Nahitaji kumpima DNA za Mtoto, Naomba kufahamu taratibu za upimaji

Nahitaji kumpima DNA za Mtoto, Naomba kufahamu taratibu za upimaji

INTRODUCTION
Mimi ni mwanaume
Nina miaka 33
Ni mtumishi wa Halmashauri moja wapo nchini
Nina mabinti wawili wa kwanza miaka 8 na wapili miaka mi3.

SCENARIO
Binti wa kwanza. Huyu ni mtoto wangu pure, yaani kila kitu ni Mimi. Ni copy ya sura na vitu vingi sanaa.

Binti wa pili.
Huyu ndio nahisi kuna TATIZO. Kifupi Kuna mambo mengi sanaa yametokea ambayo yanatia mashaka.

Watoto wangu kila mmoja na mama yake. Mwanamke wa mtoto wa pili ni mwanamke mwenye mdomo sanaaa. Na ukitaka siku yako iharibike "Hebu uongelee baba wa huyu mtoto ni nani?"

Hapo mwanzo alipozaliwa nilikataa mimba.
Ila baada ya wazazi nao kuingilia kati ilibidi nimkubali mtoto. Ila sasa Kuna mambo yanaendelea NDIO yananipa utata. Nahitaji kujua ukweli mapema.

Nimeandaa laki 6 kwa zoezi la upimaji DNA
1. Je inatosha?
2. Na procedure ni zipi?

THE PROBLEM.
Moyo wangu umegoma kabisaa kuwa na amani na huyu mtoto wa pili. Before it's to let nahitaji kupata ukweli.

#YNWA
Una laki ya chap apo Kwana uje tuongee pm
 
Huduma za uchunguzi wa vinasaba hutolewa kwa mujibu wa Sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009.Taratibu zifuatazo hufuatwa ili kuweza kupata huduma za uchunguzi;-

1. Mteja anayehitaji kupatiwa huduma za uchunguzi wa Vinasaba anawakilishwa na taasisi zilizotajwa kwenye sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya Mwaka 2009 ili kumuombea mteja husika huduma za uchunguzi

2. Kwa mujibu wa kifungu cha 25(2) cha Sheria ya vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009, taasisi zinazoruhusiwa kumuombea mteja kupatiwa huduma za uchunguzi wa vinasabani pamoja na
  • Maafisa ustawi wa jamii
  • Mawakili
  • Mahakama katika uchunguzi unaolenga kutataua migogoro
  • Jeshi la polisi kwa masuala yanayohusu jinai
  • Madakatari kwa uchunguzi unaihusiana na tiba
  • Wakuu wa Wilaya
  • Taasisi za Tafiti zinazotambuliwa Kisheria
3. Taasisi hizo zitaandika barua za maombi ya kupatiwa huduma za uchunguzi kwa niaba ya mteja husika. Barua zote zitaandika kwenda kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali.

4. Malipo ya uchunguzi ni Tsh100, 000/=kwa sampuli ya mtu mmoja, hivyo kwa uchunguzi wa Baba, Mama na Mtoto jumla niTsh.300,000/=. Malipo yote hufanyika Benki.

5. Baadaya ya kukamilisha taratibu za malipo, sampuli za mpanguso wa kinywa(Buccal swab ) zitachukuliwa na watalaam katika maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi kulingana na Maombi ya Mteja.

6. Uchunguzi utafanyika na utakapokamilika majibu ya uchunguzi yatatolewa kwa taasisi iliyoandika barua ya maombi ya kufanyiwa uchunguzi na mteja husika atapata majibu yake kupitia taasisi hizo zilizoruhusiwa kisheria.

7. Majibu ya uchunguzi hutolewa kuanzia siku ya kumi na nne za kazi baada ya kuchukuliwa kwa sampuli.
kumekuwa na malalamiko ya majibu ya uongo ili kuepusha mtoto kukosa matunzo

wazo langu, dawa ni kupeleka sample 2 hadi 4 za baba ili wajimix kwenye majibu yao
 
Mimi mwenyewe nishatia mimba demu wa mtu alafu nikamwambia mpe huyo jamaa yako.

