Naibu Waziri Mkuu majukumu yake Kikatiba ni yapi? Wafahamu waliowahi kuwa Manaibu Waziri Wakuu nchini

1. Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa anatakiwa atambue kwamba "AKUFUKUZAE HAKWAMBII TOKA"
2. Katiba Mpya nchini Tanzania kwa sasa siyo tu ni jambo la muhimu sana kuwepo bali sasa limekuwa ni suala la lazima kuwepo, "kwa gharama yoyote ile"
 
Watanzania hawajaridhika na Mkataba. Hii teua tengua sio Suluhisho.....
"serikali Ina namna mbili tu..
1. Kiheshimu hofu na maoni ya wananchi kwamba hawajaridhika na suala hili, au
2. Kuwapuuza wananchi na kuendeleza na suala hili.

Lakini wapime madhara ya kila uamuzi watakaoifanya"

Mapinduzi yapo mlangoni mwako. Chaguo namba (1)
 
Biteko akili nyingi na dhamira ya kweli
 
Kwanza Majukumu yake yameshaelwzwa kwenye barua ya Uteuzi.

Pili sheria inaweza badilishwa kama Kuna Changamoto

Mwisho Kwa Mujibu wa Katiba inamruhusu Rais kuunda nafasi yeyote anayoona inafaa.

Katelephone apumzishwe ni ana taka au hataki anamkwamisha mama.
 
Samia ni hakika sasa ameona mambo yanamuelemea kwenye serikali anayoiongoza, amechanganyikiwa, sasa anaonekana wazi hata wale aliowaamini mwanzo, hawaamini tena, amegundua wanamwangusha, mfano wao ni Jan. Makamba.

Hao japo wana kasoro zao, lakini tatizo kubwa kabisa linaanzia kwake, hataki kujisumbua, sio mfuatiliaji wa mambo, anaongoza serikali kwa mtindo laini sana, japo kuna wakati anakuwa mkali, lakini kwa waliomzoea, wanamuona anaigiza tu.

Na hii teuzi ya Naibu WM imekuja kwa sababu ipi? hamuamini Majaliwa? au ameona Majaliwa anazidiwa? au ameamua kupunguza nguvu ya Majaliwa aliyeonekana kama Rais hasa kwenye lile sakata la mgomo Kariakoo? au ameamua tu kukipeleka Kanda ya Ziwa ili kutafuta uungwaji mkono?

Nikiyatazama haya mabadiliko ya baraza la mawaziri aliyofanya Samia kwa ujumla wake, naona dhahiri kichwa kinamuuma, anatafuta watu wapya wa kuwaamini, at the same time hataki kuwakwaza wale aliowaamini mwanzo wakamwangusha, pia anataka kurudisha imani kwa wale anaoona hawamuamini tena, kwa sababu za kikanda na kidini.
 
Hapa staki kuongea sana kwa sabu sielewi mambo ya Kisheria

Naongelea hii nafasi aliyopewa na kuteuliwa mh Dotto Biteko kuwa Naibu waziri mkuu, sjawahi kuisikia na wala kuona tangu nchi yangu ipate uhuru

Hii inamaana gani? Ni mh Rais kuogopa kulivunja bunge kwa kutokumtengua waziri mkuu?

Au lipo kikatiba?

Tafadharini Waheshimiwa sana viongozi wetu meza kuu Maadimin wetu Jf

Msiunganishe huu uzi
 
Nimeona hata Rwanda kipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…