........Breaking News...................
Makamo wa RAIS wa KENYA muheshimiwa RIGATHI GACHAGUA,
Almaarufu wenyewe humuita NAIBU RAIS ameondolewa rasmi madarakani,
GACHAGUA ameondolewa madarakani baada ya bunge la SENETI,
Kumkuta na hatia kama alivyo kutwa na hatia na BUNG LA KITAIFA,
GACHAGUA anatuhumiwa kufanya makosa 11,
Ikiwemo kueneza ukabila, kujimbikizia mali, kuingilia mchakato wa manunuzi,
Pamoja na kufadhili maandamano ya kizazi cha mwisho yaani generation Z,
Almaarufu maandamano hayo yaliitwa GEN Z,
GACHAGUA anakua naibu RAIS wa kwanza kuondolewa madarakani,
Kwa style hii baada ya katiba mpya kutungwa mwaka 2010,
Huku mwenyewe akiwa hospitali amelazwa,
Baada ya kugua ghafla masaa machache kabla hajaondolewa madarakani,
Mara tu bunge la SENATE lilipo tangaza kmuondoa madarakani,
Taarifa rasmi ilitumwa kwa muheshimiwa RAIS wa KENYA muheshimiwa WILLIAM RUTO,
Na muda huohuo RUTO akaanza kuifanyia kazi kwani,
Muda huo huo wa usiku wa kuamkia leo,
Walinzi wote waliokuwa wanamlinda GACHAGUA,
Waliamuliwa kuondoka nyumbani kwake,
Pia waliamuliwa kuondoka hospitali alipokuwa amelazwa,
Nakumuacha peke yake na familia yake tu,
Pia magari yote ya ofisini pamoja na mali zote za ofisi ameny'anywa na kurudishwa ofisini,
Pia familia yake imetolewa nje ya nyumba ya makamo wa RAIS usiku huohuo,
Na GACHAGUA amepigwa marufuku kuonekana maeneo hayo,
GACHAGUA bado anapokea matibabu hospitalini kwa tatizo la moyo,
Ambalo limempata ghafla jana wakati akisubili matokeo ya maamuzi ya bunge la SENATE,
Kufuatia uwamuzi huo RIGATHI GACHAGUA,
Ameamua kukimbilia mahakamani kupinga kuondolewa kwake,
Na usiku huohuo mahakama imeunda time ya majaji watatu kushhungulikia jambo hilo,
Hata hivyo taarifa kutoka IKULU ya KENYA inasema,
RAIS wa KENYA muheshimiwa WILLIAM RUTO,
Muda wowote kuanzia asubuhi hii anatarajiwa kumtangaza mrithi wa GACHAGUA.
Makala hii imeletwa kwenu na Dhulkad Madara kutoka Morogoro