Naibu Waziri wa Afya amuondolea madaraka Mkuu wa Idara Paul Koroso, aliyemjibu “Sijali lolote hata nikifukuzwa kazi”

Naibu Waziri wa Afya amuondolea madaraka Mkuu wa Idara Paul Koroso, aliyemjibu “Sijali lolote hata nikifukuzwa kazi”

Approach aliyotumia waziri haipo sawa. Ila kuhusu watumishi kudhalilishwa nayo haipo sawa japo nao ni mabingwa wa kudhalilisha wananchi wenye shida
Pili ukweli usiopingika ni kuwa kwenye miradi hiyo Kuna wizi wa kutisha, waziri au kiongozi yoyote asipokua macho basi hakutakua na thamani ya pesa inayoonekana.

N.b
Wafanyakazi wengi iwe wa serikali au binafsi tuna uwizi Sana(Mimi nikiwemo)
Ndyo kwenye miradi Kuna ujambazi na wizi Mkubwa Sana kiongozi. Sisi tunataja approach nzuri ya kushughulika na wote wanaohusika kwa wizi wa Mali ya umma na sio matamkwa ya wanasiasa yanayoumiza wananchi wakati akina mollel wanaendelea kutafuna keki ya taifa kila uchwao!.

Leo mafuta ya kula hayashikiki, mafuta ya kuendesha mitambo Bei juu, nafaka bei juu na hakuna mwanasiasa yeyote anaeonesha mikakati madhubuti ya kunusuru wananchi dhidi ya kadhia hii. Kila uchwao ni matamko matamko matamko matamko na matamko ya akina Ummy Mwalimu ambayo yanaumiza Sana wananchi wa kawaida.
 
MOLELI NI KICHAA, ALIFANYA KAZI BABATI SHIDA, SELIANI ARUSHA SHIDA, YAANI HUYU NI CHIZI CHIZI KABISA...MAGUFULI ALIMGUNDUA HUYU NI CHIZICHIZI ANA UBARIDI KICHWANI ILI ATUKANE APAMBANE NA WAPINZANI IKATIKI.....NYIE MFATILIENI MTAJUA KABISA
Huyu si ndio alisema ana ushahidi kuwa Chadema walimpiga risasi Tundu Antipas Lissu? Au mwengine?

Amandla...
 
Approach aliyotumia waziri haipo sawa. Ila kuhusu watumishi kudhalilishwa nayo haipo sawa japo nao ni mabingwa wa kudhalilisha wananchi wenye shida
Pili ukweli usiopingika ni kuwa kwenye miradi hiyo Kuna wizi wa kutisha, waziri au kiongozi yoyote asipokua macho basi hakutakua na thamani ya pesa inayoonekana.

N.b
Wafanyakazi wengi iwe wa serikali au binafsi tuna uwizi Sana(Mimi nikiwemo)
Waziri atagunduaje wizi katika mradi wa ujenzi kwa kikao cha siku moja? Mtu ambae hata hajui kusoma Contract documents haswa BoQ, michoro na Specifications?
Unakuta msimamizi analalamikiwa kuwa kitasa kinapatikana kwa mpemba kwa shilingi 40,000 lakini yeye anamlipa mkandarasi shilingi 100,000. bila kuangalia aina ya kitasa na kujua tofauti kati ya rate iliyomo kwenye BoQ na bei ya dukani!

Amandla...
 
Ndyo kwenye miradi Kuna ujambazi na wizi Mkubwa Sana kiongozi. Sisi tunataja approach nzuri ya kushughulika na wote wanaohusika kwa wizi wa Mali ya umma na sio matamkwa ya wanasiasa yanayoumiza wananchi wakati akina mollel wanaendelea kutafuna keki ya taifa kila uchwao!.

Leo mafuta ya kula hayashikiki, mafuta ya kuendesha mitambo Bei juu, nafaka bei juu na hakuna mwanasiasa yeyote anaeonesha mikakati madhubuti ya kunusuru wananchi dhidi ya kadhia hii. Kila uchwao ni matamko matamko matamko matamko na matamko ya akina Ummy Mwalimu ambayo yanaumiza Sana wananchi wa kawaida.
Alafu sahv ni wakati wa mavuno
Na vyakula bei juu
Je ikifika Nov itakuwaje

Ova
 
Uko sahihi ndugu...

