Nakukumbusha Waziri Makamba, kama tuliweza kuileta crane yenye tani 70 tushindwaje tani 26?

Nakukumbusha Waziri Makamba, kama tuliweza kuileta crane yenye tani 70 tushindwaje tani 26?

Ni Wapi January ,alikaa na kuacha Alama chanya ya kazi Yake ??


January Makamba, Hajawahi kufaa kua kiongozi wa kuaminiwa .


Na kwa uongo wake huuu wakudhan Watanzania wote ni Wajinga..

Kila mmoja amemjua ni MTU wa Aina Gani.


Huyu MTU, yeye alipoteuliwa tu. Ndo Mashine zikaanza kuharabika, Umeme ukawa wa Ovyo..


Tukisema JK ndio anaongoza, Tunakosea???.
Mkuu hakika umenena
 
Nafikiri sio crane za kawaida, naamini waziri hawezi kudanganya nchi nzima, serikali yooote na bunge loote.
effco plant and crane hire mbona wapo pale kitambo na wana crane zakutosha sio hao tu wapo wengi pale
 
ulichosema ni sahihi effco plant and crane hire mbona wapo pale kitambo na wana crane zakutosha sio hao tu wapo wengi pale
 
Hivi effco plant and crane hire na wengineo wanafanya nini pale JNHPP na midude yao ile?
Au ndio Show off?
 
Mimi ni Mhandisi Christopher Bitesigirwe Mratibu wa Mradi wa JNHPP. Nimekuwa pale kwenye mradi kwa muda wa zaidi ya mwaka na ni Mtaalamu wa Mitambo. Kuna aina nyingi ya crane na kila crane inatengenezwa kwa kazi maalum. Kuna crane zinazotembea (movable cranes) na crane zinazofungwa mahali (immovable cranes).

Crane itakayofungwa pale kwenye handaki la kuchepusha mto (diversion tunnel) ambayo ni immovable crane imetengenezwa pamoja na gate la kufunga handaki la kuchepusha mto.

Lile gate lina vipande 14 ambavyo vina uzito wa tani 26 kila kimoja. Na vitaunganishwa vipande 7 kwa kila nusu gate lenye uzito wa tani 182. Hivyo crane itakayotumika kufunga gate kwa jina la kitaalamu inaitwa hoisting mechanism ambayo itakuwa inabeba vipande vya gates kwa ajili ya kuviunganisha na kushikilia. Baada ya kufunga gate, litamwagwa zege la kuimarisha gate hilo ambalo litakaa pale wakati wote (permanently).

Kwa kuwa crane hiyo imetengenezwa mahususi kwa kazi ya kuziba handaki la kuchepusha mto, baada ya kazi hiyo kukamilika crane hiyo haitakuwa na kazi tena.

Crane hiyo tunayoiongelea bado haijafika nchini na itakapofika ndio tunaweza kuanza kazi ya kuziba handaki la kuchepusha mto (diversion tunnel).
 
Iko siku ... Siku isiyojulikana kwa sasa, itakapofika viongozi wote wanaofikiri kuwa watanzania ni watu wasioelewa vitu vya msingi hadi kupelekea kiongozi kusema uongo hadharani tena kwa kujiamini wakati akijua kuwa anadanganya, wananchi watafanya maamuzi. Hivi nani aliamini kuwa mwamba Saddam Hussein siku zake za mwisho kwenye utawala wake angeishi shimoni kama panya? ....

Madaraka na mamlaka yatokayo kwa wananchi na kukabidhiwa kwenu viongozi, ni sawa na koti au kanzu ambayo wakati ukifika utaivua tu!!. Zitumieni nafasi mulizoaminiwa kwazo kwa busara na hekima huku mkijua kuwa malipo ni hapa hapa Duniani....

Duuu...umeme umekatika mara mbili wakati nikiandika bandiko langu hili...🤔 😳
 
Mwakani nagombea ubunge kupitia ssiem japo moyoni sinao, wataenda kunijua bungeni. Nikijiridhisha bunge au waziri analidanganya bunge lazima achezee makofi ya maana live. Najua ukiwa bungeni una kinga
 
Ina maana Adio yako mkubwa ni makamba pekee mbona mambo ya ajabu
Ukiamka Makamba
Ukilala Makamba
Ukigeuka Makamba
Mbona hawasemi mbolea ni Elfu 95 saiv au hawaoni kila kitu Makamba
Umequote wrong

Makamba ni Waziri mchapakazi

Soma Uzi vizuri, umekurupuka
 
Amejibu swali kiboya sana. Nilikuwa namuona ana maana kumbe hamna kitu. Kwanza iweje ujibu kwa kutumia maneno "inasemekana"?? Taarifa za kujaza maji mwezi Novemba si suala la inasemekana, bali ni taarifa iliyotolewa na serikali yenyewe kupitia mtangulizi wake. Ni jambo la ajabu nchi nzima kukosa crane ya tani 26, unless Ange specify labda aina hiyo ya crane ni unique. Yaani sio uwezo wake katika uzito bali aina yake. Kea kifupi. Huyu kijana kumbe mweupe sana.
Utamuitaje kijana wakati ana miaka 47?
 
Kaka kimahesabu tu.hyo milango Ina tani 26.
hao waturuki Wanaojenga reli Wana winch ya kubeba tani 40 na kitu.
Hii pia unataka uone picha?
hilo bwawa la nyerere.samia akifanya masikhara linakufa bila kuwaka umeme.
Bora life tu kwani hatutapoteza kitu. Miradi yote ya CCM Ife. Hii nchi inasonga Bila hata serikali. Ni misaada kutoka kwa mabeberu NDIO uhai wetu baas Bila wao hatuwez savaivu. Ife tu huo mradi migesi sijui mimwendo kasi mibarabara UCHWARA yote Ife tu haina misaada. Akina zinja binadamu wa awali waliishi Maisha bora hata kutuzidi sisi wenye mibarabara UCHWARA, mireli UCHWARA ya SGR , migesi UCHWARA, mimwendo kasi UCHWARA, midege UCHWARA, mihospitali UCHWARA haina dawa inajengwa kwa ajili ya wengine mimahakama UCHWARA yenye mijaji UCHWARA. Mungu angamiza wote let gharika fyeka NO MERCY. WATU WAMEPORWA HELA ZAO, WAMEPORWA WAKE ZAO, WAMEBOMOLEWA NYUMBA ZAO, WAMEULIWA NDUGU ZAO. WASTAAFU MAFAO YAO YAMEDHULUMIWA. ALMIGHTY GOD SORT US AND WIPE THEM ALL.
 
Back
Top Bottom