Najiskia kuwa mnyonge, na moyo wangu umebondeka sana. Eehh Mungu nitie nguvu

Mzee si ufungue nini kinachokusibu huenda hapa kuna mtu alishapitia the same exactly na jaribu na akapata njia so funguka mtoto wa kiume
Itoshe kusema tu, asante kwa maoni yako mkuu. Ipo siku yaja nawe utajiskia kama nilivyo jiskia mimi na hata familia yetu ilikua ikinitazama mimi ili nitende jambo lakini haikuwezekana.
Unapo barikiwa kupata mahitaji ya kukidhi familia, pia ukajitunzia akiba kwaajili ya kusaidia familia.... kisha siku moja ukapata maumivu pamoja na familia, wakati huo maumivu hayo yakahitaji maombi ama faraja..... then ninaamini utakuja kuelewa ninacho maanisha.
 
Asante kwa maombi na faraja mkuu, Mungu akutunze na akubariki wewe na familia yako pamoja na uzao wako...🙏
 
Pole sana mdogo wangu, nini shida?
Mungu akufanyie wepesi katika mambo yako.
 
Umenipa neno kubwa sana katikati ya maoni yako, sina hakika kama umeliweka kwa bahati mbaya ama lahh.... lakini kwakifupi umenikumbusha jambo la muhimu sana na umenijenga hata nimejiskia kuimarika.
 
Pole sana brother...
Kila lenye mwanzo halikosi mwisho....
Kikubwa ni kuuombea huo mwisho uwe mzuri....
 
Yesu...🙊
 
Pole sana
Nini shida??
Mmepatwa na nini??

You're in my prayers.
Mungu awavushe[emoji120][emoji120][emoji120].


Bwana awainulie Nuru za uso wake na awape Amani[emoji120]
Maombi yako yamekua msingi imara zaidi kwenye hili jaribu letu, na hakika Mungu atatutetea kwakua yeye ni muaminifu sana.
 
Mungu aliweka Summer, Autumn, Spring na Winter.
Na kila kipindi hapo kina raha na machungu yake.
Kuna kipindi tulipitia wakati mgumu saana kama familia, ulipoisha niligundua ya kwamba kilikuwa ni kipindi bora sana ktk maisha yetu kama familia.
Fikiri tungeishi summer au winter throughout all the year, maisha yangepoteza msisimko wake.
Hivyo hivyo na katika maisha yetu ili yawe na ile thamani lazima magonjwa yawepo ili ujue thamani ya afya, njaa ili ujue thamani ya shibe, kukataliwa ili uijue thamani ya kukubalika nk
 
Mnaosema Mungu anapitisha watu kwenye majaribu sidhani kama mnashauri vyema..

Labda mnafanya Counselling ya psychotherapy.

Mungu akupitishe kwenye majaribu ili uteseke?

Mungu akupe majaribu, kwamba yeye hajui Nia yako hadi akupime kwa majaribu?

Majaribu yote na shida zote hutokana na dosari za kibinadamu
 
Upo sahihi mkuu, and all of those are the meaningful of life.
Lakini pamoja na hayo yoote, maumivu bado hayaepukiki mkuu
 
'Nami nikasema nilikua kijana na Sasa ni Mzee, sijawahi kuona mwenye haki ameachwa wala watoto wake kutangatanga barabarani'

Pole sana Komredi Mungu ni mwaminifu ni suala la muda atawavusha salama.
Muhimu msisahau kushukuru kwa kila jambo.
Asante chief
 
Pole, usiache kumtegemea Mungu

soma Zaburi 9:10, ishi hapo....
Muombe Mungu tu na mizimu ya kwenu ila usimuomba kwa kupitia Uislam na Ukristu.....hutofanikiwa kamwe. Fikiria wewe ni mbongo unamuomba Mungu kwa kupitia Wataleban na Wayahudi, wapi na wapi.....inakuja kichwani kwako kweli hii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…