NW hakuwa na sababu na haki wala sababu ya kutoa uamuzi ule pale...

Kwa sababu kwa kiongozi makini naye akiwa ndiye boss wa wote wale wawili, alipaswa kujiuliza swali moja muhimu sana, kwanini hawa wahandisi wawili watofautiane wakati wote wanasimamia mradi mmoja uleule tena kwa tofauti ya figure kubwa ya fedha..?

Naye huyu Bwana Korosso sijui naye alikuwa na sababu gani tu ya ku - pre - empty maamuzi ya waziri..?

Mfano, hakuwa na sababu ya kumalizia maelezo yake kwa maneno; "........hata ukininufuza kazi..."

Hilo lilionesha dharau kwa boss wake japo boss naye ali - over react bure tu kiasi cha kutoa amri ile ambayo 100% haikuwa na umuhimu na ulazima...!
Heshima inapaswa kuwa kwa pande zote. Unaweza kukuta Waziri alitoa vitisho vya kufukuza mtu kazi ndio maana Mhandisi akajibu alivyojibu.

Amandla...
 
hamnamo mtu humo, ni vile tu hii nchi kila mtu anaweza kua mtu yeyote, usije shangaa hata wewe mleta uzi jina lako linapitishwa kua inatakiwa uwe Rais wa nchi na kijiti unakabidhiwa,
u can't make even a 5 minutes convo n serious matter with him, sasa huyo ni mtu

Bora ata yule mlevi wa Tarime anakuaga na data na upstairs yuko vyema
 
Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel ameagiza kuondolewa madarakani kwa Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa wizara hiyo, Paul Koroso kutokana na mgogoro ulioibuka katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe unaotekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Sh2.9 bilioni.

Dk Mollel pia ameagiza Koroso aswekwe mahabusu akidai amemtolea majibu na lugha ya kijeuri kuwa “hajali lolote hata akifukuzwa kazi”.

Dk Mollel ametoa maagizo hayo Julai 5 akiwa mjini Nansio Ukerewe alipofika kutatua mgogoro uliobuka kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi hospitali ya Rufaa ya mkoa katika kisiwa hicho ndani ya Ziwa Victoria.

"Kutokana na changamoto zilizojitokeza kwenye mradi huu, Koroso utakoma kuwa mkuu wa Idara ya Ujenzi Wizara ya Afya. Katibu mkuu atamteua mkuu mpya wa idara ambaye atakuja kusimamia mradi wa Ukerewe," alitangaza Dk Mollel.

Pamoja na viongozi na wataalamu wa Wizara, mkoa na wilaya, kikao hicho pia kilihudhuriwa na viongozi wa CCM, halmashauri na mkandarasi Suma JKT.

Miongozi mwa malalamiko yaliyotolewa na viongozi wa Wilaya ya Ukerewe dhidi ya Koroso ni kutowashirikisha viongozi wa wilaya na halmashauri katika utekelezaji wa mradi huo.

"Ofisi ya DC, halmashauri na CCM Wilaya ya Ukerewe hawakushikishwa katika utekelezaji wa mradi huu," Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Kanali Denis Mwila alimweleza Dk Mollel.

Muda mfupi kabla ya amri ya kuswekwa mahabusu, Koroso alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa Serikali ingeokoa kati ya Sh180 milioni hadi Sh260 milioni iwapo ungetekeleza mradi huo kwa mtindo wa Force account (kutumia nguvu za wananchi) badala ya ukandarasi.

Kiwango kilichotajwa na Koroso kilitofautiana na kiwango cha Sh600 milioni kilichotajwa na mhandisi wa mkoa wa Mwanza, Chagu Nghoma.

