Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,986
Approach aliyotumia waziri haipo sawa. Ila kuhusu watumishi kudhalilishwa nayo haipo sawa japo nao ni mabingwa wa kudhalilisha wananchi wenye shidaWewe Naibu waziri Mollel unataka wananchi wasiongee na wakuogope wakati unatumia nafasi uliyopewa vibaya na ovyo!. Mamlaka ya kumsweka ndani injia na kuamuru aondolewe kwenye nafasi yake uliyatoa wapi?. Unafahamu kuwa wewe ni mamluki na unaharibu image ya chama Cha mapinduzi?. Haujui kuwa wewe ni msaliti na ndiyo sababu uliwasaliti wananchi waliokuchagua pale ulipojiuzulu ubunge wa chama chako (CHADEMA) kilichokupa nafasi ukashinda Kisha ukakisaliti kwa kujiuzulu without any genuine reasons na ukabebwa sijui kwa mbeleko gani ukajiita mwanaCCM?. Watumishi wa umma kwa muda mrefu wamekuwa ni wahanga wa kudhalilishwa na wanasiasa na ni vema tabia hii mbovu na ya ovyo ikakemewa na kutokomezwa kabisa. Ni vema ukatumie nafasi uliyo nayo vizuri na utambue kuwa cheo ni dhamana.
Pili ukweli usiopingika ni kuwa kwenye miradi hiyo Kuna wizi wa kutisha, waziri au kiongozi yoyote asipokua macho basi hakutakua na thamani ya pesa inayoonekana.
N.b
Wafanyakazi wengi iwe wa serikali au binafsi tuna uwizi Sana(Mimi nikiwemo)