Nahitaji kumpima DNA za Mtoto, Naomba kufahamu taratibu za upimaji

Nahitaji kumpima DNA za Mtoto, Naomba kufahamu taratibu za upimaji

Unamwadhibu mtoto kwa mdomo wa mamaye?
Hivi ukimlea na mtoto akakua akitambua wewe ni babaye utapungukiwa nini?
Ukagundua sio mwanao pia utsongezewa nini?

Fanya kumtunza mtoto kama utumishi kwa Mungu.
Ukiwaza sana mambo haya utagundua umetanguliza ubinafsi.

Ni viumbe wachache watanielewa, wengine wataropoka tu.

Nhona nimwite afisa ustawi wa jamii #nyau# Joannah
Nimesikitika Sana, Ila matendo ya Mungu yalivyo ya ajabu majibu ya huyo mtoto lazima yatoke ni wake,halafu huyo anaedhani ni wake ndio ukute si wake.....mi namshauri aachane na hizo Mambo mtoto ni baraka, huwezi jua atakufaa nn mbeleni
 
Nakupa angalizo:
Ukienda kupima DNA vaa kandambili na nguo zilizochoka na hata nywele usichane , hao jamaa Wana kawaida ya kumpa MTU mtoto hata kama sio wako na usijichanganye ukaenda umependeza watakupa Tu mtoto.
 
Nimesikitika Sana, Ila matendo ya Munguauri bora kabisa, nimekupenda bure yalivyo ya ajabu majibu ya huyo mtoto lazima yatoke ni yake,halafu huyo anaedhani ni wake ndio ukute si wake.....mi namshauri aachane na hizo Mambo mtoto ni baraka, huwezi jua atakufaa nn mbeleni
UShauri bora kabisa, nimekupenda bure
 
Mtu akishapanick hua anaropoka ambayo aliyaficha bila kutarajia..

Nina Ndugu yangu aliuwawa tabata ikisingiziwa kajinyonga(jina kumbuka mwenyewe)kifo chake kili trend sana kama mna kumbukumbu

Aliachana na aliyezaa naye, ikawa wakigombana anamuambia
"kwanza mimi ndio najua baba wa mtoto ni nani"

Hio kauli asaivi ndio inaleta shidaa, Mama ndio huyo kafariki, baba akikumbuka mama alichokua anamuambia anaona kbsa huyu sio mwanae,
Baba kakaataa kumlea(hilo sio shida ndugu tunalea) ila mtoto anabaki yatima sasa ikiwa baba tunaimani yupo, Pengne ni mwingine lakini ndio hatutomjua daima, au ni huyu huyu ila aliongea kama kumuonesha dharau, maana kwa hilo halikua shida kwake.

Ni kitu inatuuma ukimuangalia yule mtoto.
Mh hapa tolu fundi 📱 anahusika, ngoja ninyamaze.
 
Mzee wa kataa ndoa yamemkuta

Mnasema mnakataa ndoa sasa imekuwaje na 😅😅wewe huna Ndoa?

Utajinyonga shauli yako

Kataa ndoa has a price, na kati gharama zake ndiyo hizo. So, asikimbie gharama za kataa ndoa.
Au alidhani kataa ndoa ni kawimbo fulani?

Watabambikiwa kila kona

Liverpool VPN Nilikwambia mkuu kupiga makampeni humu ya kuhalalisha ufuska hayakusaidii kitu, unaona sasa unahangaika kwa mkemia mkuu saa hizi, haya sasa ndio matokeo yake.

Namcheka bwana Livapuli. Stress za wana ndoa na yeye zinampata vile vile

Hajui duniani ni nginjanginja mpaka mbinguni ndio tutapumzika🤣🤣

Sikieni....

1. Mi sio muumini wa ndoa na wala siamini kwenye ndoa.

2. Kuwa na ndoa hakukufanyi usibambikiwe mtoto.

3. Mama wa mtoto wa kwanza ni mstaarabu na mtiifu kweli.
Na isitoshe mtoto wake nimefanana nae copy kabisaaaa

4. Mama wa mtoto wa pili ndio simuelewagi, kwanza ana mdomo balaaa na huwa anaongea maneno ambayo siyaelewi kabisaaaa.

5. Sina stress kabisa kwasababu tokea mimba huyu mwanamke sikumuelewa kabisaaa

6. Na sasa ndio zile hisia zangu zinajithibitisha kwa maneno yake.

7. Nachotaka ni ukweli tu nijue "JE NI MWANANGU?" Basi ili nimuhudumie nikijua ni wangu au sio.

#YNWA
 
Hata ukigundua sio wako mlee hakikisha jina shuleni la baba linakuwa lako msichana ni Mali nijuavyo mimi
 
Huduma za uchunguzi wa vinasaba hutolewa kwa mujibu wa Sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009.Taratibu zifuatazo hufuatwa ili kuweza kupata huduma za uchunguzi;-

1. Mteja anayehitaji kupatiwa huduma za uchunguzi wa Vinasaba anawakilishwa na taasisi zilizotajwa kwenye sheria ya Vinasaba vya Binadamu ya Mwaka 2009 ili kumuombea mteja husika huduma za uchunguzi

2. Kwa mujibu wa kifungu cha 25(2) cha Sheria ya vinasaba vya Binadamu ya mwaka 2009, taasisi zinazoruhusiwa kumuombea mteja kupatiwa huduma za uchunguzi wa vinasabani pamoja na
  • Maafisa ustawi wa jamii
  • Mawakili
  • Mahakama katika uchunguzi unaolenga kutataua migogoro
  • Jeshi la polisi kwa masuala yanayohusu jinai
  • Madakatari kwa uchunguzi unaihusiana na tiba
  • Wakuu wa Wilaya
  • Taasisi za Tafiti zinazotambuliwa Kisheria
3. Taasisi hizo zitaandika barua za maombi ya kupatiwa huduma za uchunguzi kwa niaba ya mteja husika. Barua zote zitaandika kwenda kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali.

4. Malipo ya uchunguzi ni Tsh100, 000/=kwa sampuli ya mtu mmoja, hivyo kwa uchunguzi wa Baba, Mama na Mtoto jumla niTsh.300,000/=. Malipo yote hufanyika Benki.

5. Baadaya ya kukamilisha taratibu za malipo, sampuli za mpanguso wa kinywa(Buccal swab ) zitachukuliwa na watalaam katika maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi kulingana na Maombi ya Mteja.

6. Uchunguzi utafanyika na utakapokamilika majibu ya uchunguzi yatatolewa kwa taasisi iliyoandika barua ya maombi ya kufanyiwa uchunguzi na mteja husika atapata majibu yake kupitia taasisi hizo zilizoruhusiwa kisheria.

7. Majibu ya uchunguzi hutolewa kuanzia siku ya kumi na nne za kazi baada ya kuchukuliwa kwa sampuli.
Asante sana
 
Sikieni....

1. Mi sio muumini wa ndoa na wala siamini kwenye ndoa.

2. Kuwa na ndoa hakukufanyi usibambikiwe mtoto.

3. Mama wa mtoto wa kwanza ni mstaarabu na mtiifu kweli.
Na isitoshe mtoto wake nimefanana nae copy kabisaaaa

4. Mama wa mtoto wa pili ndio simuelewagi, kwanza ana mdomo balaaa na huwa anaongea maneno ambayo siyaelewi kabisaaaa.

5. Sina stress kabisa kwasababu tokea mimba huyu mwanamke sikumuelewa kabisaaa

6. Na sasa ndio zile hisia zangu zinajithibitisha kwa maneno yake.

7. Nachotaka ni ukweli tu nijue "JE NI MWANANGU?" Basi ili nimuhudumie nikijua ni wangu au sio.

#YNWA
Sawa ndugu. Na sie ndo hivyo hivyo
 
S

Sio muumini wa ndoa ila unataka mazao ya ndoa
 
Unamwadhibu mtoto kwa mdomo wa mamaye?
Hivi ukimlea na mtoto akakua akitambua wewe ni babaye utapungukiwa nini?
Ukagundua sio mwanao pia utsongezewa nini?

Fanya kumtunza mtoto kama utumishi kwa Mungu.
Ukiwaza sana mambo haya utagundua umetanguliza ubinafsi.

Ni viumbe wachache watanielewa, wengine wataropoka tu.

Nhona nimwite afisa ustawi wa jamii #nyau# Joannah
Mbona hata sasa Nina wasiwasi nae ila namtunza.
Nachotaka ni ukweli JE NI DAMU YANGU au natoa matunzo kwa ufadhili ...

#YNWW
 
Back
Top Bottom