Amechambia mirinda nyeusi
Mbunge wa Jimbo la Kwela, Deus Sangu, ametangaza hadharani kuwa yuko tayari kutumia mbinu kali kushughulikia watakaothubutu kugombea ubunge katika jimbo hilo. Aidha, ametishia kuwashambulia na kuwaumiza watu wanaochapisha taarifa kumhusu kwenye mitandao ya kijamii.
Katika kauli zake, Sangu amedai kuwa yeye ni jasusi aliyefunzwa na serikali kupitia Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), akisisitiza kuwa mafunzo hayo anayatumia kuwazuia watu asiowataka kuingia au kushindana naye kisiasa ndani ya jimbo la Kwela.
Amedai kuwa kwa kutumia mbinu hizo, amefanikisha kulizuia jimbo hilo kugawanywa kinyume na mipango ya serikali na chama tawala (CCM), akisisitiza kuwa yeye pekee ana uwezo wa kulilinda jimbo hilo kubaki chini ya ushawishi wake kwa njia yoyote itakayohitajika.
Kauli hizo zimeibua taharuki miongoni mwa wananchi na wadau wa demokrasia, huku baadhi wakidai kuwa ni hatari kwa usalama na uhuru wa kisiasa katika eneo hilo.
Hiki ni kipindi cha fitna! Hiyo clip ni ya muda mrefu sana, kama sijakosea ni 2021.TISS mupo humu na mnasoma sana, toeni kanusho kuwa huyu pimbi Naibu Waziri Deus Sangu siyo mtu wenu!!
Sure wanazingua Tiss ni taasisi kama zilivyo nyingine kwanini ikubali kuchafuliwa na wanasiasa ambao kesho wapo kesho kutwa hawapoTISS mupo humu na mnasoma sana, toeni kanusho kuwa huyu pimbi Naibu Waziri Deus Sangu siyo mtu wenu!!
Si huwa nasikia TISS ukisema sema vitu kudhalikisha Idara unafichwa au unawekwa safe house, au hii ina baraka zao? Mbona kama ni jasusi ni mweupe sana kwa kichwa yaani hana nywele kabisa
mkuu kwamba 2021 inafanya uhalali wa upuuzi anao ongea huyo bwanaHiki ni kipindi cha fitna! Hiyo clip ni ya muda mrefu sana, kama sijakosea ni 2021.
Uchaguzi unakaribia, watu wanachafuana kuharibu reputation za watu.
Teeth wamejaza vilaza watupeTISS mupo humu na mnasoma sana, toeni kanusho kuwa huyu pimbi Naibu Waziri Deus Sangu siyo mtu wenu!!
Hiyo AI imejuaje mambo ya Bulgaria na kukata majimbo?Akisema sio yeye Bali AI imetengeneza sauti utabisha?
Kwani si watu wanaomfahamu ndio wameandika habari zake harafu wakaiita AI isome Kwa sauti.Hiyo AI imejuaje mambo ya Bulgaria na kukata majimbo?
Kama imejua yote hayo basi tumekwisha.
Imebidi nitazame angani ila sijaona 🌙