Naibu Waziri wa Afya amuondolea madaraka Mkuu wa Idara Paul Koroso, aliyemjibu “Sijali lolote hata nikifukuzwa kazi”

Huyo katibu mkuu hajielewi ukiruhusu hili si kila mtu atamjibu bosi wake anavyotaka??
Jambo lilo sahihi ndio lifuatwe.
Kama kiongozi hakufuata utaratibu wakubwa wake wamuache aendelee na kufanya alivyofanya?

Naamini wote watakuwa wamepata maelekezo ya namna ya kuenenda katika kutekeleza majukumu yao.
 
Huwa nakushangaa wewe unayemuona Mollel wa maana. Hebu jipe muda uchunguze akili za Mollel.
 
Kweli Naibu Waziri hana mamlaka ya kumvua cheo mtumishi wa Serikali mpaka taratibu zifuatwe.
 
Mlivyo poyoyo mtachangia ht uzushi km huu? Katibu Mkuu hawezi kulumbana ua kuonesheana mabavu na Naibu Waziri, Huu ni uzushi na uongo.
 
Hiyo tabia ya kusema nimekufukuza kazi kuanzia sasa si mnaijua nani aliianzisha?
Wateuliwa wengi bado wanajisahau,lakini wanamjua aliyeanzisha udhalilishaji huu hayupo,na aliyepo hataki uonevu,udhalilishaji na kiki.
 
Wateuliwa wengi bado wanajisahau,lakini wanamjua aliyeanzisha udhalilishaji huu hayupo,na aliyepo hataki uonevu,udhalilishaji na kiki.
Mfano huyu Mollel mambo ya ujenzi amayajulia wapi mpaka amfukuze huyo mhandisi?
 
Katibu Mkuu atumbuliwe hafai kuwepo hapo na ameonesha insurbordination ya kiwango kikubwa.

Huwezi kuruhusu mtu wa chini kujibizana na waziri ukaona ni sawa kwa Sababu sio mamlaka ya naibu waziri.
Wewe hukusikia au umesahau issue ya Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro? Tena ilikuwa kipindi cha Jiwe na agizo la mkubwa zaidi ya Waziri. Mkurugenzi Mkuu TANROADS alikataa kumuondoa.
 
Na Leo kaenda kuwalob madiwani wa jimboni kwake waukatae mradi wa maji na kuagiza mkandarasi asakwe ili aje kujibu kwanini mabomba yanapasuka na kuvujisha maji huku akimwacha injinia wa maji wa wlaya aliyekagua mradi na kujiridhisha nje! Huyo naibu ni kibuyu!
 
Tatizo ni mawaziri na wakuu wa mikoa na wilaya wote wanataka kufanya kazi za kitendaji badala ya za kusimamia sera za chama chao.

Amandla...
 
Moleli alifutwa kwenye ulimwengu wa kiroho na Askofu Gwajima🐒
 
Sura ya Mollel huwa sielewi....pure hayupo sawa kichwani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…