Nahitaji kumpima DNA za Mtoto, Naomba kufahamu taratibu za upimaji

Sawa mkuu, changamoto ni zile zile Kumbe. Fanya DNA
 
hii si kweli hata kdg
tumeona mtu anaumwa si baba wala mama wanashindwa mtolea damu kwa sababu hawana group 1 la damu
 
Huduma za uchunguzi wa vinasaba hutolewa kwa mujibu wa Sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009.Taratibu zifuatazo hufuatwa ili kuweza kupata huduma za uchunguzi;-

1. Mteja anayehitaji kupatiwa huduma za uchunguzi wa Vinasaba anawakilishwa na taasisi zilizotajwa kwenye sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya Mwaka 2009 ili kumuombea mteja husika huduma za uchunguzi

2. Kwa mujibu wa kifungu cha 25(2) cha Sheria ya vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009, taasisi zinazoruhusiwa kumuombea mteja kupatiwa huduma za uchunguzi wa vinasabani pamoja na
  • Maafisa ustawi wa jamii
  • Mawakili
  • Mahakama katika uchunguzi unaolenga kutataua migogoro
  • Jeshi la polisi kwa masuala yanayohusu jinai
  • Madakatari kwa uchunguzi unaihusiana na tiba
  • Wakuu wa Wilaya
  • Taasisi za Tafiti zinazotambuliwa Kisheria
3. Taasisi hizo zitaandika barua za maombi ya kupatiwa huduma za uchunguzi kwa niaba ya mteja husika. Barua zote zitaandika kwenda kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali.

4. Malipo ya uchunguzi ni Tsh100, 000/=kwa sampuli ya mtu mmoja, hivyo kwa uchunguzi wa Baba, Mama na Mtoto jumla niTsh.300,000/=. Malipo yote hufanyika Benki.

5. Baada ya kukamilisha taratibu za malipo, sampuli za mpanguso wa kinywa(Buccal swab ) zitachukuliwa na watalaam katika maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi kulingana na Maombi ya Mteja.

6. Uchunguzi utafanyika na utakapokamilika majibu ya uchunguzi yatatolewa kwa taasisi iliyoandika barua ya maombi ya kufanyiwa uchunguzi na mteja husika atapata majibu yake kupitia taasisi hizo zilizoruhusiwa kisheria.

7. Majibu ya uchunguzi hutolewa kuanzia siku ya kumi na nne za kazi baada ya kuchukuliwa kwa sampuli.
 
Hakuna la maana kwa hayo mambo kwanza ukizingatia si mke wako,
Mlee mtoto kama wa ndugu yako tu achana na hayo mawazo ya kishetani!
Yaani kuwa na uhakika na jambo ndiyo siku hizi mnaita mawazo ya Kishetani? Kweli jamii ya sasa ipo spidi na ni ya kinyonge sana. Mara mia ukachukue watoto mtaani ulee kuliko wa kubambikiwa.
 
Asante.
Hii ndio poa maana naifanya kimafia na kimyaaa sanaaaa.

#YNWA
 
kitanda hakizai haramuuu ... mstahi mwenzio
 
hapo halmashauri unapofanya kazi hakuna afisa wa ustawi wa jamii? huyo ndiye atakushauri zaidi kuhusu taratibu.
 
Biology ilikupita kushoto
 
Umeeleza sawia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…