Naibu Waziri wa Afya amuondolea madaraka Mkuu wa Idara Paul Koroso, aliyemjibu “Sijali lolote hata nikifukuzwa kazi”

Naibu Waziri wa Afya amuondolea madaraka Mkuu wa Idara Paul Koroso, aliyemjibu “Sijali lolote hata nikifukuzwa kazi”

sasa mambo ya "hata mkinifukuza kazi sitajali"yanatokea wapi?

madhara ya kuongea sana mpaka unaonekana kuna maslahi unayalinda.
 
Wahandisi tunaonewa sana, kosa la Engineer mpaka sasa lijaliona bado,
Wanasiasa wanakurupuka sana
 
Chukulia mfano wa cement, cement mfuko Bei yake unajulikana mfano 42.5 ni 20000, alafu umenunuliwa kwa 30000. Hapo inahitaji uwe mtaalamu kujua kuwa Kuna wizi?

Aweso alienda kukagua bwawa lililojengwa kwa mil 200, hivi ilihitaji awe na uwezo wa kusoma BOQ kujua kuwa Kuna wizi umefanyika pale?

Tatizo kubwa tulilonalo waafrica wengi ni hili la kuona suala la kupiga ni kawaida. Ndio maana Hadi leo tupo hivi.
Ni cement ya wapi? Imenunuliwa wapi? Hivi unategemea mkandarasi anunue simenti bila kuweka faida yake, gharama ya kusafirisha n.k.? Na kwenye BoQ hamna kitu kama bei ya mfuko kwenye rates. Kinacholipiwa ni zege au tofali lililotumika kwenye mradi.

Gharama ya mradi inategemea quotation ya mkandarasi. Mkandarasi anaweka kiasi anachotaka alipwe kutokana na kazi hiyo na ni uamuzi wa mshitiri kumkubalia au kumkatalia. Gharama za utekelezaji za mkandarasi zinajengwa na vitu vingi, overheads zake, gharama ya kuleta vitendea kazi, hali ya eneo, ulinzi wa eneo, ujenzi wa stoo na ofisi yake na ya msimamizi, upatikanaji wa wafanyakazi ( kuna maeneo hupati kibarua baada ya mavuno na hivyo mkandarasi anatakiwa awalete kutoka sehemu nyingine), mahitaji ya mkataba ( advance payment bond, performance bond, bima, kupima vifaa, usafirishaji wa vifaa, uharibikaji wa vifaa wakati wa usafirishaji n.k.), ushindani ( ni makandarasi wangapi wa daraja linalotakiwa ambao wako tayari kuifanya kazi hiyo), gharama ya kuleta wasimamizi wa wake ( site agents, foremen n.k) n.k. Aidha, uhakika wa malipo ( serikali ina sifa ya kutolipa kwa wakati kwa hiyo mkandarasi makini ataweka pia gharama za overdraft zitakazomwezesha kukopa pesa ili atekeleze mradi). Sasa waziri atazijuaje zote hizi mpaka aseme kuna wizi umetokea? Na wizi uko wapi kama wewe ulikubali kumlipa kwa hiari yako? Hivi ukienda Shoppers Plaza ukanunua embe kwa shilingi 10000 halafu kesho yake ukakuta maembe yanauzwa shilingi 1000 Tandale, utawaita Shoppers wezi?

Hayo mambo ya bei ya mfuko wa simenti yanatokea kwenye Force Account au mikataba ambapo mshitiri anachukua jukumu la kutoa vifaa vyote vya ujenzi. Huko ndiko unaweza kulinganisha bei ya simenti ya kwa Mangi na ile iliyonunuliwa na Mwalimu Mkuu ambae mara nyingi hana experience ya ujenzi.

Hii tabia ya kujiona unajua kila kitu na kuendekeza unafik inatutia hasara kupita kiasi. Na kama mshitiri haridhiki na utendaji kazi katika mradi, mkataba umeweka wazi hatua anazopaswa kuchukua. Kumtupa jela sio mojawapo.

Amandla...
 
Kuna watu humu Wana matatizo ya akili. Mm napingana na serikali kwenye vitu vingi, lakini unawezaje kupinga Jambo Kama hili? Toilet paper holder kwa laki 5?? Alafu huyo mhandisi bado anajibu jeuri
Hivi unadhani toilet paper holder ya Duravit inauzwa shilingi ngapi?
Urinal ya kwa Mangi inaweza kuuzwa shilingi 100,000 lakini ukitaka ya Roca utalipa milioni mbili. Na hapo hujaweka gharama za usafirishaji, utunzaji site, fundi na faida ya mkandarasi. Ndio maana ni muhimu kusoma specifications kabla ya kuita watu wezi. Kwa upande mwengine hivi ukikuta mkandarasi ameweka bei ya chini kuliko gharama halisi, utadai aongezewe pesa ili asipate hasara?

Amandla...
 
Alitakiwa kufutwa Kazi kabisa, huwezi kuwa na watumishi wakaidi.Private sector hakunaga upumbavu kama huo..

