Naingia Shambani very serious kulima Alizeti

Naingia Shambani very serious kulima Alizeti

Mkuu nenda kalime...
Experience is the best teacher...
Kapate uzoefu huko, hapa wengi wanakatisha tamaa tu nadhani wengi ni wafanyakazi wa kusubiri month end ( broilers)..
Watu wanalima na wanafanikiwa, kwanini sio wewe..
Wakati naanza kujenga nilkuwa natembelea sana jukwaa la ujenzi, wengi wanaandika vitu hawavijui, unaweza usijenge hata usinunue tofali, nimeingia field nimejenga na nimehamia...
Walopokaji wengi sana humu..nenda huko huko na pia ukifanikiwa komaa huko huko ukileta mrejesho pia watasema ni uongo

Kiongozi umeongea ukweli mtupu kabisa. Hapa JF ukiwackiliza hao w mwisho w mwezi utaogopa kuanza kitu chako.
Kama ukileta dili una ambiwa mwizi mpigaji na ndio maana una kula kimya kimya tu.
Na mwisho umemaliza vzr mno mdau wangu.
Na huyu mtu kama ulivyo sema aingie mwenyewe kazini hakuna kuckiliza hao watu wanao tisha watu.
All the best
 
sikukatish tamaa ila Maisha hayajawah kuwa Rahis kias hicho...ni vyema uende ukalime kidogo kidogo huku ukiwa unapata uzoefu hata mtu aliesomea kilimo hawez kwenda ku invest kwa eka 50 kwa kuanzia tu
 
sikukatish tamaa ila Maisha hayajawah kuwa Rahis kias hicho...ni vyema uende ukalime kidogo kidogo huku ukiwa unapata uzoefu hata mtu aliesomea kilimo hawez kwenda ku invest kwa eka 50 kwa kuanzia tu
Haya ndio mambo yanayotufanya wabongo tubaki maskini wa kutupa. Ushauri wa hovyo kabisa huu. Badala ya kumpa mikakati ya jinsi ya kupambana na changamoto,watu wanamtisha na kumtaka akimbie chagamoto.
Mwaka huu wakati napanga kuingiza mi70,nikashirikisha jamaa hapa ofisini akaanza kunitolea mifano ya watu walioshindwa. Nikamuiliza anitajie biashara moja iliyonyooka bila tone la challenge. Akabaki kujiuma uma tu. Nikamshauri angejikita kunishauri namna ya kupambana na challenge sio kunikatisha tamaa.

Kifupi Mayu ushauri mzuri utapewa na wakulima serious na wataalam wa kilimo. Sio waswahili na watu wa mitandaoni. watu wazuri hata humu wapo,mimi walinishauri nikafanyia kazi leo hii sikosi laki 8+ na zaidi kwa siku
 
Wakuu
Binafsi huwa na Bet sana na bahati nzuri nimemuotea muhindi kama M 40
Na sasa nataka kubet kwenye kilimo

Mwaka huu naingia shambani kweli kweli sio utani, naingia FRONT na sio simu
Nakwenda kulima ekari 50 za alizeti MBUGANI kisha nikitoa naweka dengu
Eneo SINGIDA kwetu kabisa

Matumizi (makadirio ya juu kabisa) kwa ekari 50

[emoji117]Kukodi shamba m 2.5
[emoji117]Kulima shamba m 2.5
[emoji117]Kupanda m 1
[emoji117]Kupalilia shamba m 2.5
[emoji117]Mbegu lk 7
[emoji117]Uvunaji/upakiaji m 2
[emoji117]Mengineyo m 2

Jumla milion 13.2
Jumlisha hidden cost jumla iwe milioni 15

MAVUNO (makadirio ya chini)

Eka moja gunia 7 badala ya 15 za wataalamu
Ekari50 x Gunia 7
Jumla inakua gunia 350

Wastani gunia moja hutoa mafuta dumu 2 bei makadirio ya chini sh elf 50 kwa dumu( dumu linakwenda hadi laki+)

350 x 2 inakua dumu 700
Dumu700 x elf50 unapata Sh M35
Hapo nime assume mashudu yamelipia gharama ya ukanuaji

JUMUISHO
M35 -M15 = M20 Faida

DENGU

Ukitoa tu alizeti unavizia nvua za mwishoni kabisa unalima dengu shamba hilo hilo hulipi gharama za kukodi tena

[emoji117]Kulima m 2.5
[emoji117]Mbegu m 2
[emoji117]Kupanda lk 5
[emoji117]Madawa (emergency) m2
[emoji117]Kuvuna/kupakia 2m
[emoji117]Mengineyo m 1
Jumla m 10
Hidden cost m 2
Jumla m 12

MAUZO
Wastani gunia 4 kwa eka badala ya gunia 8 hadi 10 kwa eka za wataalamu

Ekari50 x Gunia 4 unapata gunia 200
Gunia la dengu lina wastani wa sh Laki 1

Laki 1 x gunia 200 unapata M 20

JUMUISHO
M20 - M12 = M8 Faida

FAIDA KUU (alizeti na dengu)
M20 +M8 = M28

NB
Nimeweka makadirio ya juu sana kwenye matumizi
Na nikaweka makadirio ya chini sana kwenye mavuno na bei

Dua zenu jamani

Ntaleta MREJESHO iwe nime Lost au nime Win
Mayuuuu uweee nzua wakukembetee
 
Mkuu, Alizeti Gunia la Debe Saba Makadirio mazuri ni Lita 20 tu sawa na Dumu moja. maana hapo nimeona unasema itakupa Dum mbili sawa na lita 40 ambacho hicho kitu hakina uhalisia sana kwa sababu nimelima sana Alizeti,Huko jirani na Singida maeneo ya Kondoa pale
 
Nasikia mbegu zimeanza kutolewa kwa wakulima uwe umejiandikisha jina lkn pia utalipia 7000 kwa kilo 2 kwa Dodoma.
Ndo hizi.... Serikali wametoa kwa ruzuku. 7000 kwa kg 2 badala ya 35000
IMG_20211107_160708.jpg
 
Haya ndio mambo yanayotufanya wabongo tubaki maskini wa kutupa. Ushauri wa hovyo kabisa huu. Badala ya kumpa mikakati ya jinsi ya kupambana na changamoto,watu wanamtisha na kumtaka akimbie chagamoto.
Mwaka huu wakati napanga kuingiza mi70,nikashirikisha jamaa hapa ofisini akaanza kunitolea mifano ya watu walioshindwa. Nikamuiliza anitajie biashara moja iliyonyooka bila tone la challenge. Akabaki kujiuma uma tu. Nikamshauri angejikita kunishauri namna ya kupambana na challenge sio kunikatisha tamaa.

Kifupi Mayu ushauri mzuri utapewa na wakulima serious na wataalam wa kilimo. Sio waswahili na watu wa mitandaoni. watu wazuri hata humu wapo,mimi walinishauri nikafanyia kazi leo hii sikosi laki 8+ na zaidi kwa siku
nami nishauri kitu mkuu walau nianze dunduliza taratibu nithubutu ndugu... Nitashkuru 🙏
 
Be very careful my friend huu usimu mwaka huu mpaka mwakani bado haujasomeka kabisa, mvua zinaweza kuwa chache sanaa ukakuchukia kilimo.
 
Kwahiyo bei ya hysun 33 ni sh ngap?..mbona kila mtu na bei yake
 
Back
Top Bottom