Naibu Nishati: Tumelazimika kutafuta wakandarasi wa bei kubwa lakini kwa uharaka. Aahidi kadhia ya umeme kukoma Januari

Naibu Nishati: Tumelazimika kutafuta wakandarasi wa bei kubwa lakini kwa uharaka. Aahidi kadhia ya umeme kukoma Januari

Naibu waziri wa Nishati amewaomba watanzania kuwavumilia na kwasasa wanarekebisha mitambo ya gesi yenye matatizo na wanaamini kufikia Januari tatizo kama litakuwa halijapungua kabisa litakuwa limekwisha.

Naibu waziri amesema wamelazimia kuwapata wakandarasi wenye gharama kubwa kurekebisha mitambo hiyo lakini kwa uharaka ili kuweza kutatua tatizo lakini sasa wamejifunza na tatizo halitajirudia.

Pia Byabato amesema kipindi kifupi kijacho watajaza maji katika bwawa la Nyerere kufanya majaribio ya uzalishaji umeme na mpaka kukamilika kwake litagaharimu jumla ya trilioni 6.5 ambapo mpaka sasa Rais Samia ameshatoa zaidi ya trilioni 4 na ukikamilika utazidi uwezo wa Tanzania kuzalisha umeme uliopo sasa.

Idle talk
 
Yaani hawa ilitakiwa wanatolewa madarakani na kuswagwa mahakamani fasta.

Tukipata katiba mpya, tupitie mikataba yote kama huu wa mkarandasi wa gharama kubwa, Kuuzwa kwa Loliondo, matumizi ya mikopo, nk.

Watu washitakiwe resprospectively. Hata kama hawako madarakani.

Kuondoa kinga ya kutoshistakiwa kwa kiongozi yoyote kama Rais, makamu na viongozi wote itasaidia sana kuwa na uwazi wa hii mikataba tunayoingia.
 
Japokuwa kuna upungufu lakini huu mgao kuna hujuma kubwa na lengo wanalijua wao.
 
Unadhani tukiuwa wafanyakazi wa TANESCO kama 200 kwa kuwakata mashingo mchana kweupe watarudia kukata tena umeme? Ninyi hamjui tu
 
Tukipata katiba mpya, tupitie mikataba yote kama huu wa mkarandasi wa gharama kubwa, Kuuzwa kwa Loliondo, matumizi ya mikopo, nk.

Watu washitakiwe resprospectively. Hata kama hawako madarakani.

Kuondoa kinga ya kutoshistakiwa kwa kiongozi yoyote kama Rais, makamu na viongozi wote itasaidia sana kuwa na uwazi wa hii mikataba tunayoingia.
Swali la kujiuliza ni vigezo gani vilivyo tumika kuajiri outside sources zenye gharama kutokana na tatizo lilikuwepo?

Nature ya tatizo ni beyond ya engineers wetu?

Kwanini hawana utaalamu wa kutatua hilo tatizo? Hawana uelewa wa mechanical system nzima to how it works, na kwanini awakupewa training kabla ya kusimamia operation (there is no point of having engineers the oversee the system if they can’t do trouble shoot or repair faults).

Kwa kifupi hiyo wizara inahitaji mtaalamu. TANESCO ni technical
ni taasisi chache duniani ambazo zinataka mtaalamu wa maswala ya umeme aliefundishwa management skills. with time; sio mropokaji kama Maharage Chande.

Juzi nimemskiliza mkurugenzi wa TANESCO anaapa hakuna kufunguliwa kwa maji.

Sasa nilitegemea kwenye kuhakikisha kwake atasema tunajua kisayansi mabwawa yote ya maji yakijaa kila moja muda wake wa kuisha.

Tunapokea report ya kina cha maji kila siku na kujiridhisha kutokana na matumizi yake kisayansi na kama kuna sababu za kupungua kwa kina tofauti na sababu za kisayansi tunachunguza.

Tuna yellow and red alerts za kuchukua tahadhari kuhakikisha maji yapo na kuelezea nini kinafanyika kabla ya chanzo kukosa maji ya kuzalisha umeme..

Hila majibu yake yalikuwa ujinga mtupu ayaonyeshi kama mtu mwenye uelewa wa inventory control ya mabwawa.

Huyo waziri mwenyewe ukimsikiliza ndio salaleh, muhimu asije kujiongombea na rafiki zake wengine anaotaka kuwapa departments sensitive hawana wanachokijua.
 
Hahahahahaha naona MAGAS TURBINE ambayo hayana hata 5yrs yameanza kusumbua sasa....hivi hata warrant yamemaliza kweli au tumeviolate warrant tayari kama lile Dilimulaina la long haul tukalipeleka short haul Mwanza tukaua engine.... Hahahahaha naona anatafutiwa mtu service contract ya kurun Kinyerezi huku Tanescrow wakibaki ofisini kusubiri kulipa invoices... hahahahaha

What kind of species we are gents...
(What kind of species we are gents...)
What kind of species are we gentlemans??
 
Japokuwa kuna upungufu lakini huu mgao kuna hujuma kubwa na lengo wanalijua wao.
Kwa mtu mwenye uelewa wa ‘change management’ asingefanya upuuzi, aliofanya Makamba baada ya kuteuliwa.