Hayo ni majizi yameshaiba mali za umma Sana ndio maana unaona anakuwa jeuri.
 
Koroso, huyu sio mtu wa Mbeya kweli?

Raia wa kipande hiyo huwa hawaendeshwi kizembe
 
Tangu lini Naibu Waziri amekuwa na mamlaka ya kumtia mtu ndani? Au hata kumshusha cheo mtumishi wa umma? Tangu lini kumjibu vibaya kiongozi yeyote imekuwa kosa la jinai?

Hivi nani atamfungulia mashtaka huyo Injinia? Na hao ma dc na wengine wametajwa wapi katika mkataba? Kushirikishwa kwao ni privilege sio right. Wao kama wanataka iwe right, waiingize kwenye mkataba wa ujenzi kuwa msimamizi wa mradi atawajibika kwa DC na kamati zake.

Alipokosea injinia ni kwenye suala la Force Account. Yeye angeishia kusema tu kuwa Suma kazi imewashinda na atafutwe mkandarasi mwingine. Force account itumike kwenye ujenzi wa matundu ya vyoo na kuziba mashimo ya barabarani lakini sio kwenye miradi complex kama hospitali. Kwa kusema hivyo, nimeingia shaka na uwezo wake na huyo mwenzake wa mkoani.

Ila kwenye hili, amfungulie mashtaka Naibu Waziri kwa matumizi mabaya ya nafasi yake na kumuonea. Labda ndio yeye na wenzake watajifunza kuwa wao ni viongozi sio wanyapara.

Amandla....
Wote kwenye Utumishi wa Umma tukianza kuwajibu viongozi wetu hivyo itakuwaje?
Lazima kuwe na order ndani ya serikali katika utekelezaji wa majukumu yao.
Huyo ni wa kumuondoa kabisa. Unamjibuje mwajiri wako hivyo? Katibu Mkuu ndio mwajiri wizarani lakini na yeye yupo chini ya Waziri na Naibu wake. Ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa maadili wa hali ya juu.
Serikali sio familia ya Kambale kwamba kila mtu ana ndevu.
 
Uwanaharakati hauna nafasi ndani ya serikali. Kama wewe ni mwanaharakati kwa kuzaliwa, ondoka ndani ya serikali ukaanzishe NGO yako.
 
Koroso ni aina wanaume na wana taaluma wasioyumbishwa na figisu a wanasiasa upumbavu
 
Wote kwenye Utumishi wa Umma tukianza kuwajibu viongozi wetu hivyo itakuwaje?
Lazima kuwe na order ndani ya serikali katika utekelezaji wa majukumu yao.
Huyo ni wa kumuondoa kabisa. Unamjibuje mwajiri wako hivyo? Katibu Mkuu ndio mwajiri wizarani lakini na yeye yupo chini ya Waziri na Naibu wake. Ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa maadili wa hali ya juu.
Serikali sio familia ya Kambale kwamba kila mtu ana ndevu.
Hayo ya kuzingatia aina ya majibu yanayokufurahisha ndiyo yalitufikisha hapa.

mtu akipata ka cheo uchwara tuu tayari umekuwa baba.Embu muanze kuwa siriasi na maisha ya watu
 
Wote kwenye Utumishi wa Umma tukianza kuwajibu viongozi wetu hivyo itakuwaje?
Lazima kuwe na order ndani ya serikali katika utekelezaji wa majukumu yao.
Huyo ni wa kumuondoa kabisa. Unamjibuje mwajiri wako hivyo? Katibu Mkuu ndio mwajiri wizarani lakini na yeye yupo chini ya Waziri na Naibu wake. Ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa maadili wa hali ya juu.
Serikali sio familia ya Kambale kwamba kila mtu ana ndevu.
wenzetu huko waziri mkuu yuko anajambishwa na kupikwa kitimoto sisi huku tunakalia kulazimisha heshima ya kiungu.

huu upumbavu ndio unatukamatilia kwenye hili tope la umasikini
 
Jamaa Ni mwamba, kale ka Morel miyeyusho
Kimoleli kimesomea Mambo ya kinywa na meno, kichizi chizi fulani. Mzihangaike fatilieni historia yake mtaelewa, nyie wa vetting ebu fanyieni kazi hili acheni njaa mkasahau wajibu
 
Kimoleli kimesomea Mambo ya kinywa na meno, kichizi chizi fulani. Mzihangaike fatilieni historia yake mtaelewa, nyie wa vetting ebu fanyieni kazi hili acheni njaa mkasahau wajibu
Hakaendani kabisa na hiyo professional, watumishi wengi wangekuwa Kama huyo engineer dharau za wanasiasa zingeisha
 
Inawezekana ndugu Koroso amekosea kusema hivyo ila hawa viongozi wetu pia huwa hawana busara kabisa.....wanapenda kusema vibaya wenzao bila adabu as if wao ni malaika

Kama amesema hajali lolote hata akifukuzwa kazi ndio amsweke ndani?

Madaraka ni kuwa na hekima sio ubabe
Ajitafakari kwa maamuzi ya hasira
 
Back
Top Bottom