Kifupo tu kuwa makini na wanawake hasahasa kwenye mimba. Kuwa makini mno, wengi wanalea Watoto sio wao
 
Tafuta mwanasheria atakusaidia. Mind yu kuna kiapo utaapa kwanza hata ikijulukana mimi sio biological father of this child bado ntaendelea kumlea kumhudumia MUNGU NISAIDIE. Unashusha mkono unasaini chini ya kamishina wa kiapo. Bro kinachofata utaambiwa mtoto ni wako either ni wako au si wako majibu utapewa kuwa 100%. Mtoto ameonekana ni wako. Muhimu ni afya yako ya akili. Either ni wako sio wako usihangaike. Ni cheki Dm nikusaidie ushauri mkuu
 
INTRODUCTION
Mimi ni mwanaume
Nina miaka 33
Ni mtumishi wa Halmashauri moja wapo nchini
Nina mabinti wawili wa kwanza miaka 8 na wapili miaka mi3.

SCENARIO
Binti wa kwanza. Huyu ni mtoto wangu pure, yaani kila kitu ni Mimi. Ni copy ya sura na vitu vingi sanaa.

Binti wa pili.
Huyu ndio nahisi kuna TATIZO. Kifupi Kuna mambo mengi sanaa yametokea ambayo yanatia mashaka.

Watoto wangu kila mmoja na mama yake. Mwanamke wa mtoto wa pili ni mwanamke mwenye mdomo sanaaa. Na ukitaka siku yako iharibike "Hebu uongelee baba wa huyu mtoto ni nani?"

Hapo mwanzo alipozaliwa nilikataa mimba.
Ila baada ya wazazi nao kuingilia kati ilibidi nimkubali mtoto. Ila sasa Kuna mambo yanaendelea NDIO yananipa utata. Nahitaji kujua ukweli mapema.

Nimeandaa laki 6 kwa zoezi la upimaji DNA
1. Je inatosha?
2. Na procedure ni zipi?

THE PROBLEM.
Moyo wangu umegoma kabisaa kuwa na amani na huyu mtoto wa pili. Before it's to let nahitaji kupata ukweli.

#YNWA
Bora uache, unless ukajaribu kupima nje ya nchi, maana niliwai soma humu hata kama sio wako watasema ni wako, lengo ni kupunguza watoto wa mitaani/wasio na walezi.
 
Tafuta mwanasheria atakusaidia. Mind yu kuna kiapo utaapa kwanza hata ikijulukana mimi sio biological father of this child bado ntaendelea kumlea kumhudumia MUNGU NISAIDIE. Unashusha mkono unasaini chini ya kamishina wa kiapo. Bro kinachofata utaambiwa mtoto ni wako either ni wako au si wako majibu utapewa kuwa 100%. Mtoto ameonekana ni wako. Muhimu ni afya yako ya akili. Either ni wako sio wako usihangaike. Ni cheki Dm nikusaidie ushauri mkuu
Hakika,
 
Yaani kuwa na uhakika na jambo ndiyo siku hizi mnaita mawazo ya Kishetani? Kweli jamii ya sasa ipo spidi na ni ya kinyonge sana. Mara mia ukachukue watoto mtaani ulee kuliko wa kubambikiwa.
Sisi kwa unafki bhana eti Bora ukachukue mtoto wa mtaana!
 
Sisi kwa unafki bhana eti Bora ukachukue mtoto wa mtaana!
Siyo unafiki, hiyo maana yake kuliko kuletewa kwa kugeuzwa tutusa. Mtoto wa hivyo ana haki zote za kulelewa na wengine ila siyo huyo aliyebambikiwa.
Haya mambo ya kuchukulia vitu kiwepesi ndiyo maana siku hizo hata kugeuzwa ninyi mnaona ni poa tu na ni haki yenu pia.
 
Back
Top Bottom