Naibu Rais wa Kenya maji ya shingo, akimbilia mahakamani kujaribu kuzuia kung'olewa kwenye nafasi yake

Naibu Rais wa Kenya maji ya shingo, akimbilia mahakamani kujaribu kuzuia kung'olewa kwenye nafasi yake

Naibu wa rais Kenya amelazimika kukimbilia mahakamani kujaribu kuzuia mchakato wa kubanduliwa kwake ofisini ingawa uwezekano wa bunge kumuondoa bado ni mkubwa zaidi.

Tayari wabunge wapatao 242 wameridhia muswada huo kuletwa bungeni kati ya angalau wabunge 117 waliohitajika kisheria.

Endapo spika ataridhika kwamba matakwa ya kisheria yametimizwa ataidhinisha mjadala wa hoja na kupiga kura katika kikao cha mashauriano, na iwapo theluthi mbili ya wabunge yaani wabunge 233 kati ya 349 watapiga kura ya ndiyo ili Gachagua aondolewe mamlakani, basi ni mahakama pekee ndiyo inaweza kumnusuru asalie kwenye nafasi yake kwa mujibu wa katiba ya Kenya ya 2010.

Pamoja na mambo mengine, Naibu wa Rais huyo wa Kenya Rigathi Gachagua, anatuhumiwa kukiuka katiba, kukiuka sheria za nchi, utovu wa nidhamu uliokithiri, matumizi mabaya ya ofisi na tuhuma nyingine nyingine ambazo zitawekwa wazi na mtoa hoja mapema wiki ijayo.

Ni yapi maoni yako, ajiuzulu au apambane?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Naunga mkono HOJA,

SSH must go!!
 
Huu ni unafiki mkubwa na kukosa fadhila kwa Ruto, kwasbb bila Rigathe Gachagua kumpambania asingeweza kupata kiti cha urais. Ame-play role kubwa sana.

Hiki ndicho alichokifanya Samia pia. Baada ya kifo cha jiwe, sukuma gang hawakutaka Samia ashike wadhifa wa urais....walitaka wamchezee kekundu.

Msoga gang ikasimama kidete kuhakikisha Samia anakikalia kiti. Lkn hivi sasa Samia anaisulubu Msoga gang na kuikumbatia Sukuma gang.
Interests and Betrayal are two main constants in politics gentleman 🐒
 
  • Thanks
Reactions: G4N

Attachments

  • IMG_20240929_100502_2.jpg
    IMG_20240929_100502_2.jpg
    1.5 MB · Views: 2
Huu ni unafiki mkubwa na kukosa fadhila kwa Ruto, kwasbb bila Rigathe Gachagua kumpambania asingeweza kupata kiti cha urais. Ame-play role kubwa sana.

Hiki ndicho alichokifanya Samia pia. Baada ya kifo cha jiwe, sukuma gang hawakutaka Samia ashike wadhifa wa urais....walitaka wamchezee kekundu.

Msoga gang ikasimama kidete kuhakikisha Samia anakikalia kiti. Lkn hivi sasa Samia anaisulubu Msoga gang na kuikumbatia Sukuma gang.

Samia ni genge gani??

Arab gang? Islamic Gang? Wezi Gang?

Acheni huo upumbavu wa kulishusha na kulidogosha kabila la Wasukuma.

Ukweli ni kwamba hakuna genge, kuna Kabila la Wasukuma.

Itoshe, Rais Samia anatekeleza Magulification of Africa.

Magulification must go on, hence, "Kazi iendelee"
Upo?
 
Back
Top Bottom