Najuta kumtia umasikini Mama yangu

Kwaio wewe ndo ulimpa mama yako umasikini ??
Kama ulikua na uwezo wa kumpa umasikini bas na uwezo wa kumpa utajiri pia unao.
 
Hata mimi ninaunga mkono kwamba bora angeitoa tu mimba yako kwasababu ya upumbavu ulio nao. Kama umezaliwa 90 mwanzoni ina maana wewe ni mtu unatakiwa uwe na familia kabisa. Unavyosema hadi sasa hivi mama yako anakupambania INASHANGAZA SANA. Kilichonikera zaidi ni uliposema umesoma. Mama yako pamoja na majanga yake alitimiza wajibu wake kwa 100% wewe ndo unamletea ushenzi. Neno langu la busara kwako ni kuwa uache upumbavu na pambana ujitegemee badala ya kumtegemea mama yako. Hivi vijana mliozaliwa Dar mna shida gani?
 
Hudhuni = huzuni. Kwa uandishi huu utapata wapi kazi? Kama 75% ya maisha yako unamtegemea mama si bora tu uolewe?
 

😅😅

We nae😀
 
Mimi naona tofauti, emotionally hauko matured, na hii inaweza kuwa sababu ya kuzaliwa na kulelewa na emotional immature parents. Tafuta namna ya kukomaza hisia zako kwanza ndipo utaweza kusamehe, kujisamehe na kukubali kilichotokea na kuamua kuanza mapambano upya.

Je wajua kuwa mtoto yatima, au yule aliyekulia mtaani anaweza kuwa amekomaa kihisia kuliko mtoto mwenye wazazi wote wawili au mzazi mmoja? Hii ni kwasababu wazazi wengi kuna muda tunashindwa kuficha hisia zetu kwa watoto hasa zile hisia hasi (Huzuni, hasira, maumivu, addictions zilizopitiliza etc). Watoto naturally wanafeel wanachofeel wazazi wao bila wazazi kujua na hii huleta athari kwa mtoto kama hizi.

Key take aways: Vijana kabla hatujaamua kuleta watoto duniani tujipime kama tuko tayari kihisia, ili tuweze kulea na kuwakuza in a functional environment. Watoto wengi wana struggle na mambo ambayo hata hawajui yamewafikaje, mbaya zaidi hayashikiki, yangekuwa yanashikika wangeweza kuyavua wakakimbia.
 
Huyu ndg yetu inaonekana amelelewa na mama peke yake, bahati mbaya zaidi akalelewa kimama (huenda akawa ni mtoto wa pekee) kwahyo amekuja kushtuka akiwa amechelewa kidogo😀

Princes, Kijana wa kiume hutakiwi kulaumu kitu kama hicho, yaani unatamani mama angetoa mimba😳😳

Umasikini haujaanzia kwako wala kwa mama yako, kuna watu ni maskini ukiwaona hitojitambua kama masikini tena ila wao wameridhika na hawana wa kumlaumu..

Pamoja na hayo si kila aleyesoma alipata kazi mwaka 90 sio mbali kihivo.. kwani wangapi ni wasomi wazuri lakini hawana kazi? Huwaoni??

Huenda mama yako hata bila kubeba mimba asingepata kazi na maisha yangeenda tu na hivyo ndivyo ilikuwa, kwani pamoja na kutoajiriwa; aliwezaje kukulea na mpaka sasa umesema unamtegemea kwa kiasi kikubwa na bado wewe unamzidi elimu, anawezaje?
 
Kwa hiyo humjuwi baba'ko?
 
Yupo na Bado wanaishi pamoja...anafanya kazi serikalini yupo na cheo Cha sita kutoka chini🤣🤣🤣 japo amebakiza nusu mwaka astaafu...!
 
Sijaelewa umemtia umasikini vipi mama yako?

Kimsingi kauli hiyo ingetoka kwa baba yako ama mama yako mwenyewe ingemake sense...wao ndio wamefanya mchakato wa wewe kupatikana

Enwei,endelea kupambana,kujuta haikusaidii kitu
Asante kipenzi. Nakupenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…