongea naye akuandalie barua (Japo huwa wagumu sana kukubali) Nenda mahakamani fungua shauri la kupima DNA nenda kwa mkemia mkuu na nyaraka na vielelezo fanya malipo (laki moja kwa test 1 kwa hiyo kwa test yako na mtoto ni laki 2) mtachukuliwa samples, utasubiri majibu.
Umeeleza sawia
 
Back
Top Bottom