Naibu Waziri mteule wa Madini, Francis Kumba Ndulane ashindwa kusoma kiapo kwa ufasaha, uteuzi wake watenguliwa

Naibu Waziri mteule wa Madini, Francis Kumba Ndulane ashindwa kusoma kiapo kwa ufasaha, uteuzi wake watenguliwa

Mtu hajawahi hata kukaimu ukuu wa idara, ghafra bin vuu unampa cheo ambacho hakutarajia. Uzoefu ni muhimu hata ukiwa msomi. Si aibu kwa mshindwa kuapa tu, hata kwa mteuzi.
Unaandika kama vile unamjua kila kitu, sometimes sio lazima kucomment kama huna taarifa za kutosha.
 
Ameshatenguliwa tayari,waallah uchawi upo,hicho kipapai alichopigwa ni kiboko
Hiyo aibu najaribu kuvaa viatu vyake naona havienei kabisa.Ndugu jamaa na familia utawatizama vipi.
Hakuna uchawi hapo huyo mtu hana confidence hilo ndio linafanya ashindwe kusoma.
 
Hii sasa ni kali.



Awali Naibu waziri wa fedha ilibidi arudie kula kiapo zaidi ya mara 5 kwa sababu sehemu iliyoandikwa "Baraza la Mawaziri" yeye alitamka " Baraza la Mapinduzi"

Kali ya mwaka ni huyu Naibu waziri wa madini Francis Ndulane ambaye amekuwa akisoma kiapo huku akitetemeka na hivyo kuwekwa pembeni ili waapishwe wengine.

Wakati wa hotuba yake Rais Magufuli amesema atateua Naibu waziri mwingine wa madini baada ya Francis kufeli kula kiapo.

Sijajua manaibu waziri hawa wana mchecheto gani!

Maendeleo hayana vyama!

Niliwaona wakila kiapo utadhani watoto wa chekechea,aibu yetu Watanzania.Wamesifiwa kuwa ni miongo mwa wabunge makini zaidi ya 350 ambao Mheshimiwa amepewa na NEC hadi anashindwa kuteua.
Gwajima alimwamshauri kuwa teua yeyote na atakuwa vizuri,kiko wapi sasa?Swali linakuja,Askofu alikuwa anafikiria nini?Alikuwa anawadhihaki kina Daniel Awaki,Kasheku Musukuma au Lusinde?
 
Problem sio hajui kusoma bali problem ni kukosa confidence.

Wale wanaopiga, kudhalilisha na kutukana watoto wao kama walilazimishwa kuzaa hayo ndio matokeo yake.

Hapo sio kucheka bali kujifunza mtu mwenye elimu kama hiyo hawezi kushindwa kusoma.
 
Hao wengi ni wachumia tumbo. Ndio maana hawaweziona vitu vya rohoni. Kwahiyo usisumbuke nao; hawana chochote cha Kiungu. Si ajabu hata wao wanamtegemea Shetani kusukuma mambo yao!
 
CCM wote wanategemea nguvu za giza
mimi sijui ila siwapendi wanao tegemea nguvu za giza maaana huwa hawafanyi kazi zao kwa kutegemea uwezo wa taaluma zao bali hutegemea nguvu za giza ndio maaana mara nyigi hawajiamini
 
Dunia duara ukifikiri Sana utalia kila Mara, mheshimiwa Ndulane amekuwa mhasibu Tanroads zaidi ya miaka 10, amekuwa mkurugenzi wa mji wa ifakara, amekuwa Kiongozi wa mpira Lindi na Morogoro, amekuwa mjumbe wa TFF ktk kamati ya fedha na uongozi na amesafiri na Taifa Stars zaidi ya Mara 4, leo ameshindwa kuapa kurasa moja, hii ndiyo Dunia, tunatakiwa kutafakari kwa kina kabla ya kumhukumu
Kuwa mkurugenzi na mhasibu wa Tanroads sio hoja,hoja alileta tija gani kwenye taasisi,
Kikwete amekuwa Raisi kwa miaka 10,lakini ni kwenye uongozi wake ambapo tulishuhudia wizi,ufisadi wa kutisha,EPA,escrow,Meremeta,Richmond,
 
Hao wengi ni wachumia tumbo. Ndio maana hawaweziona vitu vya rohoni. Kwahiyo usisumbuke nao; hawana chochote cha Kiungu. Si ajabu hata wao wanamtegemea Shetani kusukuma mambo yao!
Nimekuelewa mkuu!
 
Back
Top Bottom