Kutokana na tofauti hiyo, Dk Mollel akamtaka Koroso kutoa ufafanuzi, ndipo akasisitiza kuwa hesabu zake ndizo sahihi kwa mujibu wa kanuni na msingi wa kitaaluma na kwamba yuko tayari kuchukullwa hatua yoyote.

"Mheshimiwa Naibu Waziri, kiwango nilichotaja kimezingatia kanuni, vigezo na hesabu za kitaaluma; nitaendelea kusisitiza hilo hata kama ukinifukuza kazi sitajali," alisema Koroso.

Kutokana na kauli hiyo, Koroso aliyeketi jirani na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Wilaya ya Ukerewe akajikuta anawekwa chini ya ulinzi na kupelekwa mahabusu.

Chanzo: Mwananchi
Madaraka ya kumuweka raia mahabusu bils amri ya mahakama anayayos wspi naibu waziri?
 
Utakuwa mjinga wa karne,MTU aache taaluma atumikie siasa? Na wewe unajiita msomi....fwakini kabhisa!
Watu kama nyie ningekuwa nawasweka ndani mka nyee debe...

Huu upumbavu wenu hapa chini Ndio taaluma sio?👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220706-202936.png
    Screenshot_20220706-202936.png
    109.4 KB · Views: 8
Injinia kaonyesha yeye siyo njaanjaa,kasema yuko tayari hata kufukuzwa.Huo ndiyo utaalamu wenyewe,Mollel kajikosha tu.
Kwani nani ana shida ya shibe yake? Hao mnaowatetea wanawapiga pesa zenu afu mnakenua tuu kama mandezi wapumbavu nyie..

Kwamba hiki hapa chini Ndio utalaamu sio? 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220706-202936.png
    Screenshot_20220706-202936.png
    109.4 KB · Views: 8
Kuna namna ya kuwajibishana kistaarabu kwa watu wenye nyadhifa za juu ila sio kwa huo upuuzi alioufanya huyo naibu waziri wa kuaibishana na kudhalilishana. Mbona raisi hana swaga za kishamba kama huyo naibu waziri. Naibu waziri nae atumbuliwe mana bado ana element za sifa za kijinga za awamu iliyopita.
 
Sijaona kosa la Koroso , Waziri alitakiwa aseme wazi kwamba kosa la Koroso ni lipi na uchunguzi ufanyike kubaini kama alifanya makosa sasa mtu anakujibu kwamba hawezi kubadilisha kauli maana ana uhakika na anachokiongea hata kama kitagharimu kazi yake unasema kakujibu vibaya

Ubabe hauna tija Waziri
 
Waziri atagunduaje wizi katika mradi wa ujenzi kwa kikao cha siku moja? Mtu ambae hata hajui kusoma Contract documents haswa BoQ, michoro na Specifications?
Unakuta msimamizi analalamikiwa kuwa kitasa kinapatikana kwa mpemba kwa shilingi 40,000 lakini yeye anamlipa mkandarasi shilingi 100,000. bila kuangalia aina ya kitasa na kujua tofauti kati ya rate iliyomo kwenye BoQ na bei ya dukani!

Amandla...
Chukulia mfano wa cement, cement mfuko Bei yake unajulikana mfano 42.5 ni 20000, alafu umenunuliwa kwa 30000. Hapo inahitaji uwe mtaalamu kujua kuwa Kuna wizi?

Aweso alienda kukagua bwawa lililojengwa kwa mil 200, hivi ilihitaji awe na uwezo wa kusoma BOQ kujua kuwa Kuna wizi umefanyika pale?

Tatizo kubwa tulilonalo waafrica wengi ni hili la kuona suala la kupiga ni kawaida. Ndio maana Hadi leo tupo hivi.
 
Watu kama nyie ningekuwa nawasweka ndani mka nyee debe...

Huu upumbavu wenu hapa chini Ndio taaluma sio?[emoji116]
Kuna watu humu Wana matatizo ya akili. Mm napingana na serikali kwenye vitu vingi, lakini unawezaje kupinga Jambo Kama hili? Toilet paper holder kwa laki 5?? Alafu huyo mhandisi bado anajibu jeuri
 
Back
Top Bottom