Naibu Waziri wa Afya amuondolea madaraka Mkuu wa Idara Paul Koroso, aliyemjibu “Sijali lolote hata nikifukuzwa kazi”

Approach aliyotumia waziri haipo sawa. Ila kuhusu watumishi kudhalilishwa nayo haipo sawa japo nao ni mabingwa wa kudhalilisha wananchi wenye shida
Pili ukweli usiopingika ni kuwa kwenye miradi hiyo Kuna wizi wa kutisha, waziri au kiongozi yoyote asipokua macho basi hakutakua na thamani ya pesa inayoonekana.

N.b
Wafanyakazi wengi iwe wa serikali au binafsi tuna uwizi Sana(Mimi nikiwemo)
 
Naibu Waziri hajamfukuza kazi kwasababu hana mamlaka hayo. Ila amemfuta "cheo". Cheo huwezi kukidai mahakamani au sehemu yoyote. Ni dhamana tu. Leo unapewa, kesho unanyang'anywa anapewa mtu mwingine.
 
Sina taaluma husika ila nampongeza Sana huyo engineer Kama yupo humu,nime judge kutokana na experience ya kuishi kwenye hi Nchi,wanasiasa Wana upuuzi Sanae
Engineer Hana dharau,amemaanisha anashikilia msimamo wake wa kitaalam na yupo tayari kuwajibika

NB
Kuna dalili ya kwamba engineer alitishwa kufukuzwa kazi asipokubaliana na hako ka (kipenyo)
 
Hebu tupieni kavideo tuone

Ova
 
Inawezekana ndugu Koroso amekosea kusema hivyo ila hawa viongozi wetu pia huwa hawana busara kabisa.....wanapenda kusema vibaya wenzao bila adabu as if wao ni malaika
 
Naibu Waziri hajamfukuza kazi kwasababu hana mamlaka hayo. Ila amemfuta "cheo". Cheo huwezi kukidai mahakamani au sehemu yoyote. Ni dhamana tu. Leo unapewa, kesho unanyang'anywa anapewa mtu mwingine.
Hana hata mamlaka ya kumfuta cheo. Kama ana hayo mamlaka basi anaweza kumpandisha cheo mtumishi yeyote wa umma. Mwenye mamlaka hayo ni Katibu Mkuu wake ambae ndie Mtendaji Mkuu wa Wizara. Na uamuzi wake unaweza kukatiwa rufaa katika Tume ya Utumishi. Watu hua hawakati rufaa kwa sababu mabadiliko hayo ya wadhfa yalikuwa hayaathiri mishahara yao. Lakini sasa kwa hii sheria ya Mwigulu, watu watakata tu rufaa.

Mawaziri sio watendaji katika wizara. Wao jukumu lao ni kusimamia sera za wizara.

Amandla...
 
Nadhani kanuni za utumishi wa umma/maadili kwa viongozi hajui
 
Chuo Kikuu cha Dar es salaam kiliheshimika kutokana na umahiri wa faculty yake ya Uhandisi na kimsingi miaka ile ya 1980 wahandisi ndio walikuwa Chuo

Eng Korosso heshima kwako!
 
Chuo Kikuu cha Dar es salaam kiliheshimika kutokana na umahiri wa faculty yake ya Uhandisi na kimsingi miaka ile ya 1980 wahandisi ndio walikuwa Chuo

Eng Korosso heshima kwako!
Mahiri kivipi hao wa Miaka hiyo kwani waligundua nini cha mainjinia labda?
 
Matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya watu wanaosimamia taaluma zao badala ya siasa za umagufulism
 
MOLELI NI KICHAA, ALIFANYA KAZI BABATI SHIDA, SELIANI ARUSHA SHIDA, YAANI HUYU NI CHIZI CHIZI KABISA...MAGUFULI ALIMGUNDUA HUYU NI CHIZICHIZI ANA UBARIDI KICHWANI ILI ATUKANE APAMBANE NA WAPINZANI IKATIKI.....NYIE MFATILIENI MTAJUA KABISA
 
Uko sahihi ndugu...

NW hakuwa na sababu na haki wala sababu ya kutoa uamuzi ule pale...

Kwa sababu kwa kiongozi makini naye akiwa ndiye boss wa wote wale wawili, alipaswa kujiuliza swali moja muhimu sana, kwanini hawa wahandisi wawili watofautiane wakati wote wanasimamia mradi mmoja uleule tena kwa tofauti ya figure kubwa ya fedha..?

Naye huyu Bwana Korosso sijui naye alikuwa na sababu gani tu ya ku - pre - empty maamuzi ya waziri..?

Mfano, hakuwa na sababu ya kumalizia maelezo yake kwa maneno; "........hata ukininufuza kazi..."

Hilo lilionesha dharau kwa boss wake japo boss naye ali - over react bure tu kiasi cha kutoa amri ile ambayo 100% haikuwa na umuhimu na ulazima...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…