Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (MB) ametangaza kuivunja Bodi ya ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Mji Mdogo wa Rujewa katika Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya kwa kushindwa kuisimamia ipasavyo menejimenti ya mamlaka hiyo kutimiza majukumu yake kwa ufanisi.
Mhandisi Mahundi amechukua hatua hiyo mara baada ya kubaini ukosefu wa huduma ya uhakika ya maji kwa muda mrefu kwa wakazi wa mji wa Mbarali bila sababu za msingi.
Aidha, amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (Mbeya UWASA), Mhandisi Ndele Mengo kufanya uchunguzi ndani ya siku Nneili kubaini na kupata suluhisho la changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika wilaya hiyo.
Vilevile amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Clement Kivegalo kumuondoa Meneja wa Wilaya ya Mbarali (RUWASA), Mhandisi Job Mwakasala pamoja na kufanya mabadiliko ya wataalamu katika wilaya hiyo.
Naibu Waziri amechukua uamuzi huo kufuatia kutoridhishwa na utendaji kazi wao baada ya kukuta changamoto nyingi katika wilaya ya Mbarali huku wakishindwa kuchukua hatua sahihi kuzitatua, ikiwemo kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusiana na utekelezaji na uendeshaji miradi ya maji.
Amesema wananchi wa Wilaya ya Mbarali wana kero nyingi kuhusiana na huduma ya maji huku wasimamizi wakishindwa kuwahudumia badala yake wakitoa taarifa zilizo tofauti ukilinganisha na uhalisia wa hali iliyopo, jambo linalokwamisha jitihada za Serikali kutatua kero za wananchi.
Awali kabla ya kuchukua uamuzi huo, Mhandisi Mahundi alitembelea miradi ya maji ya mradi wa Lunduga-Mawindi, Uhamila na Ilongo Group na kukuta hali ni tofauti na maelezo aliyopata, miradi ikiwa haitoi huduma na utekelezaji umesimama kwa muda mrefu.