Najaribu kufikiria kama tungewapambanisha Samia, Magufuli na Lissu leo ungemchagua nani?

Najaribu kufikiria kama tungewapambanisha Samia, Magufuli na Lissu leo ungemchagua nani?

Nafahamu fika Hayati John Magufuli hatarudi duniani. Hata hivyo, kulingana na wanavyomjadili wabaya na wapenzi wake na yale yote mazuri na mabaya aliyotenda kama binadamau, bado tuko naye kiroho kama siyo kihistoria.

Katika kuwa-assess viongozi wetu walio hai ili wajue hisia zetu na wajirekebishe au kuongeza ufanisi, kama leo ingetokea tukawapambanisha watatu hawa katika kinyang'anyiro cha kumsaka anayefaa kutuongoza na kulinda raslimali zetu, ungemchagua nani.

Kumbuka hii ni hypothesis inayolenga kuwapa tahadhali na somo viongozi wetu. Twende kazini.

View attachment 2693542
Nobody in the bucket fits to outshine Dr. JPM; he was a unique, visionary, firm on what he believed would benefit the ordinary citizens.
 
he jamani tunakosa mawazo hata,tufikiri kuwapambanisha viongoziwetu
 
Lissu - Kidogo busara imepita pembeni. Zaidi hatakuwa na uwezo wa kuwadhibiti Wakaskazini na ukabila wao.

Magufuli -
Hakuna mzuri kwa maisha ya mtumishi wa umma. Aliwafanya kama maadui. Hakupandisha mishahara wala ongezeko la mshahara. Waliishi maisha ya dhiki mbaya zaidi kupitia bodi ya mikopo aliwadhulumu Kwa Riba inayozjizaa. Hakuajiri,Kuna balaa kubwa ya wasomi mitaani. Ni chaguo la wavivu walioamua kujiita wanyonge!

Mama Samia.
Kwa !
Maslahi ya utumishi...lile deni losiloisha la bodi ya mikopo Sasa limerudi kwenye uhalisia. Nalipa na mategemeo ya kumalizika ni hakika. Madaraja nimepanda,ongezeko la Kila mwaka angalau ni kiduchu nimeliona. Ajira zinatangazwa. Kwa maisha yangu ya utumishi kuna tumaini la maslahi!
 
Nafahamu fika Hayati John Magufuli hatarudi duniani. Hata hivyo, kulingana na wanavyomjadili wabaya na wapenzi wake na yale yote mazuri na mabaya aliyotenda kama binadamau, bado tuko naye kiroho kama siyo kihistoria.

Katika kuwa-assess viongozi wetu walio hai ili wajue hisia zetu na wajirekebishe au kuongeza ufanisi, kama leo ingetokea tukawapambanisha watatu hawa katika kinyang'anyiro cha kumsaka anayefaa kutuongoza na kulinda raslimali zetu, ungemchagua nani.

Kumbuka hii ni hypothesis inayolenga kuwapa tahadhali na somo viongozi wetu. Twende kazini.

View attachment 2693542
Magufuli...
 
Back
Top Bottom