Naibu Waziri mteule wa Madini, Francis Kumba Ndulane ashindwa kusoma kiapo kwa ufasaha, uteuzi wake watenguliwa

Naibu Waziri mteule wa Madini, Francis Kumba Ndulane ashindwa kusoma kiapo kwa ufasaha, uteuzi wake watenguliwa

Yaa inawezekana, maana niliona clip alienda vizuri tu hadi mwisho, kumalizia ile 'ee Mungu nisaidie' sijui kilitokea nini wakamwambia arudie.
Alikuwa anakwama kusema " .....katika nafasi ya Naibu waziri wa madini"
 
Dunia duara ukifikiri Sana utalia kila Mara, mheshimiwa Ndulane amekuwa mhasibu Tanroads zaidi ya miaka 10, amekuwa mkurugenzi wa mji wa Ifakara, amekuwa Kiongozi wa mpira Lindi na Morogoro, amekuwa mjumbe wa TFF katika kamati ya fedha na uongozi na amesafiri na Taifa Stars zaidi ya Mara 4, leo ameshindwa kuapa kurasa moja, hii ndiyo Dunia, tunatakiwa kutafakari kwa kina kabla ya kumhukumu.
Embu enlarge, bold and underline hapo penye "amekuwa mhasibu Tanroads zaidi ya miaka 10".

Kumbe ndiyo maana!
 
Hii imetokea leo ambapo naibu waziri Fransis Ndulano alishindwa kusoma vizuri hati ya kiapo akapewa nafasi ya kurudia bado akawa anakwamakwama hadi akaambiwa akakae kwenye kiti chake. Sijui ataapa siku yingine au ndio kibarua kimeota nyasi. Sasa sijui ni uoga au wamemroga.
Fundisho:
Tuwafundishe watoto wetu kujiamini pamoja na elimu walizo nazo confidence ni muhimu.
Huyo karogwa tu na mpinzani wake maana alikuwa na machungu jamaa alikwua wa tatu lakini nidye kachaguliwa😎😎😎😎 joking!
 
Hii imetokea leo ambapo naibu waziri Fransis Ndulano alishindwa kusoma vizuri hati ya kiapo akapewa nafasi ya kurudia bado akawa anakwamakwama hadi akaambiwa akakae kwenye kiti chake. Sijui ataapa siku yingine au ndio kibarua kimeota nyasi. Sasa sijui ni uoga au wamemroga.
Fundisho:
Tuwafundishe watoto wetu kujiamini pamoja na elimu walizo nazo confidence ni muhimu.
Pressure ilimpanda ghafla kwani hakuwahi kumuona rais Magufuli live tena kakasirika. yabidi kusamehewa tu, in due time atapata tu confidence.
 
kipapai...jini lilishika sauti kwa muda!! ongopa sana sayansi ya ulimwengu usioonekana.
 
nimejiskia vibaya nimeumia zaidi eti nafasi yake kapewa mtu mwingine

lile halikua kosa la kumpokonya mtu nafasi yake,hata kama angetakiwa kupokonywa

basi asingepokonywa sasa,wangesubiri hata akianza utendaji kazi uteuzi wake ndio utenguliwe.

kilichofanyika sio jambo la kibinadamu,sio uungwana sio utu kwangu mimi sijaafiki alichofanyiwa (kutenguliwa)

Morning Speech mashuleni tulikua tunajikojolea assemble achilia mbali kuongea,unameza vitu ila ukienda mbele vitu vinapotea.

Presentation chuo ndio kabisa,kwahyo swala la ndugu yangu mimi niseme tu namuachia MUNGU.
 
Hii sasa ni kali.



Awali Naibu waziri wa fedha ilibidi arudie kula kiapo zaidi ya mara 5 kwa sababu sehemu iliyoandikwa "Baraza la Mawaziri" yeye alitamka " Baraza la Mapinduzi"

Kali ya mwaka ni huyu Naibu waziri wa madini Francis Ndulane ambaye amekuwa akisoma kiapo huku akitetemeka na hivyo kuwekwa pembeni ili waapishwe wengine.

Wakati wa hotuba yake Rais Magufuli amesema atateua Naibu waziri mwingine wa madini baada ya Francis kufeli kula kiapo.

Sijajua manaibu waziri hawa wana mchecheto gani!

Maendeleo hayana vyama!

Tatizo lenu mnamchukulia poa jembe huyo. Aliweza kujieleza mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo, aliweza kupiga kampeni mbele ya umati na aliweza kuapa mbele ya bunge. Hamjastuka tu, kuwa jamaa amekataa kijanja sana hiyo kazi,
Mchukulieni poa tu, hamjamjua
 
Tatizo lenu mnamchukulia poa jembe uyo. Aliweza kujieleza mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo, aliweza kupiga kampeni mbele ya umati na aliweza kuapa mbele ya bunge. Hamjastuka tu, kuwa jamaa amekataa kijanja sana hiyo kazi,
Mchukulieni poa tu, hamjamjua
Sizitaki mbichi hizi sungura akagumia!
 
Kwani kiapo kile wanakariri?
Swali lako zuri linajibiwa na swali kwako, uliishawasikia mawaziri na manaibu waliotangulia katika awamu zote wakiapa viapo vyenye maudhui tofauti na vile alivyotakiwa kuapa Francis?.
 
Hii inaathiriwa na makuzi pamoja na mazingira ni ngumu kuibadilisha kwa haraka.
Hakikisha siku ya presentation usiwaangalie machoni bali waangalie kwenye nywele yaani juu ya vichwa hii itasaidia kidogo
Daaa kweli lakini O level nilikuwa vzr Kwenye debate nahisi nyeto ndo factors
 
Back
Top Bottom