I'm so sorry brother.
Katika maisha kwa ujumla wake kila kitu kina pende mbili , upande usio mzuri na upande ulio mzuri .
Ukiweza kulifamu hilo hakuna hali yoyote itakayo kusumbumbua sana kwa vile wakati haudumu.
Kuna wakati unakuwa kwenye mazuri , huo wakati haudumu, unakuja wakati unakuwa kwenye mabaya, nao haudumu, hivyo unapokuwa kwenye wakati wowote uzingatie saa yoyote uta change kuelekea wakati wa namna nyingine.
Sote hatupendezwi na chochote kisicho tupa furaha, ndio maana huwa tunauzingatia sana wakati mbaya.
Binafsi huwa nadhani ni ile kukumbushwa nawe uwe unajali yoyote anaepitia changamoto kwa vile nawe kuna wakati utapitia changamoto na utatamani kupata hata mtu wa kukufariji.
Kwa ujumla pole ndugu, shika sana kuvumilia, jaribu pia kupuuza yale yasio na muhimu sana ambayo yaweza kuwa sababu moja wapo ya kukosa furaha, lakini pia unaweza ukafanya kitu kama kumtembelea mtu mwenye changamoto ili kumtia moyo, inaweza kuwa mfungwa gerezani, mgonjwa hospitali, ama yatima au mzee au mhitaji yoyote, au kwenda kwenye nyumba ya ibada hapo ukasali si kwa kujiombea wewe bali wengine, toa kabisa kujiombea wewe na familia bali fanya hivyo kwa wengine.
Na kuhakikisha ndugu yangu
Ushimen kama ukifanya hivyo asubuhi jua halita zama kabla hujarelewa na amani, ukifanya hivyo jioni asubuhi haitafika kabla haujarelewe na furaha .
Yote ya yote Mungu asimame nawe ndugu yangu.