Fine and dandy, I get the last word then.
Vema umekiri BOQ ni kichochoro cha kupitishia na chaka la kufichia wizi na uhujumu. Ndo maana umesema nikaishauri serikali BOQ iwe more detailed and specific kwenye suala kama la zege.
Hivi unapimaje au unahakikije kwamba zege limejengwa kwa kiwango cha 1:2:4 dash 14 mm aggregate ???? Tofali linapelekwa lab kupima compressive strength, zege linapimwaje ?
Tunataka kujua trip za kokoto na mchanga na cement na risiti za manunuzi.
Fundi akichepusha njia ya malori kwenda kwake anatengeneza smoking gun evidence za kumkamatisha.
Mkurugenzi wa Halmashauri Arusha kakutwa na malori kwenye saiti yake binafsi kwa sababu Mbunge wa Arusha alifatilia mpaka michanga na kokoto zinakuja site lori ngapi badala ya kusubiri kujengewa concrete specs za One Two Four dash 14mm aggregate.
Na mwisho, kama umeona kuna hoja ya kuishauri serikali iziangalie upya specs za BOQ basi hukupaswa kubeza na kunanga nilipokutaka utoe maelezo ya kina. Kunambia nikakae ana kwa ana na walimu na ma Surveyor wanieleweshe kwa sababu wewe huna muda ni dharau ya kutotaka kuhojiwa. Huna muda, umeandika ma page mangapi kwenye hii topic alone ? Hapa jamvini kila andiko linahojika, hatujali utaalam wako!
Na wahandisi wa Tanzania msiposimamiwa mnavuruga, na tutaendelea kuwakalia kooni. Mmechimba kishimo cha futi 2 mkakiita ni bwawa la milioni 200, Waziri Aweso kawakamata with your pants down. Crying shame on the profession.
Kongole naibu waziri wa afya Mollel, kongole mbunge wa Arusha Gambo, kongole waziri wa maji Aweso.
And above all else, rest in peace Pombe Magufuli, mlinzi wa mali ya umma aliyeasisi na kuendeleza mapambano dhidi ya shenanigans za mafundi wa nchi hii mpaka siku anakufa.