Hajui hata body zinatakiwa kuwa na watu wenye sifa zipi na wala sifa za mkurugenzi.

Kwa kifupi huyu malkia wa nyuki na wazimu wa mawaziri aliotuletea; inabidi apewe salamu zake 2025 achague aende kuishi Mbweni alipojenga au tumjengee hekalu lake Kizimkazi; lakini atumtakii na tumemchoka kweli hana uwezo.
 
Mimi nilijua ni Maji pekee kumbe na Mashine nazo wanasema mbovu mbona huo ni uzembe

Raisi wangu mpendwa Samia aanze fukuzafukuza na Waandishi wa habari watembelee huko kwenye Mabwawa watupe mrejesho.
 
Ccm kwa kulindana hawajambo.bora mbwakoko tuumie wengi lakini mbwakoko mmoja akafaidi.
 
Huu mgao wa kutengeneza ilikuwa ni kuhalalisha hiyo gharama kubwa. Utawasikia tuliongea na watanzania wakatuelewa. Bila machafuko sioni tukiacha kupigwa.
 
Huku ndiko kwenye kichaka cha haya mafisadi
MKUU, KWA HESHIMA KUBWA KABISA NIKUAMBIE NA NIWAAMBIE NA WATANZANIA WOTE KUA WIZARA YA NISHATI NZIMA ILIYOPO TANZANIA IKIONGOZWA NA TANESCO NI KICHAKA CHA MAFISADI WA KUTISHA, MATAPELI WA VIWANGO VYA KUSHANGAZA, WEZI WA KUTISHA KABISA KUWAHI KUTOKEA TANGU DUNIA KUUMBWA, NA HILI NI KAMA LILE LA ESCROW NA DOWANS LINARUDI KWASTAILI NYINGINE ILA MUNGU WETU AISHIVYO IPO SIKU.
 
Mvua kubwa zimeanza huko Bara Mito imeanza kujaa ni huyu Makamba anamhujumu Mkuu wake wa kazi .

Kihansi imejaa Maji Waandishi mbona hawaendi huko ili wa expose uongo uliopo
 
Zile porojo za Umeme wa Upepo pale Kititimo Singida nazo zimeishia wapi?
 
Swali la kujiuliza ni vigezo gani vilivyo tumika kuajiri outside sources zenye gharama kutokana na tatizo lilikuwepo?

Nature ya tatizo ni beyond ya engineers wetu?

Kwanini hawana utaalamu wa kutatua hilo tatizo? Hawana uelewa wa mechanical system nzima to how it works, na kwanini awakupewa training kabla ya kusimamia operation (there is no point of having engineers the oversee the system if they can’t do trouble shoot or repair faults).

Kwa kifupi hiyo wizara inahitaji mtaalamu. TANESCO ni technical
ni taasisi chache duniani ambazo zinataka mtaalamu wa maswala ya umeme aliefundishwa management skills. with time; sio mropokaji kama Maharage Chande.

Juzi nimemskiliza mkurugenzi wa TANESCO anaapa hakuna kufunguliwa kwa maji.

Sasa nilitegemea kwenye kuhakikisha kwake atasema tunajua kisayansi mabwawa yote ya maji yakijaa kila moja muda wake wa kuisha.

Tunapokea report ya kina cha maji kila siku na kujiridhisha kutokana na matumizi yake kisayansi na kama kuna sababu za kupungua kwa kina tofauti na sababu za kisayansi tunachunguza.

Tuna yellow and red alerts za kuchukua tahadhari kuhakikisha maji yapo na kuelezea nini kinafanyika kabla ya chanzo kukosa maji ya kuzalisha umeme..

Hila majibu yake yalikuwa ujinga mtupu ayaonyeshi kama mtu mwenye uelewa wa inventory control ya mabwawa.

Huyo waziri mwenyewe ukimsikiliza ndio salaleh, muhimu asije kujiongombea na rafiki zake wengine anaotaka kuwapa departments sensitive hawana wanachokijua.
MKUU UMEFAFANUA VYEMA KABISA NA NAFURAHI PIA KUA BADO ASILIMIA KUBWA WATANZANIA TUNA AKILI SANA YA KUHOJI NA HATUWEZ KUDANGANYWA KIPUMBAVU AU KIJINGA, ILA SASA TUKIHOJI HIVI TUNAAMBIWA KUA TUNAPENDA VYA BURE, TUMEMSIKIA HUKO ARUSHA AKITUNANGA WATANZANIA KUA TUNAPENDA VYA BURE, NAONA AMEANZA KULEWA MADARAKA, AULIZIE WALIOLEWA MADARAKA WAKO WAPI KWA SASA, WENGINE NI MAREHEMU, WENGINE WAKO THE HAGUE.
 
Mvua kubwa zimeanza huko Bara Mito imeanza kujaa ni huyu Makamba anamhujumu Mkuu wake wa kazi .

Kihansi imejaa Maji Waandishi mbona hawaendi huko ili wa expose uongo uliopo
MKUU PENGINE WAMEENDA ILA WANAKUTANA NA RUSHWA WAKAE KIMYA AU NA MTUTU WA BUNDUKI. MANA UKIMYA WAO PIA UNASHANGAZA.
 
Back
Top Bottom