Nahitaji ushauri wa haraka sana maana nahisi Nachanganyikiwa sasa

Nahitaji ushauri wa haraka sana maana nahisi Nachanganyikiwa sasa

Pole sana.

Usaliti ni kosa lisilo na Msamaha. Uliza popote pale sio mbinguni, kuzimu wala duniani.

Wengine watakudanganya usamehe ilhali utakuwa unajidanganya huku moyo ukiendelea kuumia.

Zingatia, kama hujawahi kumsaliti unahaki ya kumuacha.
 
Habari wanajamvi naandika Bango Hili nikiwa sijui nini nifanye na nikiwa nimechanganyikiwa Kwa Yaliyotokea na sielewi hili.wala lile.

IKo hivi Mimi ni Kijana mwenye Umri wa Miaka 46, Nilikuwa nina Mke wangu ana Umri wa Miaka 34 Tulikuwa Tunaishi naye lakini kutokana na mambo Ya kimajukumu Ukabidi Niende Dodoma kama miezi mitano au sita Ilopita Na yeye Nikamuacha Tabora.

Tulikuwa tunawasiliana Vizuri tu na kuna kipindi Ilitokea Shida kidogo mwezi mmoja baada ya mimi Kuondoka, Kulitokea Hitilafu Kwenye Ujenzi tunaofanya hapo Kahama kwakuwa nilikuwa mbali na yeye Ni mfanyakazi wa Serkali nikamuomba akakope Pesa Kiasi halafu nitakuja Kufidishia (Ndiyo Tinavyofanya siku zote).

Kama Jukumu likiwa la kwangu na yeye akiwa na means ya kufanya bhasi anafanya Mimi naandika deni.

Kwakuwa Benki walikuwa wanachelewa Ikabidi aende kwa wanaoacha Kadi akafanikiwa na kupata pesa na kila mwezi akawa anakatwa pesa zake na alikuwa anafata kiasi kinachobaki hapo ofisini..

Wiki Moja kabla nikawa Nahisi Kama Kuna uwezekano Mke wanhu ananisaliti (Mimi ni mtu wa Kufanya Sana Meditation Hivyo Hisia zikinijia bhasi lazma nizifanyie Meditation Kwa siku angalau mbili na huwa napewa clear Picture)..

Kipindi nafanya Meditation nikawa naona kabisa Mke wangu ananisaliti sasa Baada ya miezi minne kuondoka huko Nikawa namuuliza Huko ni salama mbona kama kuna kitu kibaya unafanya jibu lake hakuna shida yoyote.

Guyz huyo jamaa wa Microfinace simjui na Sijakutana naye ila kuna kitu kikawa kina niambia nimuulize Wife na nimkazanie kuhusu Huyo mtu kwa nguvu mpaka aseme ikibidi Nitumie uongo wowote kama mwanaume..

Nilifanikiwa Kimlazimisha na kumuuliza hatimaye akaamua kugunguka kuwa yule Jamaa wa Microfinace alimbaka Yeye alipokuwa Ofisini kwake Kuchukua Kiasi cha Pesa Kilichobaki na wala haikuwa dhamiri yake.

Nikamuiliza Umereport tukio hilo akajibu "Hapana"
Nikamuuliza Ulipiga kelele akajibu "Hapana maana nisingesikika wala watu wasingeniamini"

Nikawaza sana huyu Wife nimezaa Naye watoto watatu..
Na anassma alimbaka Miezi minne Exactly tangu nilivyoondka ila nisingemuuliza Nadhani ingeendelea Kuwa story ya siri yake..

Ninawaza kumpa Talaka Tatu ila bado nahofu na watoto wangu Nimempa Talaka 2 ila akili yangu bado inaona nimeumizwa sana nastahili kufanya kitu ila bado moyo unavuja damu nifanye nini??

Naombeni wan JF mnishauri Nifanye Nini maana naumia Sana.

Na kwa maelezo yake Bado siamini kabisa.

Naombeni sana Ushauri maana ametishia Kujiua endapo sitamrejea
Watu wa 'Kataa Ndoa' kila siku iendayo kwa Mungu wanazidi kujikusanyia Points.
 
Kwanza kabisa nyundo 46 wewe si kijana bali mzee aliechangamka, pili kwa kuwa tayali wewe ni mzee achana na mbanga za talaka angalia namna ya kumalizana na mzee mwenzio kwa maslahi mapana ya watoto wenu
 
Pole sana. Inaonekana ulikuwa unamwamini sana mke wako. Tuko wengi tuliopitia haya mambo. Sema wewe ulitakiwa usiwe na papara, unyate mpaka uwakamate. Ushauri wangu: Mwambie huyo mke wako aende polisi akatoe habari na anaseme kuwa alitishiwa maisha ndiyo maana akaogopa kufanya lolote. Bila shaka kwa Tanzania, itakuwa ngumu sana kuthibisha huo ubakaji, ila utakuwa angalau ''umemtingisha'' huyo mla mali za watu. Na kama ana mke, fanya mpango mke wake ajue. Ukienda polisi jiandae kuwa na fedha ya kuhonga na mbaya zaidi kama huyo jamaa ana fedha zaidi yako itakuwa kesi ngumu.
Usimdanganye mwenzio shekh.
Hapo hakuna kesi, na hiyo ilikua ni makubaliano ya hiyari.
Kwa ushauri huu, naona unaenda kumuingiza jamaa kwenye aibu nyingine ambayo itakua fedheha hadi kwa watoto na itawaumiza maisha yao yote.
Kimsingi jamaa hata hakupaswa kuja kuomba ushauri hapa, zaidi alipaswa aje atupe simulizi (kama angependa) kwa kilicho tokea na tayari amemuacha huyo mwanamke na ndipo aombe ushauri wa namna ya kulea watoto ama tumshauri namna ya kuanza upya.
 
Naenda kufungua Microfinance, huku pisi unabaka na zinajua zikipiga kelele hamna mtu ataamini zimebakwa.
 
Naenda kufungua Microfinance, huku pisi unabaka na zinajua zikipiga kelele hamna mtu ataamini zimebakwa.
 
Wewe hujawahi kumsaliti mkeo?
Kama jibu ndio basi achana nae km jibu hapana
Watu wenye taasisi za mikopo hutumiapesa kulaghai wanawake na Huwa na chain ya kutosha sabbu shida za watu zinasolviwa kwao kubakwa sidhani labda kumlaghai
Lakin maamuz ni Yako mwenyewe
Sijawahi kusaliti tangu Niingie ndoani
 
Wewe ndo tatizo, hela ya ujenzi unakopa ya nini..?
Ujenzi una haraka gani..?
Huyo Jamaa hakikisha unamfanya msukule, usiwaze mara mbili wala, ingia Pangani chap kwa haraka, akalimishwe nazi Tanga huko
Mkuu Umesoma Vizuri..
Ni kwamba kuna baadhi ya Vifaa vilipelea na ilikuwa inahitajika haraka..bank ingechelewa kutoka..
So ikabidi akachukue kwa Microfinance Wanakoacha kadi
 
nakushauri utafute viongozi wa kidini
Mkuu kuna kiongozi alifuatwa anusuru ndoa akaomba aongee na mwanamke, baada ya hapo mwanamke akawa mtiifu kwa mumewe jamaa akapeleka na fungu kwa mtumishi asijue mtumishi ndio anaekula mkewe kamwambia kama anataka waendelee amuheshimu mumewe akiendelea kumfatilia atawakamata.
 
Mwanaume? miaka 46 unampa mkeo talaka? hao watoto wataishije, acha ubinafsi ww! Leo familia acha masimango unampa talaka na mkopo kakuchukulia mfyuuu
 
Mkuu kuna kiongozi alifuatwa anusuru ndoa akaomba aongee na mwanamke, baada ya hapo mwanamke akawa mtiifu kwa mumewe jamaa akapeleka na fungu kwa mtumishi asijue mtumishi ndio anaekula mkewe kamwambia kama anataka waendelee amuheshimu mumewe akiendelea kumfatilia atawakamata.
Duh
 
Back
Top